Hatujamtendea haki Bi.Shakila

Hatujamtendea haki Bi.Shakila

Ngwananzengo

JF-Expert Member
Joined
Jul 28, 2012
Posts
1,911
Reaction score
1,315
Taarifa za msiba wa Bi Shakila zilianza kama tetesi lakini baadae ikaja kuthibitika kuwa hatunae tena. Bi Shakila Saidi alikuwa ni mwanamuziki mahili, mkongwe na hodari katika miondoko ya taarabu aliedumu kwa Muda mrefu. Kuna mengi ya kuandika na kusimulia juu ya kazi ya kutukuka aliyoifanya kwenye tasnia hii. Itoshe kusema Bi Shakila alikuwa ALAMA ya muziki wa Taarabu.

Kilicho nifadhaisha na kunitia Simanzi ni jinsi taarifa hii ilivyopewa uzio "mwepesi" kwenye vyombo vya habari pamoja na mitandao ya kijamii.
 
Hata mimi nilisikitika sana sana, mama huyo alitoa mchango mkubwa katika sanaa ya nyimbo za taarabu ambazo zilikuwa za staha na siyo mipasho.

Mtu ungetegenea Taifa letu hasa Wizara husika walao wangemuenzi kwa kitu fulani hivi kama kumbukubu ya mchango wake baada ya uhuru na kipindi chote cha Serikali ya awamu ya kwanza - Bi Shakira alikuwa amejaliwa sana kwa upande wa sauti na jinsi alivyo kuwa anaji-conduct akiwa jukwaani - R.I.P Bi Shakira utakumbukwa na wengi.

Tunashindwa na Taifa kama Misri ambalo linamkumbuka sana mwana taarabu wa miaka ya 1920s Bi Um Kuluthum (sijui kama nimepatia) au Wahindi na Latah Mangeshkar na wenzake!!
 
SI Mnaona Olympic games imekuwaje ? tumekuwa wa mwisho duniani...wana spoti wa nchi nyengine walitayarishwa na kupewa motisha ili kuleta heshima ya ushindi. Kenya wenzetu wamefanikiwa kupata medali zaidi ya 13 ...sisi zero....
hawa wasanii kina Bi Shakira wameimba sana nyimbo za amani na uzalendo..wametumika sana leo Nape kimya utafikiri aliekufa yule adui wao wa serikali 3 Jumbe...maana jumbe serikali huku bara hata bendera walishindwa kushusha nusu mlingoti...
 
TANZANIA =HAPA KAZI TU!!
Late Shakira alisababisha niupende muziki wa taarabu hasa = 'macho yanacheka lakini moyo unauma' alikuwa ni celebrity , maana hata wazungu walikuwa wanakata ticket kuja kumuoina. nakumbuka miaka mingi kidogo ila sina specifi year. kuna mzumgu alifanya safari makusudi kumtafuta shakira. na alipomuona na akamsikiliza live akasema ' now I can die peecefully'
poleni wafiwa.
 
TANZANIA =HAPA KAZI TU!!
Late Shakira alisababisha niupende muziki wa taarabu hasa = 'macho yanacheka lakini moyo unauma' alikuwa ni celebrity , maana hata wazungu walikuwa wanakata ticket kuja kumuoina. nakumbuka miaka mingi kidogo ila sina specifi year. kuna mzumgu alifanya safari makusudi kumtafuta shakira. na alipomuona na akamsikiliza live akasema ' now I can die peecefully'
poleni wafiwa.

Mkuu yaani wimbo huo nikiusikia mwili unisisimuka sana, sijui kwa nini??

Ukisikia vyombo vilivyo pangiliwa, kila hala inasikika vizuri sijui waliu-record studio gani? Kikundi hicho cha taarabu kutoka Tanga kilikuwa moto wa kuotea mbali 'real pro' ukiongezea sauti ya Bi Shakira iliyo fanana ya kinanda mtu mpaka unasahau kama kuna kifo Duniani - siyo utani.
 
kizazi cha leo kinaangalia wenye meno ya dhahabu!! shakila kwa TZ ni sawa na akina whitney Haustona ama Mikaeli Jackson walivyokuwa na umaarufukwao, walienziwa , lakini wapi hapa TZ, Angalia tu Olympic Majirani kenya wamezoa medali za klutosha!! tanzania sana sana tunaambulia wa tano!!!!!! sijui tumerogwa wapi na nani!!! we dont care michezo sanaa na wa wachezaji ama wasanii!!!!! HAPA KAZI tu Ndiyo twajua kwa mwendo kasi!!!!!!
 
kizazi cha leo kinaangalia wenye meno ya dhahabu!! shakila kwa TZ ni sawa na akina whitney Haustona ama Mikaeli Jackson walivyokuwa na umaarufukwao, walienziwa , lakini wapi hapa TZ, Angalia tu Olympic Majirani kenya wamezoa medali za klutosha!! tanzania sana sana tunaambulia wa tano!!!!!! sijui tumerogwa wapi na nani!!! we dont care michezo sanaa na wa wachezaji ama wasanii!!!!! HAPA KAZI tu Ndiyo twajua kwa mwendo kasi!!!!!!

Uzubaifu na kuendekeza siasa, Shakira angekuwa mwana siasa saa hizi sio sifa hizo, wanacho sahau ni kwamba mama huyu alikuwa anatoa mchango sana wakati wa Chama cha TANU in terms of kuhamasisha raia kutokana na nyimbo zake zenye staha.

Chukulia Wakenya - wanawakumbuka sana wasanii wao na wana riadha maana wanajua hao ndiyo wanalitangaza Taifa lao Kimataifa, na kusema kweli Serikali yao inawajali sana, sisi kwetu hapa wakina Filbert Bayi, Nyambui, Kamanya, Mwanjala nk wala hawakumbukwi na wengi ni masikini hawakufaidi chochote kwa uzalendo wao - je attitude za viongozi wetu kuhusu masuala ya sanaa na riadha inaweza kuzalisha bingwa yeyote nchini? tutabaki wasindikizaji tu, unakuta kwenye Olympic au Commonwealth games officials kutoka Tanzania ni wengi kuliko Wachezaji au wana riadha always self centered na hawajali chochote - si wanarudi kutoka Olympic sasa wasikilize visingizio watakavyo toa - Watanzania mabingwa sana kwa misamiati na zuga zuga kila kitu tunawaza "DEAL" i.e officials wana angalia watafaidika vipi, mambo ya msingi wao wanayachukulia ni secondary.

Juzi juzi hapa nilikuwa natafuta KAMUSI YA KINGEREZA to KISWAHILI kwenye mtandao baada ya kui-download nakuta nembo ya bendera ya Uingereza na nembo ya bendera ya Kenya which means wenzetu ndiyo wanataka watambulike kama ndiyo mabingwa wa kiswahili Africa Mashariki wakati nchi yao ni watu wachache wanao jua kuandika/soma kiswahili fasaha - nilipo check kwa umakini zaidi nikaja gundua kwamba wamecopy kamusi ya kiswahili ya Tanzania wakajifanya niya kwao!!!

Kama nilivyo dokeza hapo juu si ajabu Kimataifa wao ndiyo wanajitangaza ni mabingwa wa kiswahili, Bill Gates naye alikuwa amedanganyika hivyo alikuja kushtukia ujanja huo juzi juzi tu hapa baada ya watu kulalamika kwamba kiswahili kilichomo kwenye app zake si kiswahili fasaha alikuwa ameingizwa mjini na wenzetu - Sisi hapa tuanendelea kuzubaa tu, wenzetu wana exploit weakness zetu to maximum!!
 
ulichosema ni kweli
Ndio maana Dr Magufuli ana kazi sana !!!! maana kila nyanjia ilioza!!! wakati mwingine namuonea huruma maana amtumbue nani amuche nani!!! kila kona kuna vimelea na ulaji na kutowajibika , sijui hii gene tumerithi wapi!!! ukanjanja ukanjaa tu!! angalia juzu tu hata marubaniu kwenda kuchukua ndege za ATC tayari akatumbukizwa mle asiye na sifa!! kila kona!!
hati miliki za wasanii wetu hakuna , wajanja wanazo master wanafyatua tu wanaingiza mpunga wakati akina late Shakira wanakufa hawna kitu! hasa hawa wazee ndio wanaumia sana , afadhali akina na diamond!!
 
Back
Top Bottom