Hawa Ac Milan wamefikaje nusu fainali ya UEFA?

Hawa Ac Milan wamefikaje nusu fainali ya UEFA?

Kwani Marumo Gallants una wachukuliaje? Yaani kila timu inayofungwa na Yanga mnaihesabia ni mbovu. Embu angalia record ya Marumo Gallants ilivyo kakatana na nani hadi kufikia hapa kwenye nusu

Kuhusu mechi ya leo, hao wanajuana halafu pia Ac Milan kapata tu bahati ya kumuotea Tottenham kisha kwa Napoli ikawa kheri kwavile Osimhen hakuwepo game ya kwanza. Ila ni timu iliyofika tu kwa bahati ila sio ubora.

Inter wanacheza counter attack za kibabe sana pasi tatu wapo golini halafu kule mbele kuna wachezaji wenye kasi, kukaa na mpira, na kuwachukua wachezaji. Ac Milan wanezidiwa mbinu na uwezo wa wachezaji
Marumo ni vibonde na huwezi kunibadilisha huo mtazamo
 
Yaani dakika ya 11 kashapigwa mbili za chap.

Iko wapi heshima ya nusu fainali jamani?

Hawa jamaa wamepenya vipi mpaka wakafika nusu?

Nawachukulia kama marumo gallants ya ulaya
Umesahau Bayern walipigwa Goli nne na Madrid kwenye nusu fainali?? Tena goli tatu za mwanzo zilifungwa ndani ya Dk 19 Je bayern ilikuwa timu dhaifu??

Umesahau Barcelona walifungwa Goli 4-0 na bayern kwenye Michuano hii tena nusu fainali na marudiano barcelona hiyo hiyo ikala 3-0??

Umesahau Arsenal walifungwa goli 4-0 ma Barcelina tena nusu fainali...

Unailaumu AC milan kwa lipi.??

Bila shaka wewe umeanza kushabikia mpira Juzi...hujui kitu kuhusu UEFA....
 
Back
Top Bottom