Hawa ni Viongozi waliotumbuliwa na hayati Magufuli kimakosa kwa sababu za kisiasa au chuki binafsi

Binafsi katika watu ambao waliondoka kwenye ramani akaniuma Ni Nape Nnauye.
Huyu Jamaa ana kipaji Cha politics,Mama afanye Busara kumrudisha kwenye ramani,bado anahitajika.

Wengine ni malipo wa yale walofanya mfano kipindi cha uchaguzi 2015.

Waliwafanyia mambo ya ajabu wagombea wengine mfano Mamvi.

Waliwadhalilisha muno.
 
1. Dr. Nyambura Moremi
View attachment 1755243

Alikuwa ndiye mkurugenzi wa maabara ya taifa na fya ya jamii.

Alitumbuliwa kipindi janga la corona limepamba moto kwa kisingizio kwamba alipima sampuli ya ndege aina ya kware, mbuzi na mapapai vikakutwa na virusi vya corona.

Kimsingi, Dr Nyambura hakuwa na kosa bali alitimiza wajibu wake wa msingi kwa uweledi kulingana na taaluma yake kwa kuripoti majibu kadri ya kipimo kilivyoonyesha.

Itakumbukwa ni katika kipindi hicho hayati magufuli alitaka kuaminisha dunia kwamba nchi yetu haina ugonjwa korona kwahiyo hakuwa tayari kusikia taarifa yoyote juu ya uwepo wa ugonjwa huo. Hata hivyo baadae iligundulika vipimo vilivyotumika kupima sampuli vilikuwa na kasoro, hivyo Dr Nyambura alitumbuliwa kimakosa.

2. Dr Mwele Ntuli Malecela
View attachment 1755245

Alikuwa ni mkurugenzi mkuu wa taasisi ya utafiti wa magonjwa ya binadamu(NIMR).

Kipindi kumeibuka na ugonjwa usiojulikana uliohusishwa na ugonjwa wa homa ya dengue jijini Dar es Salaam, Dr mwele chini ya taasisi aliyoiongoza(NIMR) walifanya utafiti wakagundua ni ugonjwa wa zika ndipo akatangazia umma ili watu wachukue tahadhari ya kujikinga na kujilinda dhidi ya ugonjwa huo. Lakini kitendo hicho kilionekana kuwa chukizo kwa hayati magufuli akaamua kumfukuza kazi huku akimtuhumu kwamba anatumiwa na mataifa ya nje (mabeberu kama alivyopendelea kuwaita) bila ushahidi wowote wa kuthibitisha kauli yake hiyo.

Hata hivyo inasadikika kuwa kutumbuliwa kwa Dr mwele ulikuwa ni mwendelezo wa chuki binafsi ya hayati magufuli na familia ya malecela kwani hapo kabla aliwahi kumfuta kazi ya ukuu wa mkoa mama yake mwele( anne kilango malecela) kipindi cha sakata la watumishi hewa.

3. Dr Ave Maria Semakafu
View attachment 1755246

Alikuwa Naibu Katibu Mkuu wa wizara ya elimu, sayansi na teknolojia.

Alitumbuliwa kwa kosa la kutaka kuboresha elimu ambapo awali alitangaza kufuta mafunzo na ualimu wa cheti jambo ambalo Hayati Magufuli aliita ni uamuzi wa kipumbavu na baadaye akamfuta kazi.

Hata hivyo, Dkt. Semakafu alitumbuliwa kimakosa kutokana na sababu za kisiasa kwani kwa wakati huo kampeni zilikuwa zimepamba moto hivyo hayati magufuli alifikia uamuzi wa kumfukuza Dkt. Semakafu kama njia ya kujitafutia kura kwa wananchi ila suala la kuboresha elimu ni miongoni mwa sera zilizoko kwenye ilani ya uchaguzi ya chama cha mapinduzi(CCM) 2020-2025 ambayo hayati mwenyewe alizunguka kuinadi nchi nzima.
Mtoa mada, bandiko lako halina uhalisia wowote, nijuavyo mimi hawa wote walitenguliwa kutokana na kufanya makosa ya kiutendaji.
hiyo dhana ya kwamba jpm alikiwa na chuki na familia ya malecela ni uongo, mama kilango alitumbuliwa baada ya kutoa taarifa za uongo lkn kama haitoshi jpm alimpa ubinge wa kuteuliwa, iweje wewe uje uhitimishe kuwa alikuwa na chuki na malecela?
Dr mwele pia alitenguliwa kutokana na makosa yaleyale ya kiutendaji baada ya kushindwa kuwasilisha taarifa za kuwepo ugonjwa wa zika kwa wizara husika yeye kama taasisi ya utafiti na badala yake kukimbilia kwenye media na kutoa taarifa ambazo zilipaswa kutolewa na wizara.
Hili bandiko limejaa mihemuko na wala halina uhalisia wowote,usijiandikie mambo tu ukifikiri wengine hatufuatilii yanayoendelea nchini mwetu.
 
I beg to differ!! IStandWithDrMwele (RIP). DR Mwele alifanya kazi yake kimaadili kwa mujibu wa Job Description yake. Yeye alisema kwa sampuli alizoziona ameona kuna dalili za ugonjwa wa Zika. Hakusema kuna ugonjwa wa Zika, tofautisha hapo. Kabla ya kwenda kwenye vyombo vya habari, Dr Mwele alimshirikisha Waziri wake na wakakubaliana.

Ila yule MWEHU wa Chato alikuwa na sababu zake binafsi ndipo akamuta kazi.

Tafiti za sayansi hupingwa na sayansi tu na wala siyo kwa matamko ya kisiasa
 
Hatukatai kuwa Dr Mwele alikuwa mbobezi na mtaamu muhimu lqkini Dr Mwele alifanya makosa ya kikazi na hiyo ilikuwa adhabu yake.Kutangaza nchi kuwa ina ugonjwa wa Zika ilikuwa ni mbinu ya wakubwa kuiweka kqtika mpango wa chanjo ya majaribio ya hiyo Zika na Ebola.Kimsingi jambo hilo lilikuwa na athari kubwa kwa Tanzania kiusalama.
Tamko la Semakafu pia lilifanyika bila kuzingatia utaratibu na lilileta Taharuki. Na kutokana na mazingira haya baada ya Magufuli kufa nafikiri Magufuli alikuwa na maadui wengi karibu yake ambao walikuwa wanapambana kumuangusha...na ndiyo maana kwa kila jaribio Magufuli alitumia nguvu kubwa kuluzima

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kabisaaa
 
wa pili ilikuwa halali kufukuzwa hajafata sheria ya kuujulisha juu ya magonjwa ya mlipuko . ki msingi sio wajibu wake kutangaza ugonjwa wa mlipuko. kuna mwingine kma sikosei alikuwa DMO wilaya moja wapo ya jiji la Mbeya alitangaza mlipuko wa ugonjwa wa zika wakati sio jukumu lake kutangazia umma magonjwa ya mlipuko alif/utwa kazi na haibwi kokote
 
Kwa kosa gani wakati ule ulikuwa ni uamuzi wa wizara . Mawaziri na katibu mkuu mbona hawakuhusika ?!. Au anayekamatwa na ngozi ndiyo mwizi ?!

Kwa ngazi yake ya Unaibu Katibu Mkuu alikurupuka sana! Ambaye alistahili kutangaza hayo mabadiliko ni Waziri au Naibu Waziri na si mdudu mwingine yeyote kwa sababu hao ndiyo wamwaga sera wenyewe! Katibu Mkuu na Naibu wao ni watekelezaji wa Sera zilizomwagwa na waziri au naibu waziri! Kwa hiyo Dr Semakafu aliliwa kichwa kisahihi kabisaaa!

Au nasema uwongo ndugu zangu!
 
Mkuu mbona kwenye post nimeeleza in and out ilivyokuwa au umesoma kwa juu juu tu ukakimbilia kukomenti?
Nimesema by that time kulikuwa na homa iliyosaidikiwa kuwa ni dengue lakini baada ya Nimr kufanya utafiti wakagundua ni ugonjwa wa zika kumbuka dalili za ugonjwa huu na homa ya dengue zinaelekeana
Upo right mkuu, mtoa hoja hakusoma to understood but to ask questions
 
Jpm alikuwa mtu wa hovyo sana
1. Dr. Nyambura Moremi
View attachment 1755243

Alikuwa ndiye mkurugenzi wa maabara ya taifa na fya ya jamii.

Alitumbuliwa kipindi janga la corona limepamba moto kwa kisingizio kwamba alipima sampuli ya ndege aina ya kware, mbuzi na mapapai vikakutwa na virusi vya corona.

Kimsingi, Dr Nyambura hakuwa na kosa bali alitimiza wajibu wake wa msingi kwa uweledi kulingana na taaluma yake kwa kuripoti majibu kadri ya kipimo kilivyoonyesha.

Itakumbukwa ni katika kipindi hicho hayati magufuli alitaka kuaminisha dunia kwamba nchi yetu haina ugonjwa korona kwahiyo hakuwa tayari kusikia taarifa yoyote juu ya uwepo wa ugonjwa huo. Hata hivyo baadae iligundulika vipimo vilivyotumika kupima sampuli vilikuwa na kasoro, hivyo Dr Nyambura alitumbuliwa kimakosa.

2. Dr Mwele Ntuli Malecela
View attachment 1755245

Alikuwa ni mkurugenzi mkuu wa taasisi ya utafiti wa magonjwa ya binadamu(NIMR).

Kipindi kumeibuka na ugonjwa usiojulikana uliohusishwa na ugonjwa wa homa ya dengue jijini Dar es Salaam, Dr mwele chini ya taasisi aliyoiongoza(NIMR) walifanya utafiti wakagundua ni ugonjwa wa zika ndipo akatangazia umma ili watu wachukue tahadhari ya kujikinga na kujilinda dhidi ya ugonjwa huo. Lakini kitendo hicho kilionekana kuwa chukizo kwa hayati magufuli akaamua kumfukuza kazi huku akimtuhumu kwamba anatumiwa na mataifa ya nje (mabeberu kama alivyopendelea kuwaita) bila ushahidi wowote wa kuthibitisha kauli yake hiyo.

Hata hivyo inasadikika kuwa kutumbuliwa kwa Dr mwele ulikuwa ni mwendelezo wa chuki binafsi ya hayati magufuli na familia ya malecela kwani hapo kabla aliwahi kumfuta kazi ya ukuu wa mkoa mama yake mwele( anne kilango malecela) kipindi cha sakata la watumishi hewa.

3. Dr Ave Maria Semakafu
View attachment 1755246

Alikuwa Naibu Katibu Mkuu wa wizara ya elimu, sayansi na teknolojia.

Alitumbuliwa kwa kosa la kutaka kuboresha elimu ambapo awali alitangaza kufuta mafunzo na ualimu wa cheti jambo ambalo Hayati Magufuli aliita ni uamuzi wa kipumbavu na baadaye akamfuta kazi.

Hata hivyo, Dkt. Semakafu alitumbuliwa kimakosa kutokana na sababu za kisiasa kwani kwa wakati huo kampeni zilikuwa zimepamba moto hivyo hayati magufuli alifikia uamuzi wa kumfukuza Dkt. Semakafu kama njia ya kujitafutia kura kwa wananchi ila suala la kuboresha elimu ni miongoni mwa sera zilizoko kwenye ilani ya uchaguzi ya chama cha mapinduzi(CCM) 2020-2025 ambayo hayati mwenyewe alizunguka kuinadi nchi nzima.
 
1. Dr. Nyambura Moremi
View attachment 1755243

Alikuwa ndiye mkurugenzi wa maabara ya taifa na fya ya jamii.

Alitumbuliwa kipindi janga la corona limepamba moto kwa kisingizio kwamba alipima sampuli ya ndege aina ya kware, mbuzi na mapapai vikakutwa na virusi vya corona.

Kimsingi, Dr Nyambura hakuwa na kosa bali alitimiza wajibu wake wa msingi kwa uweledi kulingana na taaluma yake kwa kuripoti majibu kadri ya kipimo kilivyoonyesha.

Itakumbukwa ni katika kipindi hicho hayati magufuli alitaka kuaminisha dunia kwamba nchi yetu haina ugonjwa korona kwahiyo hakuwa tayari kusikia taarifa yoyote juu ya uwepo wa ugonjwa huo. Hata hivyo baadae iligundulika vipimo vilivyotumika kupima sampuli vilikuwa na kasoro, hivyo Dr Nyambura alitumbuliwa kimakosa.

2.
Hatimaye leo Dr Nyambura Moremi amerudi kwenye nafasi kama CEO wa National Medical Laboratory baada ya kuondolewa kwa DHULUMA na Dikteta Magufuli miaka 4 iliyopita.

FUNZO:
Ukweli ni ukweli hata kama ni wewe pekee unaoujua, useme tu.

Yule DHALIMU alitaka Nyambura Moremi aseme uwongo kuwa mashine za COVID-19 zonatoa vipimo vya uwongo ili kuhalalisha nadharia yake ya kijinga. Moremi akasimama kwenye ukweli. Akamfukuza kazi, ila yeye akafa kwa COVID-19 hiyo hiyo na Moremi leo anarudi kwenye position yake
 
Kelele tu...bandiko la kipumbavu....
Toa sabab za kwann wasingetumbuliwa
Ndio nitakuelewa kuanzia huyo wa kwanza had mwisho
Wewe ndiyo MPUMBAVU ila hujijui. Angalia Nyambura Moremi karudishwa leo
 
Wewe unataka sisi tufanyaje?!,hili linatusaidia nn sisi kama taifa?!. Kwani hao unao sema walitumbuliwa wao hizo ofisi ni Mali zao au Mali za umma!?. Wewe ulitaka wafanye kazi hapo mpk umauti uwakutie pale?!. Dah jamii forum imekusanya takataka nyingi sana,ukowemo na wewe.
 
Wewe ndiyo takataka ya kwanza katika takataka za JF
 
Kwa kosa gani wakati ule ulikuwa ni uamuzi wa wizara . Mawaziri na katibu mkuu mbona hawakuhusika ?!. Au anayekamatwa na ngozi ndiyo mwizi ?!
Muda wa kuipeleka public ile ishu ulikuwa bado ndugu. Mbaya sana Semakafu aliittoa close na uchaguzi wa 2020
 
Back
Top Bottom