Hatuwezi kuendelea kuilaumu Kenya na Mabeberu kwa matatizo binafsi ya Tanzania: 'We are paying the price of our own Wrongdoings!'

Hatuwezi kuendelea kuilaumu Kenya na Mabeberu kwa matatizo binafsi ya Tanzania: 'We are paying the price of our own Wrongdoings!'

Nimesoma "Heading" ya mada yako ni mbovu; sijasoma yaliyomo kwenye mada, lakini kwa kuangalia hizo 'charts' pekee, unastahili kujibiwa bila mihemuko.

Niseme haraka, kwamba GDP sio kipimo cha kila kitu. Tunaweza kuanzia hapo.

Lakini kwa sasa, kichwa cha habari yako ni kibovu.; kwa sababu hakuna anaye ilalamikia Kenya kwa lolote.
 
Ongezea na hili :

Hadi Magufuli anaingia, balance of trade ilikuwa inaelekea kuwa chanya. Kikwete aliacha imports za 14.6 tr (na zilikuwa na trend ya kupungua from 18.5 tr mwaka 2013) na exports za 12.4 tr (na zilikuwa zikiongezeka kutoka 8.9 tr mwaka 2013). Kwa hiyo balance ilitoka -9.6 tr mwaka 2013 hadi -2.2 tr mwaka 2015

Ila tukajiharibia wenyewe mazingira ya biashara na kufukuza wawekezaji wa kigeni na wengine wazawa. Wakaondoka na mitaji yao na ujuzi wao wakapeleka kwingine ikiwemo Kenya. Matokeo yake import hazikubadilika sana, zilishuka kidogo kuja kuwa 12.6 tr kutoka 14.6 tr alizoziacha kikwete na uuzaji wa bidhaa nje ulipungua sana kutoka 12.4 tr alizoacha hadi kufika 6.2 tr mwaka 2020 !!!! Balance ya biashara ilitoka -2.2 tr mwaka 2015 kuja -6.4 tr !!!

Kwa maana nyingine ni kuwa sera ya viwanda ilikuwa ni maneno matupu huku kiongozi wa juu hajui hata namna ya kuhuisha viwanda. Hivi tunawezaje kusema uchumi wetu ulikuwa ukikua wakati viashiria vyote vilikuwa vikionesha kwamba tunarudi nyuma??

Source: TheChanzo
Uagizaji na uuzaji bidhaa kutoka nje

Absolutely, ni kama vile Magufuli alikuwa mhanga wa ufahamu finyu wa namna sekta binafsi inafanya kazi na namna gani inasaidia kukuza uchumi. Ndo maana aliona ni sawa tu kuwamwagia nyongo wawekezaji maana yeye aliamini hata serikali inaweza ikafanya biashara. Yaani mawazo ya Magufuli na mtizamo wake juu ya uchumi na ukuaji wake, ni ideology ya miaka ya sabini na themanini kama walivoamini akina Nyerere na Sokoine.
 
Nimesoma "Heading" ya mada yako ni mbovu; sijasoma yaliyomo kwenye mada, lakini kwa kuangalia hizo 'charts' pekee, unastahili kujibiwa bila mihemuko.

Niseme haraka, kwamba GDP sio kipimo cha kila kitu. Tunaweza kuanzia hapo.

Lakini kwa sasa, kichwa cha habari yako ni kibovu.; kwa sababu hakuna anaye ilalamikia Kenya kwa lolote.
Unasema heading ni mbovu lakini husemi sababu kwanini ni mbovu.. Hii pekee inaonesha ni jinsi gani fikra zako zimekuwa finyu na subjective.

Unaangalia charts halafu hujasoma yaliyomo... pamoja na kujipa jina la 'Kalamu' ila unakuwa mvivu wa kusoma.... hapo hapo unasema GDP sio kipimo cha kila kitu! ..... Kuna makosa mengine ukiyafanya unamdhalilisha mpaka mzazi wako.

Unasema hakuna aliyelalamika kuhusu Kenya na Mabeberu... mimi nna mifano hai ya viongozi wa nchi hii na ntaweka hapa baadhi ya nyuzi hata hapa jamvini ambao wamekuwa wakilalamikia Kenya na Mabeberu...

Kama unataka mpambano wa hoja, njoo na facts tupambane..
 
Ni kama vile mfumo wa kijamaa ume corrupt akili za watanzania. Na hilo ndo tatizo maana mpaka leo hata katiba yetu bado inasema hii ni nchi ya Kijamaa. Ndo maana unakuwa na Rais haoni umuhimu wa private sekta,,, na hiyo inaenda mpaka kwenye mawazo na mtizamo wa wananchi.
We uoni wanyonge still awajui umuhimu wa matajiri.
 
Unasema heading ni mbovu lakini husemi sababu kwanini ni mbovu.. Hii pekee inaonesha ni jinsi gani fikra zako zimekuwa finyu na subjective.

Unaangalia charts halafu hujasoma yaliyomo... pamoja na kujipa jina la 'Kalamu' ila unakuwa mvivu wa kusoma.... hapo hapo unasema GDP sio kipimo cha kila kitu! ..... Kuna makosa mengine ukiyafanya unamdhalilisha mpaka mzazi wako.

Unasema hakuna aliyelalamika kuhusu Kenya na Mabeberu... mimi nna mifano hai ya viongozi wa nchi hii na ntaweka hapa baadhi ya nyuzi hata hapa jamvini ambao wamekuwa wakilalamikia Kenya na Mabeberu...

Kama unataka mpambano wa hoja, njoo na facts tupambane..
Tutaongea mkuu.
 
Yap

Na mimi huwa nafikiri kama wewe, Tanzania ni resource rich, ikiwa tutaweza kutumia tu hizi rasilimali, uchumi lazima utoke kwenye hizi levels.

Changamoto ndo kama hizo sasa kwamba... ease of doing business in Tanzania bado ipo weak, so mwisho wa siku inaua motive ya investment kwenye natural resources, mwisho was siku unajikuta tuna resources lakini nchi bado ni masikini.. ni vitu kama hivo yani

..how about ease of farming?

..au ease of raising cattle?

..pamoja na ease of doing business tuongeze vipengele hivyo viwili hapo juu.

..pia productivity ya wakulima, wafugaji, na wavuvi, inaongezeka kwa kiasi gani hapa Tz?
 
Hayupo..ndo maana atleast kuna imani kuwa tutakaa sawa..point yangu ilikuwa ni kwamba 5yrs ni mingi,damage yake ni kubwa..kama angeliwa kichwa mapema isingekuwa kama hivi sasa.
Damage ilikuwa kubwa mnoo.. ila hata sasa, kama Tanzania bado serikali haitaboresha sheria kandamizi.. gap kati ya Tanzania na Kenya litazidi kukua maana ni kwamba sisi tunatambaa wao wanakimbia
 
Unasema heading ni mbovu lakini husemi sababu kwanini ni mbovu.. Hii pekee inaonesha ni jinsi gani fikra zako zimekuwa finyu na subjective.

Unaangalia charts halafu hujasoma yaliyomo... pamoja na kujipa jina la 'Kalamu' ila unakuwa mvivu wa kusoma.... hapo hapo unasema GDP sio kipimo cha kila kitu! ..... Kuna makosa mengine ukiyafanya unamdhalilisha mpaka mzazi wako.

Unasema hakuna aliyelalamika kuhusu Kenya na Mabeberu... mimi nna mifano hai ya viongozi wa nchi hii na ntaweka hapa baadhi ya nyuzi hata hapa jamvini ambao wamekuwa wakilalamikia Kenya na Mabeberu...

Kama unataka mpambano wa hoja, njoo na facts tupambane..
Kulikuwepo na jamaa anaitwa Kalamu, halafu akapotea. Alikuwa yuko vizuri sana...Sasa ndipo akaja huyu Kalamu1, sidhani kama ndiye yule yule.
 
Back
Top Bottom