Hawa wa Nitarejea kupelekwa India kwa matibabu,Diamond kutoa zaidi ya mil 50

Pole sana HAWA..[emoji20]

..ile video ya wimbo Nitarejea uliitendea haki[emoji120]
 
Mungu akuponye Hawa uwe mzima na usirudie hivyo vitu.
 
Mwenyezi Mungu amrehem
Hawa watu ni wajinga Sana
Wanatumia madawa alaf wakiumwa watanzania nao ooooh sijui diamond amsaidii mwenzie Kwan yeye alimtuma akale hizo mihadarati,
Wakt mungine nikuacha mtu akalipa na maisha yake,
Pathetic.
 
Hongera zake kwa msaada.... lakini mwisho wa siku Hawa alitumia madawa kwa utashi wake, hata angempotezea sioni kama kuna shida hapo. Kila mtu awajibike na maisha anayochagua
umenena vyema, ila kuna jirani yangu mwanaye alikuwa mwizi kupindukia (alikuwa anaitwa mama genai) siku moja mwanaye alipgwa hoi jeshi la polisi likamuokoa, mimi nilimsindikiza mama mzazi kwenda kumuona mwizi aliyepgwa hospitali, nkamwambia mama tunachofanya ni kupingana na jamii kwani ni mwizi ukiingia kwenye 18 zake anaweza kukutoa uhai, majibu aliyonipa mama ndo nataka nkushirikishe wewe, aliniambia hivi,
1. uwe na roho kikristo na usifurahie mtu kupotea katika uovu. tenda wema kama msamaria japo ni ngumu lakini thawabu utazipata mbele.
2. binadamu kwa asili ni mwovu, lakini uchungu wa maumivu kwa mzazi ni sawa sawa na mtoto mwingine hata kama alikuwa kibaka.
niliona anazingua sana. tulivyofika hospitali mama wa mtoto ambaye ni mwizi, alisema kuwa kila siku anamwomba Mungu mtoto wake abadilike lakini sijui ni ile hali ya kukataliwa toka kwa baba yake..
kiufupi. kuwa na roho ya huruma hata kidogo kama angekuwa nduguyo wa damu au mtoto wako usingethubutu kusema haya.
 
Asante sana Diamond kwa kuonyesha huruma Mungu atakurudishia ulichotoa msaidie huyo dada Hawa.
 
Kumtibu x wako ni tahfifu ndio maana tunashauriwa tusiachane kwa ugomvi huwezi jua mtakutana wapi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…