Hatutaki maridhiano yoyote na huu utawala batili tarehe 09 tunatoka

Hatutaki maridhiano yoyote na huu utawala batili tarehe 09 tunatoka

kimsboy

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2016
Posts
11,190
Reaction score
24,620
Baada ya kutoa amri ya kuuwa Watanganyika zaidi ya elfu 10+ huku watu zaidi ya 23000 wakiwa hawajulikani walipo leo anataka maridhiano!

Maridhiano ya wauawaji?? Big No!! Eti kaua yeye halafu anataka kufanya uchunguzi yaani ajichunguze yeye!!

1. Amekwepa kuomba radhi kwa ukatili uliofanywa na vyombo vyake.

2. Amekwepa kueleza au kuelekeza miili iliyokosekana kukabidhiwa kwa ndugu zao wakazike.

3. Amekwepa kuzungumzia Utekaji ulitufikisha hapa.

4. Hajui kilichotufikisha hapa anasema Gen Z walifata mkumbo.

Wamekamata vijana wenzetu wamewapa kesi ya uhaini wamewatesa watu wamepigwa na shoti za umeme wengine wamechomwa kwa pasi, wengine wamelawitiwa wengine wamevuliwa utu wao, wapo walohasiwa halafu mtu anataka maridhiano!!

Bora mtuuwe wotee lakini hatuwezi fanya maridhiano na serikali ya wauwaji serikali ya kishetani.Subiri tarehe 09 tutawaonyesha Show hii itakua mega protest kila mtu na bango lake kwa amani kabisa

Kuna madogo pale Ubungo walikua hawana makazi wapo kama 35 hivi walikua wakilala chini ya Daraja la Ubungo na kule kwenye soko la mawasiliano wengine wanalala kule kando ya mto Gide hata zoezi la Sensa walifanyiwa mwaka 2022.

Vikosi ya serikali usiku wa tarehe 29 viliwamiminia risasi na kuwawaua kati yao 28 pale pale bila huruma!! Leo wanataka maridhiano!!

Watu wameuliwa kama wanyama vifo kila kona, hatumkumskia akilaani wala kuviamuru vya dola kuacha mara moja, aliishia tu kusema fujo zimeletwa na watu wa nje, leo anasema nini?

Hatuwezi kuridhiana na utawala haramu ulopatikana kwa njia haramu haturudi nyuma hata mtuuwe nchi nzima! Tutapambana mpaka tone la mwisho la Damu!! Tutapambana mpaka tukomboe nchi yetu haijalishi tutapoteza nini

Nimeamua kupoteza kila kitu nilichonacho kwa ajili ya nchi yangu nimepoteza marafiki waliouwawa kikatili, ndugu na jamaa nimepoteza hata washirika wa biashara kwasababu ya misimamo yangu!!

Hakuna maridhiano yoyote yale tutakula sahani moja mpaka kieleweke,Aidhaa aachie ngazi au aamuwe kuua vijana wa kiume wote nchi nzima kama alivyofanya farao kuua kila wazaliwa wa kiume wa familia za wayahudi ili kuzuia unabii kutimia lakini alishindwa.

Ndugu zangu Watanganyika wenzangu, tusirudi nyuma, tusisahau yalopita wala tusigange yajayo tusonge mbele, safari inakaribia, hakuna kurudi nyuma, hakuna kukata tamaa, kama tumeweza kuvunja pepo la uoga lililoitesa nchi hii kwa miaka 60 watu wakiogopa kutoka kuandamana na sasa hatuna uoga tena tutashindwa nini tena!!

Watu zaidi ya elfu 10 wameuliwa kinyama, watu 23000 hawajulikani walipo mpaka sasa sitaki kuelezea mateso ya ufisadi tozo na kadhalika na kuuza rasilimali zetu aiseee tuna sababu milioni za kudai nchi yetu hakuna kukata tamaa hakuna kurudi nyuma, narudia tena Sijutii kuandamana tarehe 29 na December 9 nitatoka na bango langu kuandamana.



1763103344632.jpg
 
Baada ya kutoa amri ya kuuwa Watanganyika zaidi ya elfu 10+ huku watu zaidi ya 23000 wakiwa hawajulikani walipo leo anataka maridhiano!
Hivi nyie vilaza hizi takwimu nani anawapa??
 
Sidhani kama december 9 Generation Z watakua na hizo nguvu na cofidence ya kuandamana bora tu-discuss mambo mengine wakuku..!!
 
Back
Top Bottom