Hawa Nitarejea wa Diamond yupo hoi kitandani, anaomba msaada wa kusaidiwa

Hawa Nitarejea wa Diamond yupo hoi kitandani, anaomba msaada wa kusaidiwa

Ningekuwa nimemhukumu, nisingemuombea hata hiyo huruma ya Mungu. Ninge'conclude kwa kusema hafai kusaidiwa ova.
Ila badala yake sijashawishi mtu alimsaidie, ila mimi sitaweza kumsaidia kwa hata 100 mbovu na kumwachia Mungu
Una hakika gani kama hiyo huruma uliyo omba kwa Mungu ime work out?
Je ww ni msafi kiasi kwamba una waombea watu wengine huruma kwa Mungu?
 
Tanzania ukisikia MTU anaomba msaada ujue alikua celebrity ( wengi wao),nadhani sasa waanzishe foundation yao mapema waende NHIF
 
Una hakika gani kama hiyo huruma uliyo omba kwa Mungu ime work out?
Je ww ni msafi kiasi kwamba una waombea watu wengine huruma kwa Mungu?

usitake nitoke kwenye mada. Mi si msafi ila mara zote nikiomba Mungu huwa anajibu na ninaimani hata kwa hili amesikia na atajibu vile apandavyo.
 


MWANAMUZIKI ambaye alishirikishwa kwenye Wimbo wa Nitarejea ya mwanamuziki wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Hawa Said hali yake imezidi kuwa mbaya baada ya kulazwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar akisumbulia na tatizo la ini.

Akizungumza na Ijumaa, mmiliki wa kituo cha kudhibiti matumizi ya madawa ya kulevya cha Pilli Missana Foundation, kilichopo Kigamboni jijini Dar, Pilli Missana alisema kuwa, tatizo la Hawa limetokana na matumizi ya madawa ya kulevya alilokuwa akichanganya na unywaji wa pombe kali.

“Unajua Hawa hali yake ilishaanza kutengamaa kabisa lakini kumbe alikuwa amepata tatizo la ini muda mrefu kutokana na unywaji wa pombe kali, kwa sasa hali yake si nzuri sana na anapatiwa matibabu katika Hospitali ya Muhimbili,” alisema Pilli.

Julai mwaka jana, Hawa alijitokeza hadharani na kuomba msaada baada ya kuathiriwa na unywaji wa pombe kali za kienyeji pamoja na madawa ya kulevya ambapo alipatiwa msaada na Kituo cha Pilli Missana na hali yake kuanza kuimarika kabla ya kupata tatizo jingine la ini.

Tumewachoka kwanini wanaotembeza bakuli kila kikicha wanakuwa hao hao,wacha wapambane na hali zao wenyewe.
 
Hawa wapuuzi hawastahilo huruma, huu ni wakati wa kila mtu kupambana na hali yake, pesa za kubwia unga kama nyoka angelipia bima ya NHIF saa hizi asingetuletea huu upuuzi wake.
Tena hii tabia ikome.
Omba Mungu akupe mwisho mwema.
Ww hujui hatma yako itakuwaje.
Weka maneno ya akiba.
 
download (2).jpg
images (3).jpg


Hawa wa 'Diamond' msanii wa Bongo fleva aliyeimba na msanii maarufu Diamond Platnumz wimbo wa Nitarejea kwasasa anahitaji msaada wa hali na mali kutokana na hali yeke ya kaifya kwa sasa,Akihojiwa na kipindi cha Shelawadu Hawa akiwa nyumbani na mama yake alionekana akiwa katika maumivu makali sana huku akionekana akiwa na tumbo kubwa sana na alipohojiwa na mtangazaji w akipindi hicho alisema amaekuwa akipata matibabu yake katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa kutolewa maji kila yanapojaa na hakuna lingine zaidi ya hilo na alipohojiwa zaidi alisema kuwa ameambiwa ini lake ni kubwa na halifanyi kazi vizuri hivyo atakuwa anatolewa maji tu ingawa anasema kuwa aliuliza kama kuna tiba nyingine akaambiwa ni kubadili ini na kuweka ini lingine lakini kwasasa huduma hiyo haitolewi Muhimbili labda mpaka mwakani.

Nadhani wengi wamesaidiwa na wadau au serikali kwa sababu sauti zao zilisikika na wenye mamlaka mfano mzuri ni Wastara sasa na huyu ni msanii na mtanzania ambaye naye anahitaji msaada wa hali na mali hasa msaada wa tiba na inavyoonekana kwasasa ni tiba ya ini au kubadili ini yaan Liver transplant kazi ambayo haifanyiki Tanzania mpaka huko nje ya nchi.
Nadhani wadau wanaohusika ni muhimu sasa kuangalia jinsi ya kumsaidia huyu dada ambaye anaangamia taratibu huku akiona kama sasa mwisho wa maisha yake umefika kama kuna uwezekana wa kufanya jambo kwa binti huyu basi tufanye sasa ili kuokoa maisha yake.
 
Back
Top Bottom