Hawa ndio Wasanii walioongozana na Rais ziarani Korea, Je Mnawafahamu na Wameenda kufanya nini?

Naona kila kukicha anazidi kujivunjia heshima tu,watu wana shida nyingi serikali inashindwa kutatua lakini hela zinachezewa tu kwa vitu ambavyo havina maana mara sijui goli la mama,mara sijui kusafiri na wasanii! Sasa sijui inasaidia nini!
 
Hii safari ilipangwa muda sana Ingia instagram kwenye page ya bodi ya filamu utajua

Mwaka jana walifanya mafunzo hapa mwaka huu ndio wameenda Korea

Kuhusu vigezo hapo sasa ntihani si unajua nchi imejaa wahuni hii hakuna seriousness kwenye jambo lolote

Wanachojua ni kuwafunga midomo wasemaji kwa kuwahonga ili watetee ujinga wao

Refer issue ya DP World watu wenye akili zao waliongea wee huku serikali ya samia ikutafuta namna ya kuhonga wasemaji ili watetee jambo

KAMA TAIFA TUNA SAFARI NDEFU SANA
 
Nchi itakuwaje serious kama mtu kama baba Levo anapewa coverage kwenye media?

Samia uwezo wake ni mdogo ndio maana miaka 18 tu alikuwa ashaachana na shule baada ya kufeli kidato cha nne, ndio maana machawa sasa wameligundua hilo wanamtembeza huko akapewe PhD za heshima maana za darasani asingewahi kupata maishani mwake.

Samia mwenyewe alikiri baadae alitamani kuwa mhudumu kwenye ndege hamuoni urais ni mzigo kwake?

Muwe mnafuatilia historia mengine mliyataka wenyewe
 

Kwanza kabla ujawa na wivu ujue kabisa wamejilipia wenyewe kila kitu

Na hata kama ww unataka kuwa kwenye ujumbe wa Rais inawezekana Sana

Nenda kwenye Ile Agency ya Biashara na wawekezaji jitambulishe then kila Rais akiwa anaenda sehemu flan utapata taarifa

Kama unaona hiyo Safari ina tija na kazi yako then unajiandikisha unajilipia unaenda
 
Je walikwenda kufanya nini hasa Korea? Kuimba? Ni kupoteza fedha zetu, rais anapaswa kuambatana na wataalam wa sekta mbalimbali sio hao wasanii, unafikiri nchi yetu itaendelezwa na wasanii kweli mheshimiwa rais?!
 
Angeambatana na Maghayo pia, ili amuone Jumong S Live. Maana hizi Id adriz na Mufti kuku The Infinity huwa zinamchanganya sana 😂

Cc: BICHWA KOMWE -
 
Shida ipo wapi ukitaka aende na nani...subra muhimu sana..zamu ya wengine ipo pia tuwe na subra
 
Huo msafara na huyo Raisi wameenda kwa miguu na wamejilipia gharama za Hoteli huko Seoul kutoka mifukuni mwao?!

Rais amealikwa na Rais wa Korea,

Swali ni unajua utaratibu wa Rais akialikwa sehemu?

Kama haujui then uliza
 
Ni kama namuona lamata na huyo sister wa kwenye tamthilia ya Siri
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…