Hatuwezi kuunga mkono jambo la nyongeza ya mshahara

Hatuwezi kuunga mkono jambo la nyongeza ya mshahara

Mushkov

JF-Expert Member
Joined
Feb 16, 2024
Posts
357
Reaction score
686
1. Watumishi wote wa Umma wanatakiwa kupata Increment kila ifikapo tarehe 1, ya mwezi July kila mwaka. Kwa nini hawajapata hiyo Increment wakati Budget ilipangwa na kupitishwa Bungeni? Hizo fedha za Increment za mwezi huu amechukua nani na kwa misingi gani?

Tunataka majibu ya haraka na yenye ukweli vinginevyo tunaipeleka serikali mahakamani kwa kuvunja masharti ya mkataba.

2. Upandishaji madaraja mwaka huu ni tofauti kabisa na miaka mingine.

Kuna watu walianza kazi mwaka 2003, hawajapandishwa daraja lakini walioanza kazi mwaka 2009 wamepandishwa madaraja, kwa hiyo walioanza kazi mwaka 2003 na walioanza kazi mwaka 2009 wapo sawa na hawa wote wana sifa zinazolingana.

Kwa hiyo, kama hawatafanya marekebisho, tunaazimia kwenda mahakamani kutafuta haki. Serikali hii ina shida gani lakini.

Mimi na wenzangu tumedhamiria kutafuta ya watumishi hawa.

Kwa sasa tunaendelea kutafuta mawakili wasomi ili kuipeleka serikali mahakamani.
 
Hivi hata wale wababaishaji huko kwenye maofisi ya umma nao wanatakiwa wapandishwe Daraja/mshahara kila mwaka?
Unakuta wafanyakazi wamefika ofisini tangu 07;30 lakini kazi ina anza saa tatu....ukipiga namba za simu za maofisi ndio shida kabisa; takribani 85% hazipatikani, hazijalipiwa, hazipokelewi BADO wanaohusika wanasubiri wapandishwe Mshahara/Madaraja kila mwaka wakati tija yao hata haionekani
 
Tulisharuhusu siasa kulipa kuzidi professionalism,matokeo yake wasomi wako radhi kuvua utaalamu wao na kua chawa wa wanasiasa wanaoangamiza Taifa hili.
 
Uko sahihi lakini Mimi nina maini tofauti kidogo.
Kwanini hamkwenda Mahakamani ndani ya miaka 7 ya Magufuli ambaye katika uongozi wake ndio wakati tulioshuhudia kanuni na haki za watumishi zikivunjwa kwa kiwango kikubwa?
Kwahiyo tuliza kalio, you are not patriot. Ungekuwa jasiri ungeshitaki kipindi cha Jiwe yeye hakuwahi kupandisha mtu daraja, hakuongeza mshahara, hakuweka annual increment hata mara moja, aliwatukana majukwaani, aliwatesa kupitia ma DC, maana kipindi cha Jiwe ma DC wamewasweka sana ndani.
 
Hivi hata wale wanaojibu email baada ya mwezi tena baada ya kufuatilia nao wanatakiwa wapandishwe Daraja/mshahara kila mwaka?
Unakuta namba za simu za ofisi za umma 85% hazipatikani, hazijalipiwa, hazipokelewi BADO wanaohusika wanasubiri wapandishwe Mshahara/Madaraja kila mwaka
Tena wao kila mwezi wanaomba overtime allowance
 
Magufuli ndio aliasisi dhuluma kwa wafanyakazi na sasa linaonekana ni jambo la kawaida.
 
Penal colony wa serikali ni mazuzu na wapumbavu,uende kudai haki y'ako kwenye hizi mahakama za Tanzania ?hivi uko Sawa kichwani kweli ?

Hakuna watu wapumbavu kama watumishi wa umma wa nchi hii,Kazi kupiga stories na kuwahi msosi wa mchana kwenye migahawa uku utendajikazi zero.

Bure kabisa.
 
1. Watumishi wote wa Umma wanatakiwa kupata Increment kila ifikapo tarehe 1, ya mwezi July kila mwaka. Kwa nini hawajapata hiyo Increment wakati Budget ilipangwa na kupitishwa Bungeni? Hizo fedha za Increment za mwezi huu amechukua nani na kwa misingi gani?

Tunataka majibu ya haraka na yenye ukweli vinginevyo tunaipeleka serikali mahakamani kwa kuvunja masharti ya mkataba.

2. Upandishaji madaraja mwaka huu ni tofauti kabisa na miaka mingine.

Kuna watu walianza kazi mwaka 2003, hawajapandishwa daraja lakini walioanza kazi mwaka 2009 wamepandishwa madaraja, kwa hiyo walioanza kazi mwaka 2003 na walioanza kazi mwaka 2009 wapo sawa na hawa wote wana sifa zinazolingana.

Kwa hiyo, kama hawatafanya marekebisho, tunaazimia kwenda mahakamani kutafuta haki. Serikali hii ina shida gani lakini.

Mimi na wenzangu tumedhamiria kutafuta ya watumishi hawa.

Kwa sasa tunaendelea kutafuta mawakili wasomi ili kuipeleka serikali mahakamani.
Mahakama which.

Wapeni GenZ hiyo kazi.
 
Back
Top Bottom