Hawa ndio wasaliti wa Jose Mourinho!

Hawa ndio wasaliti wa Jose Mourinho!

TheDealer

JF-Expert Member
Joined
Nov 19, 2012
Posts
2,424
Reaction score
1,130
Watu wengi wanajaribu kujiuliza ni kwa nini Mou alifukuzwa kibaruani?

Makocha wakubwa na wachambuzi wakubwa wa soka wanatanabaisha kuwa Mou alikosa 'ufalme ndani ya dressing room'. Mnakumbuka kisa cha Mou na Iker Casillas?

Kirusi kilianza kutoka kwa Diego costa, akafuatia Cesc Fabregas, akafuata Nemanja Matic, akafuata Gary Cahill, akafuata John Terry, akafuata Branslav Ivanovic, akamalizia Eden Hazard !

Sababu ni nini?

Jibu: Kila mmoja ana sababu yake, lakini kubwa kwa Fabregas ni kitendo cha kuwekwa benchi.


====================================
Et tu, Eden: How Chelsea's betrayal of Jose Mourinho actually happened - SBNation.com
====================================

Unaweza kujiuliza ni kwanini Sir Alex Ferguson alikuwa anawauza mastaa wake. Ni kwa nini alikuwa anawapiga hata na viatu? Ni kwa nini Ronaldo ameondoka united akiwa na bifu na Alex? Ni kwa nini kipindi fulani Rooney alitaka kuondoka Man U akiwa chini ya ukocha wa Sir Alex? Ni kwa nini Sir Alex anapenda kuwabwatukia mastaa wake mafunzoni kwa sauti kubwa?

Jibu ni moja tu: Sir Alex Ferguson anaelewa kuwa wachezaji wakianza kuwa wakubwa zaidi ya kocha wao; maana yake ni kuwa atapoteza 'ufalme' wake kwenye dressing room!
 
60% ya wanachelsea hawakubaliana na uamuzi wa kumuondoa mour
 
Aende tu mpuuzi Yule anajiona yy ndio yy pumbaav mmoja
 
60% ya wanachelsea hawakubaliana na uamuzi wa kumuondoa mour

Mkuu Abromovich alikuwa na maamuzi mawili.

1. Mourhino aendelee kuwa kocha, wachezaji waliotajwa waondoke summer au january kwa bei ya hasara aanze upya kujenga timu.

Na kwa spidi hii wangeshuka daraja; manake wachezaji unawaona kabisa wanauza timu.

2. Kumfukuza Mourhino, na ndio alichofanya. Sasa angalia watakavyopiga mpira.

Abromovich wala hana haja ya kumleta Hiddink kuwa kocha mpaka mwisho wa msimu.

Angempa John Terry ukocha mchezaji kama yeye hawezi kukipanga kile kikosi mpaka mwisho wa msimu;wale wachezaji watakipiga sana sasa hivi utashangaa.

Summer angeleta kocha permanent ajenge timu yake.
 
Hizo hoja ni robo ya sababu za kumfukuza Jose

Tatizo kubwa ni yeye mwenyewe si mwingne haya ni matokeo ya alichokipanda
 
Mourinho ameharibu mwenyewe; kavuna alichopanda

Watu muwe na kumbukumbu, tatizo LA Chelsea lilianza toka wachezaji waliporudi kwa pre season, Suala LA Eva au lolote lile limetumiwa kama scape goat.

Katika mechi zote za pre season Chelsea haikushinda hata mechi moja ndani ya dakika tisini hata pale ilipocheza na vikosi vya pili vya timu za marekani huko yenyewe ikawa na kikosi kamili.

Hata kabla ya mgogoro wa Eva timu ilikuwa haiperfom.
 
Kwa CV ya mourinho hakuna mchezaji hata mmoja anayefikia pale chelsea

Kiufupi watavuna walichopanda hao THE BLUES
 
Nampenda sana Josee mkarimu, mcheshi, rafiki wa wachezaji hicho ndicho kinachomuua Mou inafikia kipindi Wachezaji wake wanamdharau anatakiwa asome alama za nyakati kuweza kuwa control wachezaji wake km kile kitendo cha Costa kiliniuzi na kuniumiza sana
 
Watu muwe na kumbukumbu, tatizo LA Chelsea lilianza toka wachezaji waliporudi kwa pre season, Suala LA Eva au lolote lile limetumiwa kama scape goat.

Katika mechi zote za pre season Chelsea haikushinda hata mechi moja ndani ya dakika tisini hata pale ilipocheza na vikosi vya pili vya timu za marekani huko yenyewe ikawa na kikosi kamili.

Hata kabla ya mgogoro wa Eva timu ilikuwa haiperfom.

mbona tuliwafunga psg??? kwenye pre-season
 
Tatizo la chelsea ni kuwa walivunjika moyo baada Mourinho kumfukuza yule daktari wa kike jamani! sasa ngoja yule daktari(Eva) arudi stanford muone vijana watakavyopiga mpira
 
Mourinho ameharibu mwenyewe; kavuna alichopanda

Bora umeamua kujitokeza kusema ukweli,Mourinho kwa power aliyokuwa nayo pale Chelsea hakuna mchezaji ambaye angeweza kumsumbua,alijisahau sana kuchukua hatua.Pia kuna issue ya discipline alikuwa anaharibu image ya klabu
 
Inanikumbusha CLAUDIO RANIERI Alivyoondoka Chelsea....wengi wenu humu mlikuwa watoto.
lakini Invisible anaweza kukumbuka

Tena Ranieri ndo aliipaisha Chelsea kabla ya noti kumtoa.
 
Last edited by a moderator:
Bora umeamua kujitokeza kusema ukweli,Mourinho kwa power aliyokuwa nayo pale Chelsea hakuna mchezaji ambaye angeweza kumsumbua,alijisahau sana kuchukua hatua.

Pia kuna issue ya discipline alikuwa anaharibu image ya klabu
Vipi game la leo?
 
Lazma utakuwa mshabiki wa Arsenal wewe 7bu ulinipa ban kisa nimeisema Arsenane
Acha kudandia gari kwa mbele utagongwa na hutafidiwa!

Mkuu Invisible ni mwenyeji wa darajani pale anapopaogopa messiana!
 
Back
Top Bottom