MakinikiA
JF-Expert Member
- Jun 7, 2017
- 5,104
- 6,827
Iran yamnyonga raia mwenye uraia wa Uingereza na Iran
Raia wa Uingereza na Iran Alireza Akbari, ambaye alihukumiwa hukumu ya kifo nchini Iran, amenyongwa.Familia ya Bw Akbari ilikuwa imeombwa kwenda katika gereza lake kumuona kwa “mara ya mwisho" siku ya Jumatano na mkewe alisema alikuwa amehamishwa hadi katika gereza la peke yake.
Bwana Akbari alikuwa naibu waziri wa ulinzi wa Iran alikamatwa mwaka 2019 na kukutwa na hatia ya kufanya ujasusi kwa ajili ya Uingereza, jambo ambalo alilikanusha kuhusika.
Waziri Mkuu wa Uingereza Rishi Sunak alisema kunyongwa huko ni "kitendo cha kinyama na kinaonesha udhaifu wa utawala mbaya".
Mamlaka ya Iran "hawakuwa na heshima za haki za binadamu za watu wa kwao wenyewe," Bw Sunak aliongeza salamu za rambirambi kwa marafiki na familia ya Alireza".
Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza James Cleverly alisema hukumu hiyo lazima ipingwe.
Chombo rasmi cha habari cha mahakama ya Iran Mizan kiliripoti siku ya Jumamosi kwamba Alireza Akbari alinyongwa, bila kutaja tarehe ya kunyongwa kwake.
Habari hizo zilikuja baada ya Iran kuchapisha video ya Bw Akbari mapema wiki hii ikionesha kile kilichoonekana kukiri makosa na baada ya wizara wa intelijensia wa nchi hiyo kumtaja raia mwenye uraia pacha wa Uingereza na Iran kuwa "mmoja wa wahusika muhimu wa idara ya ujasusi ya Uingereza nchini Iran" .
'Aliteswa kwa saa 3,500'
Katika ujumbe wa sauti wa Bw Akbari alisema kuwa alikuwa akiishi nje ya nchi miaka michache iliyopita alipoalikwa kuja Iran kwa ombi la mwanadiplomasia mkuu wa Iran ambaye alihusika katika mazungumzo ya nyuklia na mataifa yenye nguvu duniani.
Akiwa huko, alishutumiwa kupata taarifa za siri kutoka kwa katibu wa Baraza Kuu la Usalama la Taifa la Iran, Ali Shamkhani.
"kwa kubadilishana na chupa ya manukato na shati".