Hatuwezi kupata uhuru wa katiba na demokrasia bila kuwa radical. Upole umetushinda

Hatuwezi kupata uhuru wa katiba na demokrasia bila kuwa radical. Upole umetushinda

Mimi ninacho furahi ni kwamba watu wameanza kuamka, angalau kuna vitu wameanza kuviona haviendi sawa wanavipinga japo ni mitandaoni. Mdogo mdogo tu hata vita za dunia zilianza na maneno maneno mpaka kufikia hatua ya kuanza kuchapana. CCM ataondoka tu siku zinakuja hii nchi ni yetu sote sio mali ya kikundi.
Inatia matumaini
 
Mkuu Makulu, MAKULUGA , mimi sio CCM mkereketwa na mfurukutwa, mimi ni wale CCM by default, tulioingia CCM kwa mujibu, enzi za chama kimoja, na kujikuta tunaendelea CCM kwasababu ndicho chama pekee, chama kwa maana ya chama!. Tanzania tuna chama cha siasa kimoja tuu, the one and only!.
P
Mkuu ni lini ccm ilisajiliwa kama chama cha siasa kwenye mfumo wa vyama vingi?
 
Hapana, hii ni kitu kinachoitwa the plain bitter reality, yaani ukweli mchungu, Tanzania tuna chama kimoja tuu cha siasa, chama dume na chama dola.
P
....tena Dume kweli kweli ndio maana hakina matunda ya kueleweka!
 
Upole kuna wakati hauleti mabadiliko hata nyerere alishasema kuhusu uhuru wa Africa. Mnao sema Nyerere alileta amani mjue kwamba amani inakuja na haki. Bila haki hakuna amani

View: https://youtube.com/shorts/7M_wnltQWao?si=h3MmufJZ-Np0mcJx

Mtu mwenye radical views kwenye siasa ni yule mwenye maoni na vitendo ambavyo vina utofauti na maoni na vitendo vya kawaida kwenye jamii. Haitoshi tu kuwa radical kwenye kuchochea mabadiliko kikatiba na kidemokrasia kwasababu tafiti za kutosha zinazo ainisha mapungufu ya katiba iliyopo ni muhimu zaidi. Mapungufu haya yaliyotolewa tafsiri ndiyo yanaweza kuwaleta wahusika mezani
 
Mkuu Makulu, MAKULUGA , mimi sio CCM mkereketwa na mfurukutwa, mimi ni wale CCM by default, tulioingia CCM kwa mujibu, enzi za chama kimoja, na kujikuta tunaendelea CCM kwasababu ndicho chama pekee, chama kwa maana ya chama!. Tanzania tuna chama cha siasa kimoja tuu, the one and only!.
P

Huo ndiyo uzalendo wengi hapa hatuna vyama lakini tunapenda nchi yenye demokrasia na haki.
 
Back
Top Bottom