Hawa na hili pekee ndiyo litakalo muokoa Rais wa TFF Malinzi vinginevyo imekula Kwake

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2013
Posts
60,660
Reaction score
121,325
Mosi.

Nawaomba wale ' Wajumbe ' wanne ( 4 ) wa TFF ambao kimsingi wameshajulikana kuwa na wao walikuwa wanafaidika nae hasa kwa ' mtonyo / pesa ' na ndiyo maana wameharibu kabisa ' mchakato ' wote wa Uchaguzi Mkuu kwa kuendelea ' kung'ang'ania ' Rais wa TFF Jamal Emil Malinzi ajadiliwe na ikibidi agombee kuwa muda wowote kuanzia sasa waitishe Press Conference na waseme rasmi kuwa wanakubaliana na Mwenyekiti Revocatus Kuuli na kwamba Jamal E. Malinzi safari yake iishie hapo.

Pili.

Namwomba Rais wa TFF Jamal Emil Malinzi kama anaweza tena kupitia yule Wakili wake Ndugu Aloyce Komba amwambie kuwa ameamua rasmi kuachana na TFF na kwamba hatogombea tena Urais kama ambavyo anaendelea ' kung'ang'ania ' huku akiharibi ' mchakato ' mzima kwa kuendelea kuwatumia hao ' Wajumbe ' wanne ( 4 ) kwa ' maslahi ' ambayo Wao na Malinzi wanayajua.

Kuna Watu siku ya Alhamisi baada ya akina Malinzi kupelekwa ' rumande ' niliposema kuwa Malinzi asicheze na ' System ' na kwamba akiendelea ' kubishana ' au ' kushindana ' nayo ' ataumia ' Yeye hawakuniamini wala kunielewa.

Nilienda mbele nikatahadharisha kuwa ' System ' ipo nyuma juu ya hili na inacheza ' Karata ' zake vizuri mno kiasi kwamba endapo wakiona Malinzi ' hasalimu ' amri kwa kuwa mpole na ' kujiondoa ' katika ' Kinyang'anyiro ' itakula Kwake na nikasema kuwa leo hatoweza kutoka kama ambavyo wengi wenu mlidhani na badala yake ili kuzidi ' Kumkomoa ' na kumuharibu zaidi ' Kisaikolojia ' leo tena Kesi yake inapigwa Kalenda ili kupima ' Upepo ' na kama Malinzi akizidi kujifanya ' Mjeuri / Kiburi ' basi kuna uwezekano akawa ' mkazi wa kudumu ' hapo Segerea.

Mwisho namalizia tu kwa kusema kuwa endapo ' Wakili ' wa Malinzi ataitisha Mkutano na Waandishi wa Habari na kutangaza kuwa ' Mteja ' wake Rais Jamal Emil Malinzi ameamua rasmi kuachana na Kugombea Urais TFF katika Uchaguzi Mkuu ujao wa August 12, 2017 basi ' nawahakikishieni ' kuwa siku ya Kesi yako kutajwa tena tarehe 17, July 2017 atapewa dhamana na tutakuwa nae mtaani.

Yangu ni hayo tu ila hapana chezea ' System ' kama ' ikikutafuta '.
 
Thanks unaposema system,unamainisha TISS?,real hii system iingilie hadi kwenye hili?,yeah kazi ipo,ila ninategemea system inayotumia tax money yangu ijikite kuona nchi yetu ni salama,nchi yangu haigeuzwi dampo ya bidhaa feki.mikataba ya ajabu,ugaidi,eneo letu la bahari haligeuzwi dampo,kunipatia viongozi wenye nia ya kweli ambao watakuwa wanajiuliza nini wataifanyia nchi yangu sio otherway round.mmm
 
Hawa watu ngoja wavune walichokipanda, wale wajumbe wanne wameonyesha ushamba mkubwa kweli kwenye hili sakata, kwa hali ilipokuwa imefikia ni kichaa tu ndio anaweza kufanya mchezo wa kumrudisha Malinzi ulingoni.

Kuna yule mwanmama sijui ni nani yake ameonyesha uzuzu wa kiwango kikubwa kwa kutaka kuwaongopea watu eti hata nchi nyingine wanafanya hivyo kumsaili mtu ambaye hayupo, waandishi waliokuwepo siku ile walitakiwa kumnasa makofi kwani hat mifano ya alichokuwa anakihubiri alikuwa hana ila apewe muda akaitafute.

Unachosema ndio kitu walitakiwa kustuka toka day one, Malinzi hatakiwi pale tena sio na system tu hata wanamichezo wengi ukiachia mbali wanufaika wa uwepo wake, kwahiyo hakutakiwa kupimana nguvu na umma.

Ngoja arefushe muda wa kukaa rumande kwani kule hakujawahi kuchoka wala kujaa kuwabeba watu wa aina yake.
 

Nani kakuambia kuwa ' System ' ni lazima iwe tu TISS? Halafu naomba nikuulize hivi katika ' thread content ' yangu hapo juu nimewataja hao TISS wako? Ni vyema ukauliza jambo ueleweshwe au uelimishwe kuliko kuwa ' mzushi ' tu. Neno ' System ' lina dhana pana mno na unaweza ukakuta hata hao so called TISS wako uliowataja au kuwahisi ' hawahusiki ' kwa lolote lile. Hivi Mkuu kwani PCCB waliomkamata wao hawafai kuitwa System? Kwani ' Mafia ' wa masuala ya Michezo hapa nchini Tanzania ambao hupenda kuweka Viongozi wao ama wenye mahaba na Simba au Yanga na wao hawawezi kuitwa System? Je baraza la Michezo Tanzania BMT kama labda na lenyewe limeona matatizo makubwa TFF na linaona Kiongozi wake ' anaharibu ' hivi na wao wakiamua ' kummaliza ' Malinzi haitoshi na wao kuitwa System?

Ningependa pia kusikia kama siyo pia kujifunza kutoka Kwako nini maana ya neno System ili pengine nami nielimike zaidi.
 
Nimekuelewa kabla Hujaandika.

Nashukuru Mkuu kwa kunielewa kwani wengine zawadi pekee tuliyopewa na Mwenyezi Mungu ni kuwa na ' maono ' makali na kuwatahadharisha Watu mapema juu ya ' hatari ' inayowaijia na waweze kuepuka ili kama ikitokea ' wakizembea ' basi wasije kulaumu kuwa hatukuwaambia.
 

Nashukuru sana kwa kunielewa Mkuu sasa ngoja waendelee ' Kupuuza ' hayo mambo mawili niliyowatahadharisha hapo juu waje wasage meno huko mbele ya safari. Hatima nzima ya Malinzi ipo kwa hawa Wajumbe wanne ( 4 ) kukubali asiwepo tena katika Kinyang'anyiro na pia kwa Malinzi mwenyewe Yeye kama Yeye kutangaza kuachia ngazi na aendelee na maisha yake mengine.
 
Malinzi anataka kumwaga mboga ,kwamba anataka akiondoka TFF huku Tz iwe imefungiwa na Fifa , hivyo anafanya vurugu za makusudi
 
Fair enough ,kutumia neno system katika uzi wako umeashiria hawa ni watu wenye mamlaka ya kuweza kubadili mchanganyio mzima wa kiutaratibu uliopo,na mifano umetoa kuhusu nguvu ya system hii kuwa once Mr.MALINZI akijitoa na kesi yake inaweza kufutwa,PCCB,sio system na hao mafia wengine uliowataja hawana nguvu za kusimamisha uchaguzi uliopo kisheria.na ninaamini kuwa PCCB wao wamewapeleka hawa mahakamani na ni Hakimu mwenye uwezo wa kutoa maamuzi.
 
Jamaa alighushi hadi risiti ya kuikopesha TFF milioni 1 na laki 2... Hahaha hachomoki

Tena ' Wamemtegea ' patamu sana na ndiyo maana ' Wahusika ' wapo kimya wanawaangalia tu hao Wajumbe Wanne na Malinzi mwenyewe. Huu mchezo umechezwa ' Kitaalam ' na ' Kimafia ' mno kiasi kwamba hata Yeye ( Malinzi ) na wale Wajumbe wake hawaamini macho na masikio yao.

Kuna Watu wanasema kuwa sijui ile FIFA ' delegation ' inayokuja inaweza kubadili kilichopo na pengine Malinzi akapata ' Unafuu ' ila niwaambie tu kuwa wakati ' mchezo ' huu wa ' Kimafia ' ukisukwa na ukasukika hivi kama ilivyo sasa hawa Jamaa ( Mafia wa Soka la Bongo ) walishajua kabisa kuwa FIFA watashtuka na kuja ' Bongo ' ila tayari hata Wao wameshaandaliwa majibu yao ya kupewa na kama haitoshi ' nimedokezwa ' kuwa kumbe kuna ' Kashfa ' nyingine ya about Tsh 12 billion zimekutwa ' zimeyeyuka ' ambapo ilikuwa ' inasubiriwa ' tu leo apewe dhamana na wakati akiwa anatoka tu pale Mahakamani basi angekamatwa tena na kuendelea ' Kusota ' pande za ' Segadansi ' kwa siku kama siyo miezi kadhaa zijazo / ijayo.

Enyi Wajumbe Wanne mlio ' Watiifu ' kwa Jamal Emil Malinzi tafadhalini kubalianeni na Mwenyekiti Wakili Msomi Kuuli kuwa Malinzi asiwepo na ' mchakato ' uendelee ili mumsaidie hiyo tarehe 17 July, 2017 ' mwenzenu ' apate dhamana la sivyo atapotelea kabisa huko ' Segadansi '.
 
wale wajumbe wa4 wa kamati ya uchaguzi wasipokuwa makini watampoteza bosi wao kwa tamaa zao wenyewe!

Nimeshawatahadharisha mapema sana katika ' uzi ' huu hivyo kama hawatanielewa au ' kunisoma ' shauri zao na ' Bosi ' wao.
 
Malinzi anataka kumwaga mboga ,kwamba anataka akiondoka TFF huku Tz iwe imefungiwa na Fifa , hivyo anafanya vurugu za makusudi

Hawezi na anapoteza tu muda wake Mkuu kwani ' Wanamume ' walishajipanga ' Kitambo ' sana na hayo anayoyapanga au kuyafikiria kuyafanya Malinzi kwa TFF na Tanzania. Amechelewa sana na alishindwa kushtukia mapema mno ' mchezo ' na ' mtego ' wa ' Kimafia ' aliochezewa tena na Watu wake wa karibu sana ambao aliwaamini.
 
Hii ina maana kuwa akitunisha msuli atakosa vyote...urais TFF na maisha huru ya uraiani.......
 

Naona unanipotezea muda wangu kwani ' nakuelewesha ' lakini bado tu Kichwa ' Tofali '. Kazi unayo!
 
Thubutuu.. Yeye asipokuwa na utetezi unaoeleweka ndo basi tena. Kwanza ilitakiwa kwa tuhuma hizi aachie mwenyewe!

Waambie hao Mkuu na wakifanya ' mzaha ' Ndugu yao ' ataozea ' kimoja ' Segadansi '. Shauri zao!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…