Wewe mwenyewe na baba yako pia.
Badala ya kuleta mijadala ya kujadili leo na kesho nzuri ya Tanzania unataka tujadili akina nani walipendwa zaidi. Kwanini usijadili sera ya awamu ya 5 na ushauri wapi pa boreshwe kwenye awamu ya sita. Ukianza kuleta ujinga humu wa mapenzi ukijibiwa vibaya usikasirike.
Kuna vijana na watu wa hovyo sana; hasa wanaojiita wapigania mabadiliko ambayo hawayajui na ukiwauliza mabadiliko yapi utasikia tuitoe CCM madarakani ili iweje utasikia yawepo mabadiliko. Ukijiona kijana unazunguka hivyo wewe jua ni boya sana.
Fikra sahihi:
Unatakiwa kupigania maboresho ya mfumo sahihi wa uwajibikaji, uwekezaji, ushirikishwaji wa wenyeji kwenye uwekezaji, tafsiri sahihi ya uwekezaji na namna wananchi watakavyonufaika kwa mujibu wa sheria, unataka sera ipi iboreshwe na kwasababu ipi na itelelezweje. Na ukiona haitendewi haki unatakiwa ndipo uanze kuiuza sera yako mbadala kwa wananchi na wakiikubali hiyo ndiyo inaweza kutawala vizuri na wewe kushinda lakini kwa namna mlivyo sidhani kama mnalengo lolote zaidi ya kutaka kutengeneza chuki kwenye jamii. Yaani mwana Chadema amuone CCM adui suala ambalo kisera ni uasi kugombanisha watu na matokeo yake unakuwa kama uhamasishaji wa uasi. Vijana tuwe makini na hizi tabia za hovyohovyo. Mfano mimi hapa tokea dunia iumbwe sijawahi kukutana na kiongozi mtendaji. Ingawa wote walikuwa wanafanya vizuri lakini kwa JPM alitufurahisha sana licha ya hivyo vichangamoto ambavyo mama naye amekuja kwa namna nyingine kuvitatua na kuendeleza mazuri na kuufanyia kazi ushauri wa wadau mablimbali.
NB: Tuache siasa za kijinga, Tanzania ni yetu sote, tupendane, tuheshimiane, tuaminiane, tuelemishane, na tuvumiliane. Usimfanyie mtu kitu ambacho hata wewe haukipendi. Kuwa chama tawala au upinzani kwasababu ya utofauti wa itikadi usitufanye tuwe maadui. Kuna familia baba Chadema na watoto CCM au mkubwa TLP na mwingine chauma. Siasa siyo uadui.