Hawa ni Viongozi waliotumbuliwa na hayati Magufuli kimakosa kwa sababu za kisiasa au chuki binafsi

Hawa ni Viongozi waliotumbuliwa na hayati Magufuli kimakosa kwa sababu za kisiasa au chuki binafsi

Binafsi katika watu ambao waliondoka kwenye ramani akaniuma Ni Nape Nnauye.
Huyu Jamaa ana kipaji Cha politics,Mama afanye Busara kumrudisha kwenye ramani,bado anahitajika.
Nape ndiye alienda kuomba radhi eeeh? Kamera zikamchukua toka nje kabisa.....daah walimwambia sijui apaki gari IFM ndiyo atembee....maana alikuwa amesweti sana
 
hakuna mtanzania mnafiki?
WAPO WATANZANIA SIO WANAFIKI!!! NAPE NI MNAFIKI, SI MLIMSIKIA ALIVYOKUWA ANAMSEMA VIBAYA MAGUFULI ; ALIVYOKAMATWA AKAENDA KULAMBA MIGUU YAKE KUOMBA MSAMAHA NA SASA AMEKUFA AMERUDIA TENA MCHEZO WAKE WA KUMNANGA!!!
 
Kelele tu...bandiko la kipumbavu....
Toa sabab za kwann wasingetumbuliwa
Ndio nitakuelewa kuanzia huyo wa kwanza had mwisho
 
Niwaunge mkono mkuu Mambo na LGF.

Niliwahi kuandika wakati wa mjadala wa kwa nini Dr. Malecela alitumbuliwa. Ilikuwa sahihi watumbuliwe kwa sababu katika maisha ya kawaida tu lazima unapofanya jambo lolote iwe ofisini au hata nyumbani katika ngazi ya familia, kabla hujalisemea jambo hilo jaribu kujiuliza kwa wapembeni yako kama jambo hilo likisemwa au kutendwa litaleta madhara gani kwa wtakaoona au kusikia.

Mtoto anaondoka kwenda kuomba unga kwa jirani bila mawasiliano na wazazi wake. Ingawa kweli hajaona unga na ana njaa, lakini anapaswa kuwauliza wazazi kwamba unga haupo stoo, afanyaje. Wazazi wanaweza kuwa na options, wampe hela akale mgahawani au akanunue unga. Kwenda kuomba bila kuuliza wazazi wake ni kuidhalilisha familia bila sababu.

Kutangaza maamuzi yoyote kwa umma hata kama una mamlaka, kama yupo wa juu yako, kabla hujatangaza omba ridhaa kwamba leo nataka nitangaze lile jambo tulilokubaliana. Akisema go ahead, si shida.

Unaweza kuwa na haki ya kutamka, lakini je ni wakati sahihi kutamka? Je, watu wako tayari kusikiliza? Ni vitu vidogo lakini ni muhimu kuzingatia.
 
Kwa dr ave maria semakafu alistahili kufukuzwa
Kwa kosa gani mkuu,?

Kumbuka ule ni mpango wa kitaifa wa kuboresha elimu na yeye kama katibu alikuwa anatimiza wajibu wake wa kuratibu sera na mipango chini ya wizara kuhakikisha adhima hiyo inafikiwa au unafikiri ulikuwa uamzi wake binafsi?
 
Dikteta alikuwa akitongoza mtu akimkataa lazima amfukuze
Sidhani mkuu umemsingizia hayati,ina maana hayati alimtongoza mpaka Huyo Dr semakafu?.

Mnyonge mnyongeni ila haki yake apewe jamani.
 
Sidhani mkuu umemsingizia hayati,ina maana hayati alimtongoza mpaka Huyo Dr semakafu?.

Mnyonge mnyongeni ila haki yake apewe jamani.
jiwe ndio ilikuwa tabia yake ata ukimtetea huwezi kupingana na ukweli kwamba alikuwa ana tongoza wakimkataa anawatumbua kwa vijisababu vya kizushi na kizandiki
 
jiwe ndio ilikuwa tabia yake ata ukimtetea huwezi kupingana na ukweli kwamba alikuwa ana tongoza wakimkataa anawatumbua kwa vijisababu vya kizushi na kizandiki
Najaribu kuwaza wale waliokuwa wanamkubalia anawagongea wapi na Yale maulinzi aliyokuwa nayo,.

Pia hakuwa na Yale maujanja ya watoto Wa mjini kama Uhuru kenyata na kikwete.
 
1. Dr. Nyambura Moremi
View attachment 1755243

Alikuwa ndiye mkurugenzi wa maabara ya taifa na fya ya jamii.

Alitumbuliwa kipindi janga la corona limepamba moto kwa kisingizio kwamba alipima sampuli ya ndege aina ya kware, mbuzi na mapapai vikakutwa na virusi vya corona.

Kimsingi, Dr Nyambura hakuwa na kosa bali alitimiza wajibu wake wa msingi kwa uweledi kulingana na taaluma yake kwa kuripoti majibu kadri ya kipimo kilivyoonyesha.

Itakumbukwa ni katika kipindi hicho hayati magufuli alitaka kuaminisha dunia kwamba nchi yetu haina ugonjwa korona kwahiyo hakuwa tayari kusikia taarifa yoyote juu ya uwepo wa ugonjwa huo. Hata hivyo baadae iligundulika vipimo vilivyotumika kupima sampuli vilikuwa na kasoro, hivyo Dr Nyambura alitumbuliwa kimakosa.

2. Dr Mwele Ntuli Malecela
View attachment 1755245

Alikuwa ni mkurugenzi mkuu wa taasisi ya utafiti wa magonjwa ya binadamu(NIMR).

Kipindi kumeibuka na ugonjwa usiojulikana uliohusishwa na ugonjwa wa homa ya dengue jijini Dar es Salaam, Dr mwele chini ya taasisi aliyoiongoza(NIMR) walifanya utafiti wakagundua ni ugonjwa wa zika ndipo akatangazia umma ili watu wachukue tahadhari ya kujikinga na kujilinda dhidi ya ugonjwa huo. Lakini kitendo hicho kilionekana kuwa chukizo kwa hayati magufuli akaamua kumfukuza kazi huku akimtuhumu kwamba anatumiwa na mataifa ya nje (mabeberu kama alivyopendelea kuwaita) bila ushahidi wowote wa kuthibitisha kauli yake hiyo.

Hata hivyo inasadikika kuwa kutumbuliwa kwa Dr mwele ulikuwa ni mwendelezo wa chuki binafsi ya hayati magufuli na familia ya malecela kwani hapo kabla aliwahi kumfuta kazi ya ukuu wa mkoa mama yake mwele( anne kilango malecela) kipindi cha sakata la watumishi hewa.

3. Dr Ave Maria Semakafu
View attachment 1755246


Alikuwa naibu katibu mkuu wa wizara ya elimu, sayansi na teknolojia.

Alitumbuliwa kwa kosa la kutaka kuboresha elimu ambapo awali alitangaza kufuta mafunzo na ualimu wa cheti jambo ambalo hayati magufuli aliita ni uamuzi wa kipumbavu na baadaye akamfuta kazi.

Hata hivyo, Dr Semakafu alitumbuliwa kimakosa kutokana na sababu za kisiasa kwani kwa wakati huo kampeni zilikuwa zimepamba moto hivyo hayati magufuli alifikia uamuzi wa kumfukuza Dr Semakafu kama njia ya kujitafutia kura kwa wananchi ila suala la kuboresha elimu ni miongoni mwa sera zilizoko kwenye ilani ya uchaguzi ya chama cha mapinduzi(CCM) 2020-2025 ambayo hayati mwenyewe alizunguka kuinadi nchi nzima.
Sasa wewe unataka warudishwe au unataka nini. Unasema wametumbuliwa kimakosa wewe ni mamlaka gani hadi tuamini sababu unazotoa. Nyie ndio wale wanashangilia magufuli kufariki dunia wakidhani serikali yake imepinduliwa. Samia jana kakujulisheni yeye sio mtu wenu na serikali yake ni ileile ya ccm.
 
Binafsi katika watu ambao waliondoka kwenye ramani akaniuma Ni Nape Nnauye.
Huyu Jamaa ana kipaji Cha politics,Mama afanye Busara kumrudisha kwenye ramani,bado anahitajika.
Umetumwa na mabeberu wewe. Nape mwingine au aliyezima bunge live?
 
Back
Top Bottom