Hawa Ac Milan wamefikaje nusu fainali ya UEFA?

Hawa Ac Milan wamefikaje nusu fainali ya UEFA?

Ni mchongo tu milan ni moja tu Inter ile AC ilishajichokea baada ya utawala wa kina Pirlo walimuacha Pirlo kwa kigezo cha uzee alaf mwamba akaenda kukiwasha Juventus na akawa mchezaji Bora serie A kwa misimu mi 3 mfululizo
 
Yaani dakika ya 11 kashapigwa mbili za chap.

Iko wapi heshima ya nusu fainali jamani?

Hawa jamaa wamepenya vipi mpaka wakafika nusu?

Nawachukulia kama marumo gallants ya ulaya
Kwani Marumo Gallants una wachukuliaje? Yaani kila timu inayofungwa na Yanga mnaihesabia ni mbovu. Embu angalia record ya Marumo Gallants ilivyo kakatana na nani hadi kufikia hapa kwenye nusu

Kuhusu mechi ya leo, hao wanajuana halafu pia Ac Milan kapata tu bahati ya kumuotea Tottenham kisha kwa Napoli ikawa kheri kwavile Osimhen hakuwepo game ya kwanza. Ila ni timu iliyofika tu kwa bahati ila sio ubora.

Inter wanacheza counter attack za kibabe sana pasi tatu wapo golini halafu kule mbele kuna wachezaji wenye kasi, kukaa na mpira, na kuwachukua wachezaji. Ac Milan wanezidiwa mbinu na uwezo wa wachezaji
 
Back
Top Bottom