Hawa Napoli msimu huu wana balaa zito

Hawa Napoli msimu huu wana balaa zito

changaule

JF-Expert Member
Joined
Jan 10, 2020
Posts
6,039
Reaction score
10,151
Kwa wale wanaofatilia Ligi ya Mabingwa Ulaya, na Ligi Kuu Italy yaani Serie A bila shaka wameshaiona ni jinsi gani Napoli wanavyoshambulia kama nyuki. Nikisema huvyo bila shaka mashabiki wa Liverpool wanaelewa kiliwakuta nini msimu huu kwa hawa jamaa.

Kama hiyo haitoshi vijana wa Ajax wakiwa nyumbani kwao wametandikwa magoli 6. Hii timu inaweza ikawa moja ya timu inayoweza kufika mbali msimu huu Champions League, hasa ukizingatia kuwa wale waliyotambulika kuwa wababe wa Ulaya wamebakia wawili tu ambao ni Bayern Munich na Real Madrid.
 
Huwa nawaza ni jinsi gani team kama chelsea inatoa 50m pound kumsajili sterling wakati napoli inatoa euro milioni kumi kupata saini ya kvicha kvaratskhelia . Huyu dogo kwa waliomfuatilia toka yupo Rubin Kazan kule urusi alikuwa ni moto kisha akarudi dinamo batumi , Napoli wakamchukua kwa hela ya kununulia maandazi kabisa. Sasa sasahivi kumng'oa pale napoli bila ya 100m pounds bado hujampata.
 
Naaaaaam
 
Liverpool msimu huu ni kama underdog Hana makali yoyote yale pengine abadilike mbele huko na huyo ajax huwa ni msindikizaji japo huwa anafika mbali.
Mashindano ya klabu bingwa ni tofauti na ligi kuu kwa hilo ulielewe. Timu inaweza ku struggle kwenye ligi yao lakini kwenye champions league ikawa timu bora kabisa na wakakiwasha vyema. Liverpool kwenye champions league kapoteza dhidi ya Napoli pekee unasemaje kuwa hana makali?

Timu kama inafika mbali hauwezi kusema ni underdog. Kama Ajax na Liverpool ni underdog basi tuhitimishe kuwa UEFA champions league ya msimu huu imejaa ma underdog zaidi ya asilimia 90. Kama hao ndio wanaingia kwenye kundi la underdog je wakina Celtic, Copenhagen, Shakhtar donetsk, Maccabi Haifa, n.k watakuwa ni akina nani?
 
Huwa nawaza ni jinsi gani team kama chelsea inatoa 50m pound kumsajili sterling wakati napoli inatoa euro milioni kumi kupata saini ya kvicha kvaratskhelia . Huyu dogo kwa waliomfuatilia toka yupo Rubin Kazan kule urusi alikuwa ni moto kisha akarudi dinamo batumi , Napoli wakamchukua kwa hela ya kununulia maandazi kabisa. Sasa sasahivi kumng'oa pale napoli bila ya 100m pounds bado hujampata.
Unaambiwa ndio mrithi wa lorenzo insigne[emoji91]

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Hapo bado Victor Osimhen hajapona dadeki!! Raspadori na Giovani simeone wanakiwasha...huyo zambonguisa na zielinski hatari...pembeni unakutana na georgian messi, Kvaradona
Hivi uyu Giovan simeone ndio mtoto wa diego simeone?
 
Huwa nawaza ni jinsi gani team kama chelsea inatoa 50m pound kumsajili sterling wakati napoli inatoa euro milioni kumi kupata saini ya kvicha kvaratskhelia . Huyu dogo kwa waliomfuatilia toka yupo Rubin Kazan kule urusi alikuwa ni moto kisha akarudi dinamo batumi , Napoli wakamchukua kwa hela ya kununulia maandazi kabisa. Sasa sasahivi kumng'oa pale napoli bila ya 100m pounds bado hujampata.
Hili pia nashangaaga sana hizi timu kubwa zinatoa pesa nyingi hivi ni kwa ajili ya kujitangaza ama nini
Japo pesa ni zao ila pia ziendane na thamn ya mchezaji mtu kama anthony eti 100m 😳
 
Back
Top Bottom