king otaligamba
JF-Expert Member
- Oct 24, 2016
- 2,178
- 2,033
Na katakundu umesahau mkuu!!!!Lips shedo,nyusi katinda na lamba lipsi huyu jamaa kuna namna sio bure!
Search Tumaini kwaya Arusha...utaona nyimbo zao mkuu.Hiyo Shangilieni imo youtube?
Cc: Otorong'ong'o umenifanya nitafute CD kwa ajili ya huo wimbo tu.Kuna ule wimbo...
"jamani shangwe, shangwe tushangile, simba wa Yuda kaaja kwa unyonge..."
Huo wimbo naweza sikiliza hata mara mia...
Huo uzi tukianzisha hatutaki mjaidina achangie chochote...akichangia hatumjibu wala kumqoute.Umeongea point...
Kuna mjitu kama Faizafoxy ikion huo uzi atasababishwa ufungiwe
Sasa ukitaka uwe na siku nzuri ya furaha haswaa nenda Radio Habari Maalum (RHM) waombe wakupe nyimbo za harusi za kwaya ya 1990-1998 hivi.Nyimbo za siku hizi ni biashara kuliko kuabudu.
Wanarudia mstaria mmoja mara mia ili wimbo ukolezee wauze.
Sintokaa nizinunue mi bado na selection yangu ya kwaya za zamani mama alinipa. Na bado zipo kwenye kanda.
Wewe tuko pamoja nduguHahaha...why not Rose Muhando?
Mimi katika nyimbo za Gospel zinazonibariki ni
Kwanza kwaya karibu zote za zamani. Hasahasa miaka ya 90-99 kama za Arusha mjini na Shangilieni. daaah
Pili, nyimbo za baadhi ya waimbaji wachache sana kama Christina Shusho, Abihudi Misholi, Ephraim Mwansasu na Bahati bukuku.
Lastly, ni nyimbo zote za kuabudu.
Hahaa watu wa zamani kigogo hawa. Hiyo siyakudumisa hata niliiimba. Umenikumbusha mbali sanaaHahaha
We jamaa mkongwe una wafaham holy cross chair
Walinishika sana, walikuwa wana wimbo wao unaitwa siyakudumisa,
Mwingine my fav Ngena nathi
Hahaha zamaniii sanaaa.
Ubarikiwe ndugu kwa mahubiri yako mazuri.Naongea kwa uchungu kwasababu mimi dunia ninaijua sana, waimbaji wengi wa gospel siku hizi hawamwimbii Mungu, wanatafuta pesa na ni vijana wasio na Roho wa Mungu bali wanaimba kama wanavyofanya bongo fleva tu. hawaimbi kama huduma. wamevamia dunia wakati wao hawatakiwi kuwa wa dunia hii. wamesahau kwamba shetani ameleta mapandikizi hapa duniani ili kunajisi wanadamu, mapandikizi kwa njia ya nguo, vipodozi,aina ya maneno ya kutumia/lugha etc, mafuta n.k ambavyo vingine vinakuwa programmed kuzimu kabisa na vinaletwa hapa duniani na maajenti ili wale wanaojifanya watu wa Mungu wakijihusisha navyo wanachafuka nafsi, wanakuwa najisi na Mungu hawatumii tena.
amini usiamini, wapo wanatinda nyusi, wanapaka poda, wananyoa minyoo ya kihuni, wanavaa mavazi ya kihuni, wanatunga nyimbo za kihuni, wanacheza kihuni kuliko hata watu wa dunia (wanacheza vibaya kuliko hata waimba taarabu), nyimbo zao hazina upako bali zina maudhui ya kawaida ya dunia hii tu.
lakini katika kufanya hivyo, hawajui kabisa. mwingine akikuangalia utafikili shogaa, kwa jinsi alivyovaa, alivyojikubua usoni, alivyopakaa poda, alivyopakaa lipstick mdomo unanona, alivyojiweka ni shetani kabisa, lakini yeye hajijui, ameenda kimwili shetani akamvika vazi la kishetani ili aiaibishe njia ya Mungu. ni sawa na unapomchukua mshamba kijijini ukamleta hapa bongo, yeye ni mwanaume ukamvalisha gauni ukamdanganya kuwa hiyo ni kanzu ya pwani we vaa tu nenda sokoni, atavaa, moyoni yeye hana nia mbaya wala hana uchafu wowote, ila watakaomwangalia watamuona shogaa. ndivyo ilivyo kwa hawa, ninaamini wengi sio wakameroon, ila wanavyojipodoa kwa uwongo wa shetani na wachungaji wao kwamba unatakiwa kuwa smart, usmart ule wanaiga ule wa dunia ambao shetani amewavalisha maajenti wake waimba bongo fleva, wao wanavaa vilevile na kubehave vilevile, kumbe hawajui wao ni tofauti kabisa na wapo ulimwengu mwingine. mioyoni mwao hawako wakameroon, ila wamevalishwa mavazi na shetan anayowavalisha watu wa aina hiyo. ndio maana kumekuwa na allegation nyingi sana kwa watu kadhaa ambao sitawataja hapa, kwamba hawaeleweki, sisi tunaowafahamu tunajua wanaeleweka lakini kwa jinsi wanavyojiweka na kubehave kwa kuifuata namna ya dunia hii, kunafanya watu wasiwaelewe na wasione tofauti kati yao na wao. hawa wasitegemee kwamba Mungu anawatambua, katu, Mungu sio vuguvugu kiasi hicho.
Biblia inasema wala tusifuatishe namna ya dunia hii....., unajua dunia inabadilika kila siku, lakini watu wa Mungu hatutakiwi kubadilika kwasababu sisi tunaye Roho wa Mungu ambaye habadiliki. ukiongozwa na Roho hautabadilika hata pale dunia hii itakapobadilika. tatizo ni kwamba kati ya watu 100 katika kanisa, wale wanaoongozwa na Roho, wanaotembea kiroho hawazidi watatu. ndio makanisa ya siku hizi. ndio maana utakuta kanisani wanawake wamevaa vibaya, wachungaji nao wamevaa mavazi ya kumeremeta kama wanamuziki wa congo, wanawaza hela tu badala ya kutengeneza roho. Mungu atusaidie.
Kuna AIC shinyanga na KKKT kijitonyama wanaimba rohoni pia.huwa nasikiliza nyimbo za
1. marehemu fanuel sedekia,
2. chang'ombe vijana na ile kubwa, na
3. ULYANKULU- barabara ya 13(mapigano)
Nakuelewa sanaa. Sijui kama vijana / watoto wa leo wanapata malezi kiasi gani ya kuwaivisha kiroho kiasi hiki na kuwaacha na kiu ya kutamani injili ya nyimbo pindi waachanapo na wazazi wao kama tulivyokuwa sisi. Inasikitisha sana. Nathubutu kusema tulilelewa. Mungu awabariki sana wazazi wetu. Dunia ya leo kama hukuivishwa lazima upotee tu. Hakuna namna.Kuna ya kwaya kuu Arusha na Kilimanjaro kwaya.
Ukiwa unaserch usisahau kuweka Kilimanjaro kwaya kutubu dhambi na kuziacha.
Imo nyimbo nyingi tu.Hiyo Shangilieni imo youtube?
Kuna nuhu, habari ya mwana mpotevu, na ile ya isaka duh harariCc: Otorong'ong'o umenifanya nitafute CD kwa ajili ya huo wimbo tu.
Pia nimefurahi sana kupata wadau wa nyimbo za kwaya za zamani.
Katika nyimbo za hao waimbaji, kuna ule wa
"Nakulilia Jehovaa, uko wapii messiah mbona u mbali nami bwanaa"
Katika huo wimbo na kinanda kinavyopigwa daah.
Naukubali sana shangilieniKuna ule wimbo...
"jamani shangwe, shangwe tushangile, simba wa Yuda kaaja kwa unyonge..."
Huo wimbo naweza sikiliza hata mara mia...
IPO album nzimaHiyo Shangilieni imo youtube?
Mmh binamu basi umri wako c haba, unakimbizana na jide itakua, aaaahSijawahi kuchoka kisikiliza kwaya ya Tumaini-Shangilieni, naweza kuingia You tube hata siku nzima nasikiliza tu nyimbo zao.
Nawapenda sana pia walinilea kwani karibu waimbaji wote pale walinifahamu tangu nikiwa mdogo.
Gozbrert katosha humuKumbe ni hao...
Ndio maana napenda sana kwaya kuliko waimbaji binafsNakuelewa sanaa. Sijui kama vijana / watoto wa leo wanapata malezi kiasi gani ya kuwaivisha kiroho kiasi hiki na kuwaacha na kiu ya kutamani injili ya nyimbo pindi waachanapo na wazazi wao kama tulivyokuwa sisi. Inasikitisha sana. Nathubutu kusema tulilelewa. Mungu awabariki sana wazazi wetu. Dunia ya leo kama hukuivishwa lazima upotee tu. Hakuna namna.
Anzisha Uzi Maalumu,na Kisha Ututag Tuliochangia Katika Uzi Huu,Tuweke Audios,Videos na Picha za Old Schools za Gospel...Najua na Wengine Watavutiwa Kuja Kuuchangia na Kuuongezea Nyama!IPO album nzima
Tuanzishe Uzi Maalumu wa "Old School Gospels za Tanzania" na Kisha Watu Wachangie Kwa Kuweka Audios,Videos na Picha za Kwaya Hizo!Na Nina Uhakika Kuna Watu Baki Wataongezea Nyama Katika Uzi Huo!Ndio maana napenda sana kwaya kuliko waimbaji binafs
Waimbaji binafs nawakubali hawa
Ambwene Mwasongwe
Joshua Mlerwa
Shusho
Wengine wapiga hela tu