Hawa Nitarejea wa Diamond yupo hoi kitandani, anaomba msaada wa kusaidiwa

Hawa Nitarejea wa Diamond yupo hoi kitandani, anaomba msaada wa kusaidiwa

Siku nikitoa hela Yangu kumsaidia msanii ambae alikuwa na uwezo Wa kufungua bima ya afya, naomba siku hiyo nipigwe viboko mwaka mzima.
Uyasemayo leo hata wenzio waliopatwa na maradhi yenye kuwatesa leo waliwaambia wengine wakati wa afya njema zao,kumbuka maradhi ni ibada kwa mwanadamu hata unapotoa maneno makali na dhihaka yapime na yatoe kwa kiasi binadamu ni dhaifu sana kwa mola wake huijui dakika wala saa ya mbele yako uzima na pumzi ulizopewa bure zisikupe kiburi.
 
Ni huzuni kwa kweli! Huyo amenisikitisha zaidi kwa maumivu anayoyapata mwanae ni kiasi gani mama zetu wanapata maumivu wanaonapo watoto wao tupatapo majanga,huenda binti huyu angejituliza na kuishi maisha ayatakayo mola wake basi mama yake asingemwaga machozi leo hii kumlilia mwanae anavyopata tabu,tunaamini kila tatizo ni mpango wa Muumba lkn mengine ni shetani kupitia sisi,Na hatua iliyofikia kwa mgonjwa ni matumaini yake ya kupandikizwa ini tena huduma ambayo haijulikani itaanza lini na elimu yangu ndogo ini ni moja kupandikizwa sijui itang'olewa ya nani ili apone,mwenye kuweza hilo ni mama anaeumia leo kwa matatizo aliyomkanya mtoto jana,Hatua iliyopo kwa mgonjwa ni mbaya na anapata taabu sana tumuombee tu " Kama Mwenyezi Mungu alimpa uhai zaidi ya alionao sasa basi na ampe nafuu na kumponya mjawake huyu ila kama ni muda umefika basi na amchukue kumpoza na maumivu ayapatayo leo"tunamuombea kheri ktk tiba yake,kupona kwake,na kumlejea mola wake.
Hali sio nzuri kwa kweli!
Nimeandika na kufuta kama mara sita hivi.....
 
Life has a lot of options! Within the options, problems are part of the package as well. Amongst the best is to opt 'safe/healthy life style''.

Pole sana dada Hawa. Hiyo ni mitihani ya Dunia, na kila mtihani una majibu. Kila mmoja wetu aliye hai hatujuwi kesho yetu, hatujuwi our destiny. As humans, we are all unaware of our end-results.

Mwenyezi Mungu akufanyie wepesi kwenye maradhi yako... inshaAllah.

Tumchangie chochote kile.

-Kaveli-
 
Nawaomba wasanii kwa umoja wetu tumchangie msanii mwenzetu bi hawa anaumwa Ini limevimba.Msanii huyu ndie yule aliyeimba na Msanii Diamond wimbo uitwao Nitarejea .Msanii Hawa amelazwa Hospital ya Muhimbili
 
Ungejitambulisha ww ni msanii gn ili followers wako wakuunge mkono
 
Nawaomba wasanii kwa umoja wetu tumchangie msanii mwenzetu bi hawa anaumwa Ini limevimba.Msanii huyu ndie yule aliyeimba na Msanii Diamond wimbo uitwao Nitarejea .Msanii Hawa amelazwa Hospital ya Muhimbili
mungu amjalie AFYA iliyo njema inshaalllah
 
wasanii wengi wapumbavu sana akiwepo na huyo Hawa, pombr kali tena mwanamke na ana mtoto anategemea nini, hajali malezi na carrier yake, hakujali kujitunzia heshima, leo hii analia lia, sijui kwa nini huwa hawajifunzi. Mwanamke gani anakesha bar analewa pombe kali, anavuta bangi/madawa ya kulevya leo hii anakaa anaomba kuhurumiwa, kwa wenye roho ngumu kama mimi huwa tunaishia kusema Mungu amrehemu na amsaidie kadri apendavyo Yeye
 
Mtoa mada ungejitambulisha vizuri tukakuelewa baada ya hapo utupe taratibu za kumchangia
 
Nnavyojua huyu alikua ni demu wa mond kipindi kile akaja kuwa mlevi na mtumiaji wa drugs! WCB wasijiweke pembeni ktk hili
 
Back
Top Bottom