Ukiona mtu anamchukia Samia ujue hana kazi, anafanya biashara ambazo hazina sehemu ya kupigia mapene, hana njia za kupiga pesa, hajichanganyanyi na biashara za Kinondon, Ilala na Kijitonyama.
Mimi kiukweli nisiwe mnafiq. Hakuna kipindi nimepiga madeal makubwa makubwa kama hiki. Yaani unaangalia tu wapi kuna harufu ya mzoga unakusanyika na mafisi wenzio.
Mama amefungua milango na madirisha ninyi tu hamwoni nafasi za kupigia pesa mnazubaa mpaka aje awashike mikono? Ubwege huo. Kwa sasa sisi hatugusi salary. Mimi huwa mwisho wa mwezi natoa pesa account ya salary nahamishia nyingine. Msije sema situmii salary siku zijazo.
Tunakula tuna ondoka without a trace msije chagua tena Rais kama Magufuli aje kutufunga mikono. Kwa sasa ni nguvu na uwezo wako tu wa kula. Usikae kulalamika. Piga pesa dogo. Hukuzaliwa na mtu. Shauri yako.