Hawa hapa maadui wa Taifa la Tanzania

Tunatokaje hapa Ndugu? Je tuichague CHADEMA katika kiti cha Urais? Tuunde KATIBA mpya? Unadhani hizo zitakua solutions?
Solution ya hapa,
Wananchi tuhamasishane sisi kwa sisi, wewe mhamasishe jirani yako na mimi nimhamasishe jirani yangu tuanze kufuatilia na kupata taarifa zote za muhimu zinazohusu taifa letu na mambo yoote ya msingi.

Nguvu iliyopo ya kushabikia simba na yanga, iwe nguvu hiyohiyo ya kufuatilia taarifa muhimu kuhusu migodi yetu ya dhahabu na migodi ya chuma, pamoja na katiba yetu iliyopo.
Jamii ikishajengewa uwezo wa kufuatilia vitu vya msingi kupitia hiyo kuhamasishana, itakupata uelewa mkubwa zaidi. Hii itatupa wepesi kuona nafasi tuliyonayo ya kuleta mabadiliko katika mfumo mzima wa maisha yetu.

Yafaa sana kujua katiba yetu iliyopo inasemaje.
kuijua katiba itatupa wepesi wa kujua kama ina madhaifu au mapungufu, na vilevile itatusaidia kujua haki zetu za msingi. Watu wengi hatujui haki zetu za msingi zilizopo kikatiba.

Tupeane elimu sisi kwa sisi juu ya haki zetu za msingi na tusaidiane kwa dhati, kuijua katiba yetu ipaswavyo.

Viongozi wanatuburuza kwa sababu wanajua hatujui pakusimama, hatujui haki zetu.

Baada ya kuielewa katiba, tutajua kama kuna uhitaji wa kuibadili au la. Ni Lazima kwanza tuijue katiba yote na vipengele vyake vyote kabla ya kuibadili.
Hii itatupa nafasi ya kujua pa kuanzia. kwa sababu tatizo kubwa lipo kwenye mfumo wa elimu na mindset ya watanzania.
Hili suala si la u-CCM wala U-CHADEMA, ni swala la kitaifa linalohusu maisha yetu moja kwa moja pamoja na vizazi vyetu pasipo kujali itikadi za kivyama.

Ujinga au kutokuwa na ufahamu kwa wananchi ndiyo mtaji mkubwa wa wanasiasa wasio na nia njema na nchi yetu.

Baada ya hayo yote tubadili yote yaendane na kile tunachokihitaji, tuachane na nadhalia.
Mfumo wa elimu ubadilishwe uendane na mahitaji yetu.
Katiba pia ibadilishwe iendane na yale tunayoyahitaji kama jamii
 
Naona kama haya uliyosema yatatuchelewesha na kutupotezea muda tu. Mimi naona bora tuingie barabarani au wewe unasemaje?
 
Mzee kipusa! Umeandika nini sasa!
 
Naona kama haya uliyosema yatatuchelewesha na kutupotezea muda tu. Mimi naona bora tuingie barabarani au wewe unasemaje?
Yatupasa kujua kwanza mzizi wa tatizo,
Tunaweza kuingia barabarani na tusitatue tatizo. Au kusiwe na support ya majority. Unadhani kwa nini wakati wa mgomo wa kariakoo kuna jamaa walikuwa wanataka kufungua maduka ilihali kuna mgomo?
 
Tutajulia huko huko barabarani. Mbona wao wanatuletea mambo na wanayalazimisha yaende kwà haraka bila kupenda kwetu? Kwanini na sisi tusifanye hivyo...bila wao kupenda?
 
Tutajulia huko huko barabarani. Mbona wao wanatuletea mambo na wanayalazimisha yaende kwà haraka bila kupenda kwetu? Kwanini na sisi tusifanye hivyo...bila wao kupenda?
Jeshi likiwa upande wa wananchi, au wananchi tukiondoa hofu ya kufa hilo litawezekana bila shida. Hofu ya kifo nayo ni tatizo.
 
Jeshi likiwa upande wa wananchi, au wananchi tukiondoa hofu ya kufa hilo litawezekana bila shida. Hofu ya kifo nayo ni tatizo.
Tuingieni barabarani. Hawa jamaa wamezidi upumbavu. Wanadharau sana!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…