Hatuwezi kuendelea kuendesha nchi kwa matamko ya jukwaani

Hatuwezi kuendelea kuendesha nchi kwa matamko ya jukwaani

fazili

JF-Expert Member
Joined
Jun 10, 2011
Posts
16,427
Reaction score
22,418
Mgogoro wa wafanyabiashara Kariakoo unatokana kwa kiasi flani na mazoea ya viongozi wetu kuendesha nchi kwa matamko ya jukwaani. Tangu lini tamko la kiongozi jukwaani likawa sheria?

Jambo kubwa kama ukusanyaji wa kodi na msamaha wa kodi kwa miaka 3-5 linatamkwa tu jukwaani bila maandishi yoyote?

Wanasiasa acheni hovyo hii mnasababisha hasara na vurugu nchini. Mnaacha kuweka utaratibu mzuri wa kukusanya kodi halafu mnakimbilia kukopa matrilioni nje huku mnaacha pesa inazagaa nchini! Viongozi wa Tanzania acheni uzembe na uvivu.
 
Tatizo la Tanzania ni siasa.

Siasa zinafanya watendaji washindwe fanya kazi yao.

Kama hapo tutegemee TRA kushindwa kusanya sehemu kubwa ya mapato
 
Tangu lini tamko la kiongozi jukwaani likawa sheria?

Jambo kubwa kama ukusanyaji wa kodi na msamaha wa kodi kwa miaka 3-5 linatamkwa tu jukwaani bila maandishi yoyote?
Kuna watu hawatakuelewa kwenye hii statement. Wanafikiri mtu akiongea jukwaani ndio kashaagiza.

Serikali inafanya kazi kwa nyaraka. Wakitaka hayo matamko yatekelezwe ni lazima wasaidizi wa rais wakitoka hapo waandike waraka wa ku- officialize hayo matamko, ili wasimamizi wa sheria watumie huo waraka kufanya kazi.
 
Hilo nalo wahusika huko serikalini wakaliangalie. Walifanyie kazi!
 
Kuna watu hawatakuelewa kwenye hii statement. Wanafikiri mtu akiongea jukwaani ndio kashaagiza.

Serikali inafanya kazi kwa nyaraka. Wakitaka hayo matamko yatekelezwe ni lazima wasaidizi wa rais wakitoka hapo waandike waraka wa ku- officialize hayo matamko, ili wasimamizi wa sheria watumie huo waraka kufanya kazi.
Waraka haubadili Sheria, ni suluhisho la muda mfupi
 
Back
Top Bottom