Nadhani tunapindisha habari ama tunaingilia fani zisizo zetu. Inawezekana kabisa Polisi wakawa wanakosea kwa namna moja ama ingine, lakini sidhani kama baadhi ya mambo tunayojadili hapa JF kuhusiana na hii kesi yapo sahihi.
Sasa hebu tuangalia hoja zako juu ya hili na kuona kama mwenzetu hii fani "yako"!
Naungana moja kwa moja na Polisi kumshikiria huyo kijana aliyemrecomend houseboy wa kwa Balozi kwanza; Yeye kama 'mdhamini' nina hakika alimrecomend vizuri (+ve) na ndio kisa akapewa kazi ya uhausiboy, na ninahisi ktk kumdhamini huko alihakiki kuwa liable kwa lolote litalotendekana na kijana huyo akiwa kazini nyumbani kwa huyo balozi mpaka hapo atapoamua kufuta udhamini wake.
This is one of the worst assumption ever attempted.. from recommendation to patronage of sort inashangaza. Tangu lini mtu aki mrecommend mtu kupata ajira mahali fulani basi anakuwa liable na kila anachofanya mtu huyo kwenye ajira mpya? Hata mzazi akimtafutia mtoto wake kazi mahali na yule mtoto akaboronga au akafanya uhalifu kamwe hatumshikilii mzazi!
Zaidi ya yote "hisia" zako kuwa huyo aliyerecommend aliingia kama makubaliano fulani kuhusu "lolote" litakalotokea nyumbani kwa Balozi ni hoja isiyo na msingi. Mtu pekee anayewajibika na yote yaliyotokea kwa kumwajiri Mabakuri ni Balozi Daraja peke yake na peke yake tu unless wakati anakubaliana kumwajiri huyo kijana kuna mtu alimshikia bunduni kwenye kisogo cha kichwa chake kumlazimisha amuajiri.
Na hujagusia suala la kabila la kijana kuingizwa katika hili kiasi kwamba wanataka sasa kuwafanya watu wote wa kabila hilo wanaoishi maeneo ya balozi daraja kuwa "possible suspects".
Yote mawili hayakubaliki na yanaonesha kile ambacho tunaweza kukiita "kitovu cha uzembe"; yaani matumizi mabaya ya madaraka.
Sasa MKJJ, kama mtu kamdhamini mtu, kwa nini asiwehojiwe na Polisi huenda akawa na taarifa zozote kuhusiana na houseboy huyo (Si lazima zihusiane na case at hand), Back ground yake na kadha wa kadha. Je anafikiri anaweza kupatikana wapi na vitu kama hivyo.
Hakuna mahali popote ambapo imewaidia kuwa anayeshikiliwa alimdhamini huyo kijana zaidi ya kumtafutia ajira mahali ambapo yeye mwenyewe aliwahi kufanya kazi.
Ninachofikiri mimi huyu yupo Kimahojiano (ushahidi) zaidi na siyo mshtakiwa. Nisahihishwa kama nimekosea tafadhali.
Fikra zako hazina msingi katika kile kinachosemwa hadi hivi sasa. Hakuna haja ya kukusahihisha kwani ungefuatilia toka mwanzo kisa hiki wiki moja iliyopita hadi leo hii kijana anatafutwa kwa kutuhumiwa kuhusika na mauaji na siyo kusaidia uchunguzi au kwa sababu za kimahojiano. As a matter of fact wangetoa tu na picha yake (wanaweza wasiwe nayo) na while they are at it wamtangaze kuwa ni "wanted dead or alive" na kuwa kuwa yuko "armed and dangerous"! Ili watakapomuona wasimpe nafasi ya kujieleza bali wammalize tu watuoneshe mwili wake!
Suala la Waziri Mramba hapa lipo nje kabisa, hata sijui umeliingizaje? Lets talk kuhusiana na kifo cha huyu Mama tu.
Huwezi kuona kuingiliana kwa hili kwa sababu unajaribu kutenganisha mambo yanayohusiana kwa kuyaangalia moja moja na hivyo kujikuta kila linapokuja jingine unaanza upya!
Hakuna sababu za kukamata waliowkisha fanya kazi kwa Daraja, though Polisi wanaweza kuchunguza waliokwisha fanya kazi kama kuna ulazima huo, and may be wanachunguza, who knows.
Kwanini ni sehemu ya uchunguzi as a matter of fact mtu wa kwanza kutakiwa kutoa maelezo na kubanwa alikuwa awe ni spouse yaani Daraja. You have to eliminate him from possible suspects ndio uweze kufocus kwa wale wengine. Hadi hivi sasa sijaona mahali popote ambapo Daraja amesafishwa kutokuhusika (siyo kwa sababu ya maelezo yake kuwa alikuwa Muheza na kuwa mtumishi wa nyumbani anahusika) bali kwa ushahidi wa kisayansi wenye kushawishi akili, kukubaliana na ushahidi na usiokuwa na kujipinga.
Huyo kijana hajakamatwa kwa vile ni kabila moja na houseboy wa Balozi, bali anashikiliwa kwa vile ndiye alimdhamini houseboy huyo .
Hii ni sababu ambayo wewe unaitoa. Kwa maelezo yao inaonekana amekamatwa viile vile kwa sababu kabila lake linahusiana na huyo kijana; vinginevyo unaweza vipi kuelezea kauli hii:
"The two are from the same tribe according to police." Why mention the tribes of the two individuals if it is not relevant to the investigation?
Hii inaondoa dhana kwamba Polisi watakamata kabila zima. See the link kati ya houseboy na huyo jamaa anayeshikiliwa utaiona, unless uamue kuwa mbishi tu.
Ndio kawaida ya baadhi yetu, tunapenda mepesi mepesi mtu akikubana unakimbilia "mbishi, wivu, anajifanya anajua sana!" just answer the arguments presented, show them how weak they are, I will respond to yours and let the best argument win. Otherwise stop whining.
Binafsi nasema, inawezekana kweli houseboy akahusika na mauaji hayo ndio maana kakimbia/haonekani.
Inawezekana ameuawa vile vile baada ya kutekwa na kamwe hatopatikana milele na wauaji wanaangalia pembeni huku wakitabasamu!
Sijui kwa nini Mume wa marehemu asihojiwe. Kwa habari ilivyo kwenye magazeti, hainiingii akilini, unless kama waandishi wameiweka ndivyo sivyo,kama ambavyo nilifikiri nilipoona hili bandiko, nikajua kweli Polisi wamemkamata jamaa vile tu ni kabila moja na suspect (houseboy), kumbe sivyo.
wao wenyewe ndio wamesema hilo la ukabila kwani miye nimelitunga toka ndotoni? Ati hujui kwanini mume wa marehemu asihojiwe au hata dereva wake.. do you want me to list some few possible reasons kwanini hadi kina Mkapa wanamlaumu House Boy? inanikumbusha suala la mauaji yaliyodaiwa kufanywa na Ditopile.. viongozi wa serikali wakaanza kutoa pole kwa Ditopile! hadi tulipowaweka sawa hapa hapa JF
RIP Mrs. Daraja[/QUOTE]