Hawa madogo wa Simba wametegwa tena, wanategeka

Hawa madogo wa Simba wametegwa tena, wanategeka

Dan Zwangendaba

JF-Expert Member
Joined
Apr 25, 2014
Posts
5,814
Reaction score
8,118
Tangu niijue na kuifuatilia Simba sijawahi kuona kikosi kibovu cha Simba kama kilichocheza juzi na Mlandege. Haijawahi kutokea hata Simba B ikawa hovyo kiasi hiki.

Kocha Mgunda pamoja na kukerwa na namna walivyocheza, leo wamekichezesha kikosi kilekile isipokuwa Kibu tu. Watoto ni watoto tu. Bila kujua kuwa huo ni mtego, naona madogo wanacheza kwa standard ileile. Hakuna jitihada, pasi mkaa, wanapoteza mipira hovyo, hawajui kufungua wala hatuoni vipaji vile tunavyotarajia kuona kwa vijana wadogo kama hawa. Wengi ni wa kufukuza tu hapa.

Ogopa Sana Hakimu akikwambia Jitetee.
 
Hayo Kwao ni Mazoezi Ya CAF CCL, usichukulie serious....!

Ya nini Kujiumiza..!
 
Ndo uwezo wao ulipoishia…!!! Acha makasiriko mkuu…!! Simba TUNA KIKOSI KIPANA…!!! Huoni soka hilo…!!!??
 
Huu ni mtego kweli watu wanarukaruka hovyo kutuliza mpira ni kipengele, bora ya Okrah wengine wote upuuzi mtupu..
 
Inabidi muelewe katika pro sports yoyote, wachezaji wa ziada hasa wale ambao huwa hawachezi kabisa katika mechi huwa wanatumika zaidi mazoezini katika kuwapa support wale wanaotumika. Hilo ndiyo jukumu lao la kwanza.

Mara moja moja sana hawa wachezaji wa akiba mmoja mmoja anaweza akatumika katika mechi pale inapobidi sana.

Shida ya Simba ni kuwa baadhi ya wachezaji hawa wanalipwa pesa nyingi zaidi ya majukumu yao katika timu, ingawa hapa labda tunaongelea wachezaji wawili au watatu na pia watu walikuwa na mategemeo makubwa na baadhi yao walipoletwa ingawa hawajawahi kukuzwa na wasemaji wa timu kuwa wana uwezo mkubwa.

Hivi Kyombo alivyoletwa Simba, kuna mtu ndani ya Simba alisema tutegemee makubwa kutoka kwake? Au Okwa?
 
Tangu niijue na kuifuatilia Simba sijawahi kuona kikosi kibovu cha Simba kama kilichocheza juzi na Mlandege. Haijawahi kutokea hata Simba B ikawa hovyo kiasi hiki.

Kocha Mgunda pamoja na kukerwa na namna walivyocheza, leo wamekichezesha kikosi kilekile isipokuwa Kibu tu. Watoto ni watoto tu. Bila kujua kuwa huo ni mtego, naona madogo wanacheza kwa standard ileile. Hakuna jitihada, pasi mkaa, wanapoteza mipira hovyo, hawajui kufungua wala hatuoni vipaji vile tunavyotarajia kuona kwa vijana wadogo kama hawa. Wengi ni wa kufukuza tu hapa.

Ogopa Sana Hakimu akikwambia Jitetee.
Yaani wameingia kwenye mtego vizurii..ukiachwa hapoa au kukaa benchi hakuna wa kumlaumu
 
Okwa, Kiyombo sio wa kuichezea Simba. Bora hata na Kibu D.
 
Wote hamna hata kibu d
Kocha mpya kamkubali KibU D.

Wachezaji wazawa wanasikitisha sana, hawajitumi.

Kyombo ni mrefu, ana nguvu, bado kijana.
Sasa mpe mpira atembee nao
Hapo ndipo utaishia kucheka tu.

Kijana kutoka Simba B aliyefunga goli pekee kombe la Mapinduzi ana kitu Mguuni.
Mchezaji anaonekana hata kwa mikimbio yake tu akiwa hana mpira.
 
Kyombo ana mwili mzuri wa mpira ila hana foundation nzuri ya mpira. Kuna vitu alivikosa katika hatua zake za mwanzo za kujifunza mpira ni vigumu kukua kutoka hapo alipo hata akae chini ya uangalizi wa Zidane labda mpaka ku reset akili yake aanze upya. Hilo ni tatizo la wachezaji wetu wengi wazawa.
 
Back
Top Bottom