Habari,
Msanii wa mziki wa kizazi kipya aliyetamba na wimbo wa Nitarejea alioshirikishwa na Diamond, Hawa Said ameangukia mikononi mwa wachungaji wapiga dili ili wamuombee baada ya kuathirika kiasi kikubwa na matumizi ya madawa ya kulevya.
Katika hali ya kustaajabisha kanisa hilo lisilo na soni liitwalo God Kind Life limemshikisha bango lenye maandishi yanayodhalilisha utu wake, kupigwa picha na kusambaza kwenye mitandao ya kijamii.
Mimi kama mtanzania sijapenda kilichofanya na kanisa hilo, haya makanisa hewa yanaudhalilisha ukristo.
Pole sana Hawa kwa kugeuzwa mtaji na wachungaji makanjanja.
Video ya Wimbo wa Nitarejea wa Diamond Platnumz alioshirikishwa mwanadada Hawa