Hawa ndio wanasoka wanaopewa kick sana kuliko uwezo wao

Scholes bado alikua anauwezo wakawaida tu nae kwenye ulimwengu wasoka, Ila ni kweli kwa PL alikua yupo juu kiuwezo.
unamfahamu Rui Costa?, Aimar? mehmet Scholl?
Rui Costa sijui kwann media zilikuwa hazimpi kiki
 
Ha ha ha ha ha ha ha ha ha Karim Benzema, takataka kabisa hii.
 
Kwa kweli mkuu kama Neymar angekuwa mzuri kama anavyopambwa na kikosi cha PSG tungeshuhudia Madrid anakufa pale pale Bernabeu.

Nakubaliana na wewe mkuu, angeanza yule Di Maria tungeshuhudia matokeo tofauti. Neymar akibebwa na Messi sana ila ameshindwa kutambua kuwa mpira aliofanikiwa pale Barca ni Messi ndo amefanya awe vile. Kule PSG atawika huko huko france tu ndo maana kwa sasa anatangatanga aende Madrid.
 
mtoa mada nimegundua ni shabiki wa chelsea, usiniulize nimejuaje....

back to the topic, ngoja nikukosoe....
1. neymar ni level nyingine mkuu, acha chuki na majungu... jamaa anaujua mpira, anauamrisha na unamtii kadri awezavyo. unaijua record yake tangia akiwa huko kwao sau paulo ? barca ? now PSG ?
number hazidanganyi amefunga magoli mengi, na ametoa assist za kutosha.....

je unaijua record yake ya ufungaji timu ya taifa ? kaitafute alafu uje hapa... acha chuki kumfananisha neymar na hazard sijui sanchez unakosea sana, hao wanamkaribia ila hawamfikii

2.pogba.... ni kiungo mzuri mshambuliaji, ananyumbulika vizuri, anapiga pasi fupi na ndefu, anajuatoa assists, anaanzisha mashambulizi pia anafanya tackling. inawezekana jose anamtumia sivyo pale man utd kulingana na falsafa yake ya soka la kujilinda anashindwa kuwa na uhuru, mda wote anakuwa na ile mentality ya kujilinda zaidi ndio maana anacheza deep sana.

3.zlatan,,,.doh namba hazidanganyi, wacha nisiongee sana ila hapa kaonewa. ninachoweza kusema jamaa ni unluck kwa sababu hajawahi kushinda UEFA na sidhan kama atashinda tena.

4. ozil mvivu flan lakin sio kwa kiwango unachokiita galasa... fuatilia records usiongee tu.

5. benzema ... hapa pengine kuna ukweli wa ulichokisema,
 
Neymar yuko vizuri, Zlatan shida ni umri ila alikuwa bonge la mchezaji labda kama umemuonea man u.. Pogba kwa aina ya uchezaji wake na nafasi yake uwanjani huwezi ona umuhimu wake moja kwa moja. Kiufupi hueleweki hata kidogo ww mchezaji mzuri unampima kwa kuangalia nini? Maana unachanganya maelezo yako mf kwa Neymar vyote muhimu unavitaja anavyo halafu unamalizia eti anapaishwa
 


Kabisa mkuu Aleyn! Mpira aliofanikiwa neimar pale Barca ni Messi ndio amefanya awe vile. Upo sahihi kabisa. Kama ni mimi ndie kocha wake ningemuanzisha Di maria/mapafu ya mbwa uone mziki wake. Halaf Sharo Neimar aingie Dakika ya 70. Sema anaangaliwa zaidi neimar, kwa style iyo wamechemsha..na UEFA wataisikia 😀😀
 
Uzi wako hauna mvuto sana baada ya kutomuandika LAUDIT MAVUGO huu mzigo uliingia Tz kwa mkwara na mbwembwe za hali ya juu Sana leo hii tunajionea matunda yake
 


Na Nyinyi Moderator Nyuzi Kama Hizi Za Kijinga Zisizo na Mantiki Mungelikuwa Munazifuta Bhana zinaboa Wasomaji.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…