Hatuwajibiki kwa pamoja ila tunalaumiana na kutegeana

Hatuwajibiki kwa pamoja ila tunalaumiana na kutegeana

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
376,316
Reaction score
871,876
TLS tuliitisha Mdahalo wa Kitaifa kuzungumzia Utekaji Baadhi ya sababu kuu zinazochangia utekaji kulingana na mjadala ule ni pamoja na

Udhaifu wa mifumo ya utendaji wa Jeshi la Polisi ( Colonial Mentality ) na kutotenganishwa kwa shughuli za Upelelezi na Uchunguzi kutoka Jeshi la Polisi na Kuwa Idara inayojitegemea na kujiendesha

Kukosekana kwa ufanisi katika vyombo vya usalama, ikiwa ni pamoja na upelelezi duni, rushwa, na ukosefu wa rasilimali, kumechangia wahalifu kuendesha vitendo vya utekaji bila kuogopa hatua madhubuti.

Uingiliaji wa siasa katika vyombo vya dola
Kuwepo kwa matukio ambapo vyombo vya dola vimetuhumiwa kushiriki au kufumbia macho vitendo vya utekaji, hasa kwa watu wanaoonekana kuwa tishio kwa mamlaka malalamiko haya tumeyasikia toka kwa Edgar Mwakabela,Mwamlima,Mdude Nyagali nk.

Kutokuwepo kwa uwajibikaji na haki kwa waathiriwa .
Hii inachangiwa na kukosekana kwa uwepo wa Taasisi ya kulisimamia Jeshi la Polisi haswa linapo lalamikiwa.Njia ya msingi ni kuiboresha Tume ya Haki za Bimadamu na Utawala bora kwa kuzipa Uhuru,Fedha ya kutosha,Kuajiri wataalamu na wapelelezi wake pamoja na kuwa na timu ya wanasheria wake wanao wajibika moja kwa moja kwa Tume hii.

Wengi wa waliotekwa au kutoweka hawajapata haki, na serikali mara nyingi haifanyi uchunguzi wa kina wa matukio haya na Polisi imekuwa ikitoa Majibu ya jumla jumla .Mazingira kama haya yanawapa wahusika ujasiri wa kuendelea na vitendo hivyo bila woga wa kuchukuliwa hatua.

Malengo ya kisiasa na udhibiti wa uhuru wa kujieleza

Baadhi ya matukio ya utekaji yameripotiwa kuwalenga wanaharakati, waandishi wa habari, na wanasiasa wa upinzani, jambo linaloashiria kuwa kuna nia ya kuzima sauti za upinzani na ukosoaji. Hii ni Mazingira kama ya upoteaji wa Kaina Soka na Wenzake,Madhila ya Kina Mdude Nyagali, Soka,Edagar Mwakamele,Mwalima ,Mzee Ali Kibao nk

Uhalifu wa kimfumo .
Uhalifu wa kupanga, kama vile magenge yenye nguvu, yanaweza kushiriki katika vitendo vya utekaji kwa lengo la kutisha, kupata fidia, au kusaidia ajenda fulani za watu wenye mamlaka.Lakini ni Mara chache magenge kqma haya kuteka wakosoaji .Haya yabakuwa na malengo binafsi yenye kulinda au kuendeleza magenge ya Kihalifu.

Kukosekana kwa sheria kali na Kukosekana utashi wa kuzitekeleza.

Ingawa kuna sheria zinazopinga vitendo vya utekaji, utekelezaji wake umekuwa dhaifu na hili pia linachangiwa na baadhi ya maamuzi ya Mahakama ambayo kwa mazingira yanatoa hifadhi kwa wenye dhamana ya kulinda uhai wetu kujificha na kukwepa wajibu wao, na hivyo kuruhusu vitendo hivi kuendelea pia nchi kutokuwa na mfumo thabiti na kuridhiwa kwa Mkataba wa Kimataifa kuhusu utekaji au upotezwaji wa watu.

Credit: Mwabukusi rais wa TLS
1742957951740.jpg
 
Namna ya kumaliza utekekaji ni rahisi sn wala haihitaji akili kubwa, ni kupiga marufuku polisi kukukamata bila kuwa na uniform, kitambulisho, lazima watoe taarifa kwa VEO/Mwenyekiti wa mtaa na mwisho ukikamatwa iwe lazima kuwajulisha ndugu zako, kinachofanywa kwasasa polisi ndiyo wahusika wakubwa. Simple
 
Tukio kama la Lisu wanakwambia hatoi ushirikiano ambapo ni hoja ya kipumbavu sn, je angekufa wangemfuata kaburini atoe ushirikiano? CCTV ziko wapi? kwanini eneo lile walitoa walinzi? hawa ndiyo watekaji wakubwa
 
Back
Top Bottom