Hawa Standup Comedy wa Tanzania, nyie wana JF wanawachekeshaga?

Troublemaker

JF-Expert Member
Joined
Jun 8, 2015
Posts
20,834
Reaction score
40,641
Hell...

Nazungumzia hawa kama wanajiita sijui Watubaki na cheka tu. Naonaga matangazo yao kiukweli naona watu wanacheka vitu ambavyo hata havichekeshi.

Au ni mimi ndiye nina stress. Maana ule ni usimuliaji tena hata kwa vitu havichekeshi. Na style ni stori utotoni ilikua hivi mara vile.
 
Watu Huwa wanaenda na Vicheko vyao pale..

Ukisema uende Umenuna utarajie wao ndiyo wakuchekeshe haitawezekana Mkuu..

Mtu Jana umelala na Njaa, Mke amekukimbia na Watoto, Baba Mkwe bado anakusumbua umalizie Mahari.. Mchepuko amekutumia Meseji haoni siku zake, Boss amekupa Overtime ila amegoma kuongeza malipo... Ukiwa na Hali hii pale usiende Kisha utarajie kuchekeshwa...
 
Ongezea baba mwenye nyumba anataka KODI yake

Hapo kucheka ni ngumu maana maisha yako yanachekesha ila unashindwa kucheka iweje ukacheke kiholela
 
Comedy inahitaji watu wenye akili sana, wachekeshaji wengi wa Tanzania ni watu wenye akili kidogo.
 
Hamnaga kitu mule aisee. Watafute ploti tu waanze kulima nyanyachungu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…