Hawa waimbaji wa injili mbona wana mapozi tata sana?

Hahaha
Kweli ulijua vitu vingi.
Yule dada, kuna bro wangu alikuwa ana msifia enzi hizo, bas shemeji akamwambia ukiendelea kumsifia huyo dada huu mkanda natupa.
Mi hapo sikuwa na elewa sana ila nilivo kuwa mkubwa nikikumbuka nacheka sana, that girl was cute!!
 
Hahaha. Ila jamii forum hii ina mambo kweli..

Basi haya
 
wew mwenyew unafananaje![emoji50][emoji50][emoji50][emoji50]mie nawaona kawaida sana
 
Naongea kwa uchungu kwasababu mimi dunia ninaijua sana, waimbaji wengi wa gospel siku hizi hawamwimbii Mungu, wanatafuta pesa na ni vijana wasio na Roho wa Mungu bali wanaimba kama wanavyofanya bongo fleva tu. hawaimbi kama huduma. wamevamia dunia wakati wao hawatakiwi kuwa wa dunia hii. wamesahau kwamba shetani ameleta mapandikizi hapa duniani ili kunajisi wanadamu, mapandikizi kwa njia ya nguo, vipodozi,aina ya maneno ya kutumia/lugha etc, mafuta n.k ambavyo vingine vinakuwa programmed kuzimu kabisa na vinaletwa hapa duniani na maajenti ili wale wanaojifanya watu wa Mungu wakijihusisha navyo wanachafuka nafsi, wanakuwa najisi na Mungu hawatumii tena.

amini usiamini, wapo wanatinda nyusi, wanapaka poda, wananyoa minyoo ya kihuni, wanavaa mavazi ya kihuni, wanatunga nyimbo za kihuni, wanacheza kihuni kuliko hata watu wa dunia (wanacheza vibaya kuliko hata waimba taarabu), nyimbo zao hazina upako bali zina maudhui ya kawaida ya dunia hii tu.

lakini katika kufanya hivyo, hawajui kabisa. mwingine akikuangalia utafikili shogaa, kwa jinsi alivyovaa, alivyojikubua usoni, alivyopakaa poda, alivyopakaa lipstick mdomo unanona, alivyojiweka ni shetani kabisa, lakini yeye hajijui, ameenda kimwili shetani akamvika vazi la kishetani ili aiaibishe njia ya Mungu. ni sawa na unapomchukua mshamba kijijini ukamleta hapa bongo, yeye ni mwanaume ukamvalisha gauni ukamdanganya kuwa hiyo ni kanzu ya pwani we vaa tu nenda sokoni, atavaa, moyoni yeye hana nia mbaya wala hana uchafu wowote, ila watakaomwangalia watamuona shogaa. ndivyo ilivyo kwa hawa, ninaamini wengi sio wakameroon, ila wanavyojipodoa kwa uwongo wa shetani na wachungaji wao kwamba unatakiwa kuwa smart, usmart ule wanaiga ule wa dunia ambao shetani amewavalisha maajenti wake waimba bongo fleva, wao wanavaa vilevile na kubehave vilevile, kumbe hawajui wao ni tofauti kabisa na wapo ulimwengu mwingine. mioyoni mwao hawako wakameroon, ila wamevalishwa mavazi na shetan anayowavalisha watu wa aina hiyo. ndio maana kumekuwa na allegation nyingi sana kwa watu kadhaa ambao sitawataja hapa, kwamba hawaeleweki, sisi tunaowafahamu tunajua wanaeleweka lakini kwa jinsi wanavyojiweka na kubehave kwa kuifuata namna ya dunia hii, kunafanya watu wasiwaelewe na wasione tofauti kati yao na wao. hawa wasitegemee kwamba Mungu anawatambua, katu, Mungu sio vuguvugu kiasi hicho.

Biblia inasema wala tusifuatishe namna ya dunia hii....., unajua dunia inabadilika kila siku, lakini watu wa Mungu hatutakiwi kubadilika kwasababu sisi tunaye Roho wa Mungu ambaye habadiliki. ukiongozwa na Roho hautabadilika hata pale dunia hii itakapobadilika. tatizo ni kwamba kati ya watu 100 katika kanisa, wale wanaoongozwa na Roho, wanaotembea kiroho hawazidi watatu. ndio makanisa ya siku hizi. ndio maana utakuta kanisani wanawake wamevaa vibaya, wachungaji nao wamevaa mavazi ya kumeremeta kama wanamuziki wa congo, wanawaza hela tu badala ya kutengeneza roho. Mungu atusaidie.
 
Tena rose ndio huwa simuelew kbs anakata mauno cjaonaa
 

Hahahaha aisee kumbe dada tulikuwa tunampenda wengi ...Mimi nilijiapiza kabisa siku naona lazima niende kwa madiba nikamate mzulu wangu yote kwa sababu ya kumpenda huyo dada

Or else Ethiopia acha tu
 
Ndio maana nasikiliza mapigano ulyankulu. ( mwenye mamlaka yote)
Tumaini kwaya Arusha (shangilieni )

Yaani napenda Sana hizo kwaya za zamani.
Sijawahi kuchoka kisikiliza kwaya ya Tumaini-Shangilieni, naweza kuingia You tube hata siku nzima nasikiliza tu nyimbo zao.

Nawapenda sana pia walinilea kwani karibu waimbaji wote pale walinifahamu tangu nikiwa mdogo.
 
Sijawahi kuchoka kisikiliza kwaya ya Tumaini-Shangilieni, naweza kuingia You tube hata siku nzima nasikiliza tu nyimbo zao.

Nawapenda sana pia walinilea kwani karibu waimbaji wote pale walinifahamu tangu nikiwa mdogo.
Mkuu kuna hii kwaya inaitwa Kilimanjaro kwaya (kutubu dhambi na kuziacha )

Ningeomba ingia YouTube usikilize.
Katika kwaya zote nilizosikiza na mama yangu hii iko juu ya yote .
 
Mkuu kuna hii kwaya inaitwa Kilimanjaro kwaya (kutubu dhambi na kuziacha )

Ningeomba ingia YouTube usikilize.
Katika kwaya zote nilizosikiza na mama yangu hii iko juu ya yote .
Kutubu dhambi na kuziacha si ni ya Tumaini? Au waliirudia?
 
Ndio maana nasikiliza mapigano ulyankulu. ( mwenye mamlaka yote)
Tumaini kwaya Arusha (shangilieni )

Yaani napenda Sana hizo kwaya za zamani.
Hzo nyimbo hunikumbusha utotoni hazichoshi kuimba na kusikiliza, kwaya ya mamajusi, kijitonyama, wale walioimba mwana mpotevu, nyimbo za zamani zilikua na upako sana, za sasa nyingi magumashi matupu.
 
Sijawahi kuchoka kisikiliza kwaya ya Tumaini-Shangilieni, naweza kuingia You tube hata siku nzima nasikiliza tu nyimbo zao.

Nawapenda sana pia walinilea kwani karibu waimbaji wote pale walinifahamu tangu nikiwa mdogo.
Hyo kwaya kiboko ukisikiliza unaguswa kabisa moyoni.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…