MzeeKipusa
JF-Expert Member
- Feb 10, 2023
- 2,705
- 4,967
- Thread starter
- #41
Yumo kwenye orodha mpya. #ChomboYaFundiNi nani?
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Yumo kwenye orodha mpya. #ChomboYaFundiNi nani?
Solution ya hapa,Tunatokaje hapa Ndugu? Je tuichague CHADEMA katika kiti cha Urais? Tuunde KATIBA mpya? Unadhani hizo zitakua solutions?
Naona kama haya uliyosema yatatuchelewesha na kutupotezea muda tu. Mimi naona bora tuingie barabarani au wewe unasemaje?Solution ya hapa,
Wananchi tuhamasishane sisi kwa sisi, wewe mhamasishe jirani yako na mimi nimhamasishe jirani yangu tuanze kufuatilia na kupata taarifa zote za muhimu zinazohusu taifa letu na mambo yoote ya msingi.
Nguvu iliyopo ya kushabikia simba na yanga, iwe nguvu hiyohiyo ya kufuatilia taarifa muhimu kuhusu migodi yetu ya dhahabu na migodi ya chuma, pamoja na katiba yetu iliyopo.
Jamii ikishajengewa uwezo wa kufuatilia vitu vya msingi kupitia hiyo kuhamasishana, itakupata uelewa mkubwa zaidi. Hii itatupa wepesi kuona nafasi tuliyonayo ya kuleta mabadiliko katika mfumo mzima wa maisha yetu.
Yafaa sana kujua katiba yetu iliyopo inasemaje.
kuijua katiba itatupa wepesi wa kujua kama ina madhaifu au mapungufu, na vilevile itatusaidia kujua haki zetu za msingi. Watu wengi hatujui haki zetu za msingi zilizopo kikatiba.
Tupeane elimu sisi kwa sisi juu ya haki zetu za msingi na tusaidiane kwa dhati, kuijua katiba yetu ipaswavyo.
Viongozi wanatuburuza kwa sababu wanajua hatujui pakusimama, hatujui haki zetu.
Baada ya kuielewa katiba, tutajua kama kuna uhitaji wa kuibadili au la. Ni Lazima kwanza tuijue katiba yote na vipengele vyake vyote kabla ya kuibadili.
Hii itatupa nafasi ya kujua pa kuanzia. kwa sababu tatizo kubwa lipo kwenye mfumo wa elimu na mindset ya watanzania.
Hili suala si la u-CCM wala U-CHADEMA, ni swala la kitaifa linalohusu maisha yetu moja kwa moja pamoja na vizazi vyetu pasipo kujali itikadi za kivyama.
Ujinga au kutokuwa na ufahamu kwa wananchi ndiyo mtaji mkubwa wa wanasiasa wasio na nia njema na nchi yetu.
Baada ya hayo yote tubadili yote yaendane na kile tunachokihitaji, tuachane na nadhalia.
Mfumo wa elimu ubadilishwe uendane na mahitaji yetu.
Katiba pia ibadilishwe iendane na yale tunayoyahitaji kama jamii
basi sawa.Ubinafsi umo kwenye kundi la UJINGA
Mzee kipusa! Umeandika nini sasa!Enzi zetu wakati nakuwa mambo hayakuwa kama ilivyo sasa.
Nakumbuka, nilikuwa nikishuhudia viongozi wengi sana wakistaafu huku wakiwa hawana miliki ya vitu vingi.
Nionavyo Mimi, naona tayari MEZA imeishapinduliwa.
Maadui wakubwa wa Tanzania ni:
1. UJINGA (Enzi zetu hii ilikua kwà WANANCHI/ RAIA)
2. MARADHI (yalikuwa kwà Watumishi na Wafanyakazi)
3. UMASIKINI (ulikuwa kwà Viongozi)
Nasema meza imepinduliwa kwasababu, hivi sasa. UJINGA umewatawala viongozi walio wengi. Na wengi wao wanajidanganya kuhamasisha ujenzi wa mashule kwà ajili ya Wananchi wakati kiukweli kwasasa Wananchi hawana shida kabisa ni hizo shule zao (Kwani wameishagundua haziwasaidii watoto wao zaidi ya kuwatia UMASIKINI/wanaona bora wakae na watoto wao wasiwapeleke shule kupoteza muda na mwisho kuambulia Kukosa Kazi/ajira)
VIONGOZI wengi wamejirundikia mali za wizi na kuwafanya Wananchi/ Raia kuwa na UMASIKINI uliokithiri.
USHAURI: Ndugu zangu, hatuwezi kamwe kuwaondoa hawa maadui kwà kuipindua meza tutakua tunajidanga sisi wenyewe tu.
Ni vyema tukajitafakari sana kwà dhati ya mioyo yetu na kwà kukubaliana na ukweli. Tusiyakwepe matatizo tuliyonayo kwà kuyapaka rangi ya lips.
Tujitahidi sana kuzitumia experiences zetu, lessons zetu, study zetu na wisdoms zetu vizuri.
Mimi Mzee Kipusa, kwà dhati ya moyo wangu nina amini ya kwamba taifa letu haliwezi kamwe kuendelea na kuwa lenye Mafanikio kama tukiruhusu Milango na Madirisha yetu kuwa yamefungwa muda wote. Ni lazima tukubaliane kuifungua either Milango au Madirisha (kimojawapo). Hapa ndipo tutaweza kupiga hatua za kweli na zenye uhakika.
Nipe mji , nitakueleza vyema nilichokiandika.Mzee kipusa! Umeandika nini sasa!
Yatupasa kujua kwanza mzizi wa tatizo,Naona kama haya uliyosema yatatuchelewesha na kutupotezea muda tu. Mimi naona bora tuingie barabarani au wewe unasemaje?
Tutajulia huko huko barabarani. Mbona wao wanatuletea mambo na wanayalazimisha yaende kwà haraka bila kupenda kwetu? Kwanini na sisi tusifanye hivyo...bila wao kupenda?Yatupasa kujua kwanza mzizi wa tatizo,
Tunaweza kuingia barabarani na tusitatue tatizo. Au kusiwe na support ya majority. Unadhani kwa nini wakati wa mgomo wa kariakoo kuna jamaa walikuwa wanataka kufungua maduka ilihali kuna mgomo?
Jeshi likiwa upande wa wananchi, au wananchi tukiondoa hofu ya kufa hilo litawezekana bila shida. Hofu ya kifo nayo ni tatizo.Tutajulia huko huko barabarani. Mbona wao wanatuletea mambo na wanayalazimisha yaende kwà haraka bila kupenda kwetu? Kwanini na sisi tusifanye hivyo...bila wao kupenda?
Tuingieni barabarani. Hawa jamaa wamezidi upumbavu. Wanadharau sana!!!Jeshi likiwa upande wa wananchi, au wananchi tukiondoa hofu ya kufa hilo litawezekana bila shida. Hofu ya kifo nayo ni tatizo.