Hawa ma bilionea wa Kibongo mbona hawana Private Jets wala Yachts?

Hawa ma bilionea wa Kibongo mbona hawana Private Jets wala Yachts?

Mijitu serikalini INA wivu,chuki,husda,mizandiki...Gwajima kanunua helcopter anatajwa anauza ngada..Manji kanunua TIGO hivyo hivyo ..Mo,Rostam,Mengi,Kikwete's,Bakhresa's etc wote wanaweza kununua jets
 
Kuna wanaotaka kuonekana matajiri na kuna wanaotaka kuwa matajiri,
Jifunze kupitia hilo,

Halafu kwenye nchi yenye roho za kimaskini kama hii ni kujitafutia matatizo na kina bashite
 
Ushuru mkubwa...sasa hata kuingiza kipajero tu unadai ushuru wa bei ya Vitz...unategemea ntakuelewa hata kama nina hela?? mbona nikashinde angani nchi za watu kama shida ni helcopter. Yatch utaishia kuziona tu kwenye video za kina domo hadi unyooke ewe mtanganyika
 
Kuna wanaotaka kuonekana matajiri na kuna wanaotaka kuwa matajiri,
Jifunze kupitia hilo,

Halafu kwenye nchi yenye roho za kimaskini kama hii ni kujitafutia matatizo na kina bashite


Kweli mkuu, huku kwetu watu wanazembea kutafuta ila wanachukia mafanikio ya watu.
Mtu akiwa na maendeleo kidogo tu utasikia huyo ni mtu wa magano n.k
 
Hao maprince Waleed, Talal, Faisal nk pesa zao ni halali maana baba yao Sultan Abdulaziz Al Saud ndiye founder wa Saud Arabia iliyokuwa na vinchi vidogovidogo akaifanya Saud kuwa taifa lenye nguvu na utajiri wa mafuta huku akitoa huduma zote muhimu kwa raia zake pia maisha bora

Wewe ungelia na Kikwete na wanamitando kwa kujitajirisha haraka kwa kukwapua mali za nchi hii huku wakiacha watanzania wakiwa na njaa, hawana huduma Za afya, hawana ajira wala huduma za jamii usilie na akina Prince Waleed wao wameanza kutanua baada ya kuhakikisha wasaud wako poa na hawana shida za kijinga sie akina Kikwete, Ridhwan, Chenge, Ngeleja, Tibaijuka, Muhongo, Karamagi, Omar Nundu, Rostam, Maswi, nk wanakwapua na kutajirika na wengine kuweka pesa nje ya nchi wakati watanzania wana njaa kwahiyo hapo nani wa kulaumiwa usultan wa Saud au wanamtandao?
Umeongea point za maana
 
Pesa za kununulia private jet watu wanazo....Ishu ni kwamba mazingira ya kumiliki private jet tz yana vikwazi kama ilivyo kwa mabilionea wa tz kutomiliki magari kama bughati

1.Miundo mbinu ni mibovu..Tajiri anataka atoke dar aende kucheki mashamba yake huko sumbawanga au kilosa...aisee zile airstrip za vumbi wapi na wapi maana gulfstrem inafaa itue kwenye viwnja at least vya lami. Hapo hata kwa usafiri wa barabara tajiri akinunua bughati hii mishimo na mituta mbona bughati inachakaa fasta

2.Mafundi na spea ni changamoto-Umewahi kujiuliza kwanini unashauriwa ununue toyota ukiwa bongo?, jibu ni kwamba upatikanaji wa mafundi na spea za toyota ni mrahisi sana na gharama nafuu, Sasa we agiza gari hata haijazoeleka uone mziki wake utaingia cost za kuleta mafundi kutoka nje hadi uombe pooo...Ndivyo ilivyo kwa ndege, Gulfstream raha yake muwe wengi wenye nazo ili spea zisiwe shida na mafundi wawafate kuwatengenezea mlio nazo.

3.Serikali ni kikwazo - Makodi na madocumentation ni mengi na yanakera sana,,, Mabilionea wengi ni watu wanaojali muda na hawapo tayari kuzinguliwa safari zao eti kisa kuna document haijasainiwa na mkuu alietoka kidogo kupata kahawa mgahawani.

4. Kuishi kijamii kufikiri kidunia: Mabilionea wengi wanapenda kuweka status zao ziwe juu lakini ziwe kwenye mipaka ya jamii ..kwa mfano hapa kwetu ukimiliki range rover basi it is more than enough na hivyo ndivyo ilivyo hata marekani ambapo kuonekana bilionea kipimo cha wengi ni private jet....So jamii zina affect lakini hawa mabilionea hawafikitii kwa mipaka ya jamii yao bali huishi kwa mipaka ya jamii yao lakini hufukiria kidunia zaidi..na pia kwa wanaosoma vitabu hawa mabilionea wanazingatia sana triple bottom line..just imagine bilionea ana p.jet lakini watz ni masikini kupita kiasi..hii inaleta pia picha mbaya kwa kampuni ya bilionea


IGA MBINU ZA KUPATA PESA NA SIO MATUMIZI
 
Matajiri wengi wa kibongo wametajirika kutokana na UBAHILI wao. So there is no way watanunua private jets wala Yatch..
 
Back
Top Bottom