Hawa ndio MaDj wakali zaidi Tanzania

Hawa ndio MaDj wakali zaidi Tanzania

Dj Mafuvu
Dj Zero
Dj Mubbah

Hawa ndio ma dj wangu bora duniani ukimtoa Dj Khaleed
Huyo Khaled weko ni cha mtoto pia makelele na mayoe ya bangi ndo yanamfanya mumtolee macho kuwa ni mkali.. Wakat kuna Djz wanoma na wakali kama Dj Doug. E Fresh, Dj Master Flex, Dj Premier, Dj Scrutch, Dj Envy, Dj Drama and many more..
 
Huyo Khaled weko ni cha mtoto pia makelele na mayoe ya bangi ndo yanamfanya mumtolee macho kuwa ni mkali.. Wakat kuna Djz wanoma na wakali kama Dj Doug. E Fresh, Dj Master Flex, Dj Premier, Dj Scrutch, Dj Envy, Dj Drama and many more..
hao wengine ata siwafaham mkuu, ngoja niwafatilie aisee
 
Ukiacha kuweka play list nzur ya muzik,hv steve b ana sifa gan za zaid il na yy tumfanye km reference ya dj wakal bongo? nionavyo mm steve b anafunikwa mno na dj d ommy kwa sasa
Dj d ommy ndo dj bora kwa sasa bongo hii,kwenye kizazi hiki..jamaa anajua kumix kweli kweli
 
Kwa bongo Dj mafuvu, ila mbele namkubali Dj Premier na pia ni Producer moja ya biti ninayoipenda aliyoitengeneza ni ya wimbo wa Animals ya Dr dree ft Anderson paak, kutoka ktk album ya Dr dree straight outta Compton , bonge la biti.
 
Mmmmh! Sijaona
Petter Mo hapo! Huyu Jamaa Nouma sana
Tatizo lenu mnachanganya mahaarage na njugu mawe. Ni kweli isiyo pingika,zote ni mboga ila hazifanani na mapishi yake ni tofauti sana.
 
Huwa naenda klabu Mara moja moja huwa nasikia nyimbo za aina moja tu ( bongo flavor )mpaka inakera
 
Dj Exclusive
Dj Khaleed
Dj Neptune
Dj Dreka ndio ma dj bora kwangu.
 
1,Khalid Uledi - Dj KU Times fm, Huyu jamaa anapokuwa kwenye mashine hutaboreka kumsikiliza huwa ana Playlist Bomba kinoma.

2,John Dilinga Matlou (Dj JD-radio one), Huyu naweza Sema ndo legendary wa MaDj wote bongo,, Jamaa huwa ananikosha sana na flash back zake full mzuka aisee mcheki kila jmos.

3,DJ Dusco Dalla - Bomba fm Zanzibar - Jamaa huwa anakun'guta madude ya mbele hatari tupu Sema huwa ananiangusha pale anapogeuka kuwa mtangazaji badala ya Dj mwishowe huishia kuharibu tu sababu hana swaga za utangazaji, namkubali sana huyu mtu.

3,Dj Side - Hits fm Zanzibar, Jamaa yuko vizuri kwenye mixing ingawa sio mfuatiliaji sana wa bongo flavor ila sometimes Playlist yake huwa inategemea sana jinsi mpenz /mke/rafiki zake walivyom treat kabla hajaanza kipindi . Akiacha kujifanya much know sana itabaki kuwa ni moja kati ya Dj bora hapa Tz.

4,Dj Makey, mara ya mwisho kumsikiliza ilikuwa East Africa radio Sina uhakika kama bado yupo hapo, Ana mixing za hatar hasa hasa umkute anagonga bolingo hata kama shemeji yenu anahitaji gegedo huwa namwambia asubir kipindi kiishe.

5,DJ Majizo for Shizo - Alianzia Magic fm baadae akaibukia Efm, kwa wale mnasikiliza Efm mtakuwa mnasuhuzika vilivyo na mitwango yake

6,Dj Steve B-Clouds fm, huyu ni Legend mwingine kwenye kazi hii naweza Sema ndo Dj bora kuliko wote pale mawingu fm.

6,Mafuvu Baby - Alikuwaga kwa mzee Mengi na baadae akasepa sijui yuko wapi kwa sasa ila all in all I do appreciate his work.

7,Dj Venture - clouds fm, ukiondoa Steve B hapo mawingu basi huyu jamaa ni habar nyingine, Nakumbuka wakati clouds inaungua pale jengo la kitega uchumi Venture ndo alikuwa studio anapiga mangoma sasa kuna jingle moja alikuwaga anaipenda na ilizoeleka sana kwa wasikilizaji inasema ^MOTO UNAWAKA ^ siku ya tukio kama saa tatu usiku hivi ikasikika saut MOTO UNAWAKA, watu wakahisi jingle tu kumbe jamaa ndo anatoa taarifa hivyo, ghafla mitambo ya radio Ikazima kesho yake ndo tukajua kumbe Venture alimaanisha studio inaungua.
Namkumbuka sana DJ JD mtaa wa mangoma pale redio one kila jmamos asubuhi hv mpaka mchana, miaka ya 2000 mwanzoni
 
Back
Top Bottom