Wanajukwaa, nina imani wote mko sawa.
Pasipo kupoteza muda, naomba niingie kwenye mada tajwa hapo juu.
Binadam kwa kawaida, huwa na hulka ya kulipiza kisasi kwa aliyemkosea au adui yake. Hiki ndicho kinajidhihirisha kwa viongozi wetu, hasa wabunge, maana kila anayesimama anakuja na hoja ya kuwakomoa wananchi badala ya kutafuta namna ya kuwapunguzia makali ya maisha.
Mengi yamekuwa yakijadiliwa na wabunge wetu hasa yenye mlengo wa kuwakandamiza wananchi wao tena "waliowachagua kwa kishindo"!
Hivi wabunge wetu hasa hasa mwalunyege anajua hatari ya kuendesha bodaboda?! Anajua matibabu ya mifupa gharama yake? Anajua kwamba asilimia kubwa waendesha bodaboda wanatakiwa kurudisha rejesho kila siku kwa wamiliki wa hizo bodaboda? Hivi anajua kwamba wengi huwa wanaingia kuendesha bodaboda kama option ya mwisho baada ya njia nyingine zote za ajira kushindikana?
Jamani Wananchi wenzangu, ifike mahali tuwaombe msamaha hawa viongozi wetu hasahasa watunga sheria wetu "tuliowachagua wakatuwakilishe", watusamehe pale tulipowakosea, vinginevyo tutafika 2030 tumechakaa sana.
Nawasilisha.