Hawa wachina wanaharibu uchumi wa Nchi yetu


Unajua kitu kinaitwa Competitive advantage mkuu?Au ukiona tu tuna malighafi unaona kila kitu tunaweza kuzalisha?

Dunia inakimbia sana,tatizo si tuna amini kwamba mkishakua na malighafi tu then lazima nchi iwe tajiri,sa hivi service based industries zina-boom kuliko hata hizi manufacturing based industries ila sisi tumekomaa na tunayo yaamini tu.
 

Nilichomaanisha ni kwamba hata nikimsikiliza hapo simuoni kama ni intellectual,no wonder hata msikitini waliona anawarushia tu wakamlamba kibao heavy.
 
Tumia lugha ya staha kidogo Mkuu utaeleweka tu sio lazima uniharibie siku yangu

Nimekusoma comment yako Kuhusu Nyerere kuamua kufuata left wing na kuachana na right wing,lkn Mzungu na mchina ni wale wale wote wabaya, hakuna hata mmoja wao angalau basi mwenye lengo zuri na Africa au Tanzania yetu

Wote hawa wanakuja kupora kwa kalamu na ubabe

Ndio nimeshauri hapo juu kuwa baadhi ya bidhaa ambazo zinapatikana hapa nchini ziwekewe kiwango cha kuagiza pale kwenye upungufu kwenye soko la ndani

Kwa kuwa bado hatuwezi kuvimbishiana vifua na china kwenye uzalishaji viwandani
Kwa wakati huu
Ni bora serkali ikaweka nguvu kwenye mazao ya kipaumbele kwa ajili ya export, mfano Korosho na pamba na tumbaku ili kuipatia Nchi fedha ya kigeni
 
Nilichomaanisha ni kwamba hata nikimsikiliza hapo simuoni kama ni intellectual,no wonder hata msikitini waliona anawarushia tu wakamlamba kibao heavy.
Acha uongo. Nimekufahamisha wapi alilambwa kibao na kwa nini au hujayapenda?

Huyo ambae si "intellectual" aliwekwa na nani madarakani? Hahaha, THE only intellect in the world.

Nafahamu inauma bado, stahamili tu utazowea.

Nafahamu unaelewa kasema nini kwenye hiyo video clip na ni "taboo" kuyasikiliza hayo kwa watu kama wewe. Bado inauma?
 
Nadhani China ilianza kwa kumiliki makampuni makubwa ya ujenzi ambayo yalienda overseas hasa Africa na asia ndio walipoanza kuboom

Kwakuwa serkali ya Tanzania bado ni vigumu kufinance kila individual intellectuals
Ni bora ingetengeneza kampuni za umma kwa projects mbali mbali ambazo zinakuwa 100% financed na serkali lengo ikiwa ni kuhskikisha wanachukua creams kwa ajili ya kufanya local projects ili fedha yetu isitoke nje iendelee kujenga uchumi wa Nchi

Kuanzia barabara, majengo,kilimo,nk
Kuwekezwe kitaalamu na sio kimazoea
 
Uvivu ndiyo unakufanya ufikirie hayo. Nani kaandika "left wing" na "right wing"? Kwani naandika kuhusu mechi ya Simba na Yanga hapa? Unanini wewe?

Nyerere kama kuomba omba misaada alienda kote. Umesahau ya Kennedy au siku hizo ulikuwa bado wewe tulipoletewa msaada wa chakula kwa hisani ya watu wa USA?

Lugha mbaya nimeanza mimi au wewe uliyesema unanyonywa? Si wewe vile vile huwa unasema mabeberu, umesahau? Hivi ulikuwa hujuwi kazi ya beberu ni nini? Kupanda tu.

Lugha msizozipenda muanzishe wenyewe halafu mlalamike. Hukuandika wewe kuwa mchina anakunyonya?
 

Ebu jaribu kuwapa huo ushauri labda wakakusikia...
Wengine tukijaribu tunaambiwa tumetumwa na mabeberu!
 
Service based is industries inaenda km mapacha manufactured based industries

Mfano kwenye service inategemea manufactured ili iweze kupaform

Ili uweze kutoa huduma kwa Wananchi wako lazima utengeneze miundo mbinu bora itakoyoalocate resources kabla ya kuanza kuzalisha au kupata faida kwenye service based industries

Angalia China wanaipromote ligi ya mpira wa miguu iwe ligi bora kwa miaka 50 ijayo,lkn walianza na kujenga miundo mbinu kwanza na kuandaa vijana ambao watakuwa competitive hii Ndio naweza kuiweka kwenye service based industries

Kwani sisi tunashindwa nini?
 

Ni kweli kabisa ni taboo kwangu kama ilivyoo taboo pale msikitini kwa yale mazungumzo aliyoyazungumza mpk akalambishwa ile alamba alamba.

Ni mwendo wa taboo kila sehemu.
 
Kuna pombe inaitwa burudani ukinywa unaeongea kama Huyu jamaa,we una kiwanda hapa?mifuko ya kubebea vitu tu mmeagiza viwanda vya china watengeneze.
 
Ni ajabu, kuona CCM wanajaribu kuwa kataa Marafiki wetu wa ukweli.
 
Zungumzeni yote lakini mimi konde langu nalitupia mtanzania mwenyewe, mpenda dezo dezo, mla rushwa katika "service provision based industries", mfanya "boycott" na "sabotage" katika "goods manufacturing based industries". Mchina ni Mbaya ndiyo ila Mtanzania ni mbaya zaidi sawa na nyani achekaye la mwenzie bila kujua lake likoje! Kule Madagascar wakati wanamuuzia Mchina kahawa kwa vikombe wanajua ubaya wake hata kabla ya harakati za uhuru, wakikwepa vipimo vya mzani. Hakuna kesho tuanze leo kujisahihisha kuondoa ubinafsi wetu kwanza. Tunajihujumu wenyewe.
 
Kabisa Mkuu, ukiangalia sekta ya Ujenzi Wachina wametawala si kwa sababu wazawa hawana uwezo wa kujenga barabara bali ni kuwa wao wamewezeshwa. Wana benki ambazo zinawapa Bondi na mitaji bila dhamana. Wanapata unafuu wa kuingiza bidhaa kutoka kwao,

Katika hali Kama hii Mkandarasi mzawa atashindana vipi? Hata Sheria ya manunuzi ya margin of preference haifuatwi.
 
Wachina ndiyo marafiki wa Kweli nyie
wazee wa lumumba..... So mtuliee tuli

Ova
 
Wana manufacturing industry sijui unategemea nini, sasa vitu vinunuliwe wapi? Hatutengenezi hata cover za simu peke yake alafu unasema wazuie importation? Biidhaa 99% zinazonunuliwa kutoka nje hakuna mtu anatengeneza Tanzania na ni vitu vya muhimu watu wanahitaji ndiyo maana wafanyabiashara wana import. Vingekuwepo viwanda vya ndani vinatengeneza same product labda, ila kwa kua hakuna huwezi zuia. Zuia vitu ambavyo vipo ndani, mfano huwezi kuta mtu anaenda China kununua maziwa au cement huku Tanzania vipo.
 

Kibaya zaidi over 70% ya bidhaa hizo ni fake na TBS yetu wakiwa wanalipwa mishahara yao!
 
umeongea point zuri sana. ila utekelezaji waki unahitaji akili sana. na katika utawala huu hakuna mwenye akili ya kuweza kuona hilo na kulifanyia kazi kwa njia inayoweza kunufaisha watazania. kwanza kitu kinacho takiwa kufanyiwa kazi ni kufanya utafiti vitu vinaweza kuzalishwa nchini natukajitosheleza. kwa kuanzia tuweke kiwango cha juu kwa kitu chocho kinacho tengenezwa nje nakuja kuuzwa nchini.
 
China baada ya kuachana na Ukomunisti mkongwe na kuingia Uchumi wa Kibepari walianza kwa kusomesha watu wao wawe na ujuzi wakutosha na pia Makampuni makubwa ya nje yaliyokuwa yakifanya miradi China ilikuwa lazima kuwa na wabia wa Kichina Kama Supplier au Subcontractor. Baada ya muda wakajenga uwezo na kuwa na viwanda vya msingi Kama spares na malighafi nyingine. Waliendelea kukazia Sheria ikawa ili kiwanda kiweze kuwekeza lazima malighafi na vipuri vitoke humo humo ndani. Katika kufanya hivyo wakajikuta wanakuwa na viwanda na malighafi za kutosha pia Makampuni yao yakawa makubwa kiasi yakaanza kushindana na Makampuni ya Magharibi hadi leo.

Tunachotakiwa kufanya hapa si kurudisha Mashirika ya Umma, Bali Ni kuwawezesha Makampuni ya Wazawa katika miradi mikubwa pawe na ubia kisheria. Chukulia ujenzi wa SRG na Rufiji, Kama Wazawa wangepewa japo asilimia 30, ingelikuwa pesa nyingi Sana na wangejenga uwezo wa kuweza kufanya makubwa.
 

Mkuu haya ni matokeo ya hulka ya kikoloni na kibaguzi tuliyojengewa kwa miaka mingi...
Yaani ni kama pale kwenye familia yenu... Hamjiamini kiasi kila kitu na huduma zote muhimu mnategemea kutoka familia nyingine??
Sasa kwa nini muendelee kuitwa familia?? To
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…