Ngwananzengo
JF-Expert Member
- Jul 28, 2012
- 1,911
- 1,315
Taarifa za msiba wa Bi Shakila zilianza kama tetesi lakini baadae ikaja kuthibitika kuwa hatunae tena. Bi Shakila Saidi alikuwa ni mwanamuziki mahili, mkongwe na hodari katika miondoko ya taarabu aliedumu kwa Muda mrefu. Kuna mengi ya kuandika na kusimulia juu ya kazi ya kutukuka aliyoifanya kwenye tasnia hii. Itoshe kusema Bi Shakila alikuwa ALAMA ya muziki wa Taarabu.
Kilicho nifadhaisha na kunitia Simanzi ni jinsi taarifa hii ilivyopewa uzio "mwepesi" kwenye vyombo vya habari pamoja na mitandao ya kijamii.
Kilicho nifadhaisha na kunitia Simanzi ni jinsi taarifa hii ilivyopewa uzio "mwepesi" kwenye vyombo vya habari pamoja na mitandao ya kijamii.