Hawa, Eva, Eve ni nani?

Hawa, Eva, Eve ni nani?

Mycle255

New Member
Joined
Sep 15, 2021
Posts
2
Reaction score
2
"NANI ATASIMULIA HADITHI YA SHETANI BAADA YA KUSIKIA UPANDE WA MUNGU?"
MIMI NIPO TAYARI KUSIMULIA, NITAANZA NA HAWA (EVA,EVE), NYOKA (The Divine Serpent) NA KUMALIZIA DHAMBI YA ASILI (Original Sin)

SEHEMU YA KWANZA:

Kwa takriban miaka 1,400 hadi 2,500, mamilioni ya Wakristo, Wayahudi na Waislamu wameaminishwa kabisa kwamba Hawa alikuwa mwanamke wa kwanza (the mother of human race) kwa sababu tu waandishi wa Agano la Kale walisema hivyo. Iliaminika kwamba waandishi hao walikuwa wamefahamishwa na Mungu, na Mungu asingeweza kusema uwongo.

Lakini, bila shaka, wasomi wa Biblia wanajua wazi kwamba Agano la Kale lina uwongo usiohesabika, makosa mengi, migongano na chembe kibao za wizi; maana waandishi hawakuwa wabunifu. Walikuwa wanakili (yaani wananakili) na wakusanyaji wa maandishi ya kale, ambayo mara nyingi waliyaharibu au hawayakuelewa. Hawakuandika maandiko yao ya uumbaji kwa kufahamishwa na Mungu, badala yake waliibadilisha kutoka vyanzo vingi vya hadithi ya Miungu ya kale.

Kitabu cha Mwanzo, Biblia inafungua kwa hadithi mbili tofauti za uumbaji. Masimulizi hayo yanafanana kwa kuwa yote mawili yanaeleza uumbaji wa wanyama, mimea, na wanadamu, lakini yanatofautiana kwa njia kadhaa na hata yanapingana katika masuala muhimu.

Katika Mwanzo 1, Mungu anaumba mimea, kisha wanyama, na kisha anaumba mwanaume na mwanamke. Katika Mwanzo 2, Mungu anaumba mwanadamu, mimea, kisha wanyama, na baadaye anamgawanya mwanadamu kuwa mwanaume na mwanamke.

Kwa sababu ya tofauti hizi na nyinginezo, kuna uwezekano kwamba waandishi tofauti wenye maoni na ajenda tofauti za kitheolojia waliandika hadithi hizi. Tofauti katika masimulizi zinaonyesha kuwa kila mwandishi alikuwa njia yake ya kipekee ya kuelezea uumbaji.

Katika Mwanzo 1, Mungu anaonekana yu mbali, akiumba kupitia kutamka iwe hivi itokee hivi n.k. kulingana na mpango mkuu. Picha hii inatofautiana na Mwanzo 2, ambapo mwandishi anamwonyesha Mungu kama mtu anayefanana na mwanadamu ambaye anatembea bustanini na kama mfinyanzi anayefanya kazi na udongo, mjuzi, akiumba kwa kutumia mikono yake. Mungu katika toleo hili anaonekana kuwa na mwili (physical body) tofauti na yule wa Mwanzo 1. Huyu aliwezea hata kutembea na kutafuta Adam alipojificha. 😆
Hata hivyo licha ya tofauti hizi, hadithi hizi mbili ziliandikwa upya (kuhaririwa na kuunganishwa) katika Mwanzo ili kuwa moja.

Hadithi hii ya kuzaa kwa mwanaume (male birth-giving) ilibuniwa mahsusi na mtaalamu wa marekebisho ya mfumo dume ili kumpa mwanaume mamlaka sawa ya maisha yote juu ya mwanamke ambayo hapo awali mamlaka hayo yalikuwa yakishikiliwa na mama juu ya mtoto wake. Mwandishi alirekebisha dhana ya zamani, ya awali kwamba akina mama walitengeneza umbo la watoto wao kutoka kwa damu yao ya ndani ya uterasi na mifupa ya watoto wao kutoka kwa mbavu zao wenyewe. Jina la kale la Mungu wa uzazi wa huko Sumer lilikuwa Nin-Ti, linalomaanisha “Mwanamke wa Ubavu“ (Lady of the Rib) na “Mwanamke wa Uzima” (Lady of Life).

Katika lugha ya huko Sumer, mbavu (rib) huitwa Ti, ikitamka "tii", pia neno Ti lina maana ya "to make live". Kwa hiyo jina Nin-Ti lilimaanisha "The lady who makes live" vile vile "The lady of the rib"
SUMER ni eneo la kale kabisa la Ustaarabu lililopatikana Kusini mwa Mesopotamia.

Katika hadithi za mwanzo za uumbaji huko Mesopotamia (sasa hivi Middle East), mwanaume wa kwanza alitolewa kutoka kwa ubavu wa MWANAMKE wa kwanza, na si kinyume chake.

NARUDIA
Katika hadithi za mwanzo za uumbaji huko Mesopotamia (sasa hivi Middle East), mwanaume wa kwanza alitolewa kutoka kwa ubavu wa mwanamke wa kwanza, na si kinyume chake.

Kulingana na maandiko ya Kibabiloni, jina la mwanaume wa kwanza lilikuwa Adamu, linalomaanisha “udongo wenye damu,” (bloody clay) likimanisha pia hirizi ya kushika mimba iliyotumiwa sana na wanawake wa kale.

Waliamini kwamba wangeweza kupata mimba kwa kutengeneza sanamu ya udongo ya mtoto mchanga na kuipaka damu ya hedhi. Kwa karne nyingi, kifungo cha kweli cha uhusiano kimetazamwa kama "damu" kwa sababu katika nyakati za kale uhusiano pekee wa damu uliofikiriwa ulikuwa kati ya mama na mtoto. Watafsiri wa kisasa kwa kawaida hutoa maana ya “Adamu” kuwa “dunia nyekundu” ili kuficha umaana wake wa awali.

ITAENDELEA...

1*drR0L40tiS5xmn_fWuoLBw.jpeg
 
Back
Top Bottom