Hatujui kutengeneza matangazo lakini!

Hatujui kutengeneza matangazo lakini!

Ebana lile la Hallow Mpenzi ndio tupo Kona ya Mwisho hapa! hivi bado lipo Sijatizama kitambo Local Channel.

Me matangazo niliyokuwa nayapenda :-

1.La ITV--- Hebu Tueleze Siri ya Mafanikio Yako... Mtoto wa Kiiraqw anajibu Sio Siri Ni Revola tu Jamaa anauliza Revola Peke Yake? cute anajibu ''Ndio Kwani Mwasho ni Laini na Huniweka Fresh Mchana Kutwa...

2.Lile la Salama Condom... japo si lilikuwa ni la Kenya au Tz? Salama changuo la kisasa!!!!!! Mpya bora kwa bei nafuuu..!!!!

Hivi kuna anae likumbuka la Ntindilititindilo Cafenol ni Bora haina asprin peke yake, hupunguza maumivu ya kichwa homa mafua na Fluu, Cafenol ni dawa bora hushinda Maumivu.. imeshinda zingine zote, Cafenol ni dawa namba One Cafenol Cafenol bambaaa!

Kuna La Relova Revola Revola Revola.....revooola ah Sabuni Mpya
 
Kwa kweli Wtz hutujui kutengeneza matangazo ya biashara lakini nimeliangalia tangazo la Simtank ambalo limemshirikisha mchekeshaji Ramadhani Mwinshehe 'Kingwendu' kwa kweli nimelikubali pamoja na kasoro zake chache. hebu nawe sema chochote kuhusu hili au macho yangu yana makengeza!

Tatizo letu wabongo hatutaki kutoka nje ya boksi.. Matangazo mazuri nearly 99% unayoyaona kwenye TV zetu yametengenezwa na watu wa nje wabongo wachache sana wenye uwezo wakutoa concept za maana na kuzigeuza kuwa visuals.. Hata hilo tangazo la Simtank wametengeneza wahindi wa Pilipili entertainment wtz walienda tu kusaidia kushika taa na kuunga waya..
 
ukiangalia lile la Vita Foam hutakaa ununue hilo godoro milele. linatapisha
Nitakushitaki umeiba kero yangu!LOL yaani lile tangazo huwa najiuliza wenyewe wakikaa wanafikiri nini? na hujui kama wanatangaza godoro au kingine !
 
Mtoa mada anasema "HATUJUI KUTENGENEZA MATANGAZO" akimaanisha matangazo ya kibongo na ametaja tangazo la Kingwendu sasa mtu unapotaja tangazo la EPIQ au TUPO WANGAPI na kadhalika, je hayo yametengenezwa na wabongo ? Tusome mada na kuielewa ndipo tuchangie. Tutaje matangazo yaliyotengenezwa na kampuni zetu za kibongo ili tutoe CREDIT.
 
Matangazo Tanzania ni mgogoro. Fikiria lile tangazo la Sharobaro na wazazi wake wamekuja kumpokea airport halafu wanafika home na kasanduku. Kwanza nyumba na waishio bonge la contrast.
Halafu sijui kinywaji arrrgghhh

Haya lingine lile la Airtel Money Sharo na Majuto kama sikosei. Huyo Sharo domo upande sijui ndio swag, haya!
halafu eti King Majuto anapewa bila KUKATWA ( By the way the kukatwa thing huwa inanipelekeaga mawazo ya maji taka.. nahisi kama kuta....) . halafu eti anapigiwa matarumbeta.

Njoo la godoro eti anapiga makalio ya mkewe kama basi sijui Tandika Gongolamboto.

Mwisho magodoro gani sijui yule dada anasema yana walantii kadi! what the heck! Pheeeewwww!

Lakini ndio hivyo tunaishi na watu wanakula kamisheni zao
 
Hakuna tangazo nnalolichukia kama lile la Bambo la godoro, hasa anapojirusha kitandani kama taahira.
 
tangazo ni lile la zantel epic nation bana......hawa wengine wanachekesha tu

Kwa kweli lile ni katika matangazo bora ya mwaka huu, sina uhakika kama lina mpinzani, mengi ukiyaangalia ni lazima uchafukwe na roho
 
Ebana lile la Hallow Mpenzi ndio tupo Kona ya Mwisho hapa! hivi bado lipo Sijatizama kitambo Local Channel.

Me matangazo niliyokuwa nayapenda :-

1.La ITV--- Hebu Tueleze Siri ya Mafanikio Yako... Mtoto wa Kiiraqw anajibu Sio Siri Ni Revola tu Jamaa anauliza Revola Peke Yake? cute anajibu ''Ndio Kwani Mwasho ni Laini na Huniweka Fresh Mchana Kutwa...

2.Lile la Salama Condom... japo si lilikuwa ni la Kenya au Tz? Salama changuo la kisasa!!!!!! Mpya bora kwa bei nafuuu..!!!!

Hivi kuna anae likumbuka la Ntindilititindilo Cafenol ni Bora haina asprin peke yake, hupunguza maumivu ya kichwa homa mafua na Fluu, Cafenol ni dawa bora hushinda Maumivu.. imeshinda zingine zote, Cafenol ni dawa namba One Cafenol Cafenol bambaaa!

Kuna La Relova Revola Revola Revola.....revooola ah Sabuni Mpya

na lile la kiwi... Heeeebuu jitoookeeeeze, simaaaama,..jioonyesheeee... Mbele za watuuuuu...
 
na lile la kiwi... Heeeebuu jitoookeeeeze, simaaaama,..jioonyesheeee... Mbele za watuuuuu...
Haha hilo pia nalikumbuka hadi midundo yake oi

Unalikumbuka na lile la General Tyre? Sauti ya Mtu mzima haswa akiimba Tyre general kutoka Arusha..... Tanzaniaaaa

Pia Kula La ''Oko'' Vipi Rambo aaah Pancha Bwana.. Pancha wakati kuna Oko?
 
kuna la protex la zamani kweli, We omari, Kazi kujikuna tu ngwaara ngwara, em peleka chai. then omari anadondosha vyombo. bosi anamaind "Omariii"

Na yale ya fanta ya zamani. kuna mshkaji anaitwa Fred, msanii kweli.
 
''Kule hakusomeki Meeen!..............NIMEHAMIA!'' hahahahahahahahahahahaaaaa!
 
kuna la protex la zamani kweli, We omari, Kazi kujikuna tu ngwaara ngwara, em peleka chai. then omari anadondosha vyombo. bosi anamaind "Omariii"

Na yale ya fanta ya zamani. kuna mshkaji anaitwa Fred, msanii kweli.

Omary ilikuwa noma mpaka Diamond saundo wakatungia na rap. Ila ndugu hiyo username yako mmmhhh..
 
Back
Top Bottom