Hatuna Forensic Science digrii/diploma Tz?

Hatuna Forensic Science digrii/diploma Tz?

Hapo kwenye Red inagharimu kweli kweli,nakushauri hata ukiisoma mkuu USIENDE BOT(BENKI KUU YA TANZANIA).Wanajua wenyewe,sijui ni kwanini ni waoga hivyo.

Hao wana tatizo,Mirror-Imaging .Kuna theory moja inaitwa cognitive Trap ya mwanainteligensia aliyebobea anaitwa Heur.He said - one must understand [the foreign leaders'] values and assumptions and even their misperceptions and misunderstandings. ... Too frequently, foreign behavior appears "irrational" or "not in their own best interest.

Kwa wale wanaotafuta vyuo kwa level ya Diploma au kuandaa mazingira ya Ph.D in governance, ukipata vyuo vizuri kama Mercyhurst College Institute for Intelligence Studies (MCIIS). Hiki kiko Pennyslevania,US na Brunel UK ni vyuo vizuri sana

Maneno kwamba ww ni mwanausalama yatakuandama sana ktk harakati zako za kisiasa hata kama hayana ukweli. Watz tunawaogopa sana watu hawa wakati kazi pekee wanayofanya ni kulinda viongozi wa magamba. Ni jukumu lako kueleza ukweli ili kupambana na propaganda hzo.

Kuhusiana na topic, ktk kupambana na uhalifu kisayansi, tupo nyuma kama miaka 60 ukilinganisha na mataifa yaliyoendelea. Yaani ukiangalia Medical detectives-on etv ndo unaelewa tupo nyuma kiasi gani. Wakati hapa hatuna hata kozi za diploma, kwa USA forensic experts ni PhD holders with years of experience. Nilisikitika sana kwa jinsi 'serial killer' wa bongo (miezi kadhaa iliyopita) alivyokuwa anatafutwa 'manually'. Mpaka leo kimya, naona wanasubiri aue tena.
 
Forensic nadhani ni kubwa sana Bila hata chuo kuna watu kwa elimu waliyo nayo ya career nyingine wakipigwa msasa tu wanaweza kuboboboea zaidi kwenye specific forensic

Mfano Ofisi ya CAG prority zake ziko kwenye kukagua mahesabu ya kihasibu tu . Lakini kimtazamo wangu ofisi ya CAG inatakiwa kuwa na vitengo vya

  • ICT Audit - Hawa ni watu wenye ujuzi wa specifation ya mifumo ya kompyuta serikalini( tovuti, Database, Network ) kama inakidhi viwango na haina matatizo.
  • Engineering / Mechanical / Technical Audit
  • Education system Audit
So kwa mtazamo wangu kuwa forensic expert kama tayari una degree ya uhasibu, kompyuta , engineering na nyinginezo ni rahisi sana sabau ni kuongeza skill ndogo tu.

Kwa hiyo mwanakijiji nakushauri muulize kwanza anapenda kubobea kwenye forensic ya mambo gani.? ( Kompyuta, Uhasibu, mauaji ya silaha, etc). from there nadhani kidogo atakuwa emejisogeza kwenye forensic kwa mbali.

Otherwise kibongo bongo mwambie Atafute mambo ya Auditors ( Nadhani wana mitihani yao ya kimataifa ) Huo Auditrs ndio njia ya kueleka kwenye forensic kibongo bongo
 
Mimi ni mmoja wa wahitimu wa kwanza udsm aliyesoma kozi ya forensic chemistry. Wakati tunasoma hyo kozi tulikuwa na matumaini ya kuendelezwa zaidi kwa sababu aliyekuwa anatufundisha (dr ngasapa) alikuwa anatupa matumaini kibao.Baada ya sisi sidhani kama hyo kozi ipo tena na hata ile maabara iliyoanzishwa serikalini hata haifanyi kazi wafanyakazi wake huwa wanaenda kujikalia tu na kurudi hme na kusubiri mshahara
 
Mwanakijiji Forestic science inasomwa katika kada mbali mbali hapa Tanzania lakini siyo kwa ajili ya Intelijensia na Uchunguzi wa kubaini makosa na hivyo aiitwi kwa jina hilo, tunazo maabara; kuna mtu niliwai kukutana naye na sample moja anapereka nje ya nchni kufanya test ambayo inaweza kufanyika hapa Dar. UDSM Mlimani kitengo cha Biologia, Chemia, Engineering, SUA na Muhimbili wana masomo ambayo unaweza kuyageuza na kuyatumia kwa ajili Forestic na pia wana vifaa, kuna baadhi ya vyuo pia wanavyo ambavyo sitaweza kuvitaja leo kwa sababu vimevishau. Ni jina tu la Degree linaweza kuwa geni lakini mambo yakawa ni yaleyale.

Katika kesi yetu ya Tanzania muhimu hapa siyo elimu ya Forestic peke yake, maana watu wapo ingawa wachache, muhimu zaidi ni sheria yetu iitwayo "Evidence Law" ni lazima ijengwe upya kutamka na tambuwa aina ya ushahidi ambao ni wa lazima katika matukio kama hayo ambayo yanahitaji Forestic na pia iende mbali kubaini kazi itakayokubalika mahakamani itafanywa na idara gani na watu wenyewe elimu gani.

Nadhani tuna matatizo mengi katika sekta ya upelelezi kwa ujumla, ndio tuna hitaji hao uliowadhania lakini tatizo ni kubwa kuliko hapo, tunahitaji idara huru za Upelelezi wa makosa ya jinai ambazo hazitakuwa chini ya Polisi kama FBI hili polisi waache kubambikizia watu kesi, wataalam wachache tulionao wa upelelezi hawana mahala pa kufanyia kazi hapa Tanzania, baada ya idara then ije sheria wakati huo utashangaa sana kuona wataalam wapo.
 
Mkuu hizo bachelor huenda ndani yake kuna somo au course ya forensic lakini si kwamba wanatoa degree ya forensic. I stand to be corrected
Ofcoz hata mimi najua hakuna degree ya forensic bt ndan ya hizo kozi kuna course za forensic zinafundishwa thats why i have requested for maboresho! Nadhan ideal ya kuanzisha Law Enforcemen degree pale udsm wamelenga ktk kuandaa independent state prosecutors coz hatuna na kwa sasa kazi zao zafanya chini ya DPP ofic. Hii coz inasomwa na mapolisi, uhamiaji, na usalama wa taifa sana pale udsm. Idadi yao ni ndogo na kuna haja ya kuongeza namba ya udahiri!
 
Maneno kwamba ww ni mwanausalama yatakuandama sana ktk harakati zako za kisiasa hata kama hayana ukweli. Watz tunawaogopa sana watu hawa wakati kazi pekee wanayofanya ni kulinda viongozi wa magamba. Ni jukumu lako kueleza ukweli ili kupambana na propaganda hzo.

Kuhusiana na topic, ktk kupambana na uhalifu kisayansi, tupo nyuma kama miaka 60 ukilinganisha na mataifa yaliyoendelea. Yaani ukiangalia Medical detectives-on etv ndo unaelewa tupo nyuma kiasi gani. Wakati hapa hatuna hata kozi za diploma, kwa USA forensic experts ni PhD holders with years of experience. Nilisikitika sana kwa jinsi 'serial killer' wa bongo (miezi kadhaa iliyopita) alivyokuwa anatafutwa 'manually'. Mpaka leo kimya, naona wanasubiri aue tena.

Thanks alot for your candid Advise,hata hivyo wanahitaji Elimu ya Uraia Zaidi

Profesa wangu wa Counter-Propaganda and Psychological warfare Prof(Dr) Ben D.Mor wa Galillee university hakunifundisha hivyo,na badala yake inabidi nitumie alichonifundisha Brig.Gen.(Res) Ambassador Ruth Yaron kuhusu Media,Public opinion and National security.

kuhusu huyo serial Killer (nadhani unamaanisha yule wa wanawake) kwa kweli hiyo ni aibu kwa taifa.tunatumia mbinu za kijima kumtafuta serial killer.Akija serial killer aliyekuwa America those days anatumika kama symbol ya serial killers kwenye mafunzo ya investigation Edward 'Ed' Gein si angekuwa amewamaliza wanawake Tanzania hii by now?

hatufuati kanuni za Usalama,hatutumii technology za usalama.Sasa sijui CPI ya Israel ilifanya kazi gani kwa Tanzania maanake Tanzania ni mojawapo wa mataifa yaliyonufaika huduma nyeti za usalama kutoka CPI ya Israel pamoja na Kenya,Equitorial guinea na Nigeria kwa upande wa Africa.

Ndiyo maana naona tuna tataizo mno kwenye usalama wa taifa letu kuliko kitu kingine,Watu wakichoka na demokrasia sijui............! Hii loophole tuliyo nayo,we ngoja tu......!

Ningeshauri tu kama kuna police,mwanajeshi,mwanadiplomasia a mpelelezi anayetaka kujiendeleza kimasomo afanye mpango haraka kama ana uwezo apate Admission Haifa University Israel,Galilee Institute au apate Training kutoka CPI-Israel
97918338.jpg
61159915.jpg

14591617.jpg
 
Back
Top Bottom