Hatuachani sana mkuu huwezi kuamini ndo namaliza kusoma kitabu cha Audie Murphy(the most decorated soldier in WWII) kinaitwa To Hell And Back. Yaani interest yangu ni mambo ya zamaani tangu nikiwa shule ya msingi huko napenda sana kufuatilia kuanzia vitabu, documentaries etc
Yaani sometimes mpaka wazee wenyewe wananigwaya
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] nakumbuka nikiwa chuo nilirudi nyumbani ndg yangu mmoja aliniazima PC wakati anarudisha Kuna kauli moja aliongea na kuanzia hapo aliniogopa sana.Kwa vitu alivyokuta mle ndani.
[emoji16][emoji16][emoji16][emoji16]
Schoolmates walikua wakiniita Wikipedia yaani wakitaka info za mtu utasikia "muulizeni marapai" hatari tupu. Ila imenisaidia sana kama connection, maongezi deep na watu wazito for hours alafu tunaenda sawa tu yaani.
Kuna Prof mmoja mstaafu akisikia nimerudi likizo lazima aniite tuongee mawili matatu. Ila haya maisha bwn
[emoji23][emoji23][emoji23]
Haaahahaha hatari sana Mkuu kumbe na Wewe ulikua Wikipedia ya shule Kama Mimi nakumbuka Kuna wadau walikua wananiamini Mimi nikiwapa madini ya Slave trade, Industrial revolution,1stWW,2nd WW nk
Kiasi kwamba hata waalimu wa history hawawaamini mpaka wapate uhakika kwangu
Daaa yaani kiufupi wakati wenzangu wapo Leo Mimi nilikua kesho Yao kitambo
Sijui ule ujuaji ulikua unatokea wapi nakumbuka nikiwa form two Kuna madam alituweka kimagroup na kutupa Kazi mwisho wa siku mnawasilisha mbele ya darasa Sasa ndugu unajua nature ya shule nyingi za kata hata hakuna material ya kupata nondo makundi mengine waliishia kutoa Boko tu
Nakumbuka kundi langu nikiwa kiongozi ikafika siku ya kuwasilisha imebaki nusu saa tu hata kujiandaa hakuna swali ni mambo Slave trade lenye muunganiko na industrial revolution Aiseee nikagawa hints chap Kwa wahuni na kupanda mbele nilijikuta nalichakata chakata mpaka mifano inaenda French revolution na kina Bonaparte Napoleon
Mwisho kwani hata wanafunzi walielewa basi kwanza madam mwenyewe Nahisi hata Yale madini ndio kwanza aliyasikia kwangu akabaki kaduwaa tu
Toka siku hiyo madam akawa ananiheshimu na mpaka kupoteza confidence anavyofundisha kisa Mimi Kuna mda akawa anatoa notes tu halafu ananiangushia jumba bovu niwafundishe wadau!
Mwaka huu mwanzoni nilikutana nae mji Fulani akashangaa harakati zangu za kitaa tu akashangaa
Sijui alijua nitakua mchunguzi wa mambo kale kule misri?
😁😁😁😁😁