Hawa waimbaji wa injili mbona wana mapozi tata sana?

Hawa waimbaji wa injili mbona wana mapozi tata sana?

Kuna ule wimbo...
"jamani shangwe, shangwe tushangile, simba wa Yuda kaaja kwa unyonge..."

Huo wimbo naweza sikiliza hata mara mia...
Cc: Otorong'ong'o umenifanya nitafute CD kwa ajili ya huo wimbo tu.

Pia nimefurahi sana kupata wadau wa nyimbo za kwaya za zamani.

Katika nyimbo za hao waimbaji, kuna ule wa

"Nakulilia Jehovaa, uko wapii messiah mbona u mbali nami bwanaa"

Katika huo wimbo na kinanda kinavyopigwa daah.
 
Nyimbo za siku hizi ni biashara kuliko kuabudu.
Wanarudia mstaria mmoja mara mia ili wimbo ukolezee wauze.

Sintokaa nizinunue mi bado na selection yangu ya kwaya za zamani mama alinipa. Na bado zipo kwenye kanda.
Sasa ukitaka uwe na siku nzuri ya furaha haswaa nenda Radio Habari Maalum (RHM) waombe wakupe nyimbo za harusi za kwaya ya 1990-1998 hivi.

Hizo nyimbo hata you tube haziko ila baadhi ya wachungaji wana record zao.

[emoji445] Bwana harusi sikiliza....huyo ndiye wakoo...

Umekabidhiwa rasmi leo...umtunze, umlinde, sawa kama mboni ya jicho lako [emoji445]


Huo wimbo ukiupata utafurahi.
 
Hahaha...why not Rose Muhando?

Mimi katika nyimbo za Gospel zinazonibariki ni

Kwanza kwaya karibu zote za zamani. Hasahasa miaka ya 90-99 kama za Arusha mjini na Shangilieni. daaah

Pili, nyimbo za baadhi ya waimbaji wachache sana kama Christina Shusho, Abihudi Misholi, Ephraim Mwansasu na Bahati bukuku.

Lastly, ni nyimbo zote za kuabudu.
Wewe tuko pamoja ndugu
 
Naongea kwa uchungu kwasababu mimi dunia ninaijua sana, waimbaji wengi wa gospel siku hizi hawamwimbii Mungu, wanatafuta pesa na ni vijana wasio na Roho wa Mungu bali wanaimba kama wanavyofanya bongo fleva tu. hawaimbi kama huduma. wamevamia dunia wakati wao hawatakiwi kuwa wa dunia hii. wamesahau kwamba shetani ameleta mapandikizi hapa duniani ili kunajisi wanadamu, mapandikizi kwa njia ya nguo, vipodozi,aina ya maneno ya kutumia/lugha etc, mafuta n.k ambavyo vingine vinakuwa programmed kuzimu kabisa na vinaletwa hapa duniani na maajenti ili wale wanaojifanya watu wa Mungu wakijihusisha navyo wanachafuka nafsi, wanakuwa najisi na Mungu hawatumii tena.

amini usiamini, wapo wanatinda nyusi, wanapaka poda, wananyoa minyoo ya kihuni, wanavaa mavazi ya kihuni, wanatunga nyimbo za kihuni, wanacheza kihuni kuliko hata watu wa dunia (wanacheza vibaya kuliko hata waimba taarabu), nyimbo zao hazina upako bali zina maudhui ya kawaida ya dunia hii tu.

lakini katika kufanya hivyo, hawajui kabisa. mwingine akikuangalia utafikili shogaa, kwa jinsi alivyovaa, alivyojikubua usoni, alivyopakaa poda, alivyopakaa lipstick mdomo unanona, alivyojiweka ni shetani kabisa, lakini yeye hajijui, ameenda kimwili shetani akamvika vazi la kishetani ili aiaibishe njia ya Mungu. ni sawa na unapomchukua mshamba kijijini ukamleta hapa bongo, yeye ni mwanaume ukamvalisha gauni ukamdanganya kuwa hiyo ni kanzu ya pwani we vaa tu nenda sokoni, atavaa, moyoni yeye hana nia mbaya wala hana uchafu wowote, ila watakaomwangalia watamuona shogaa. ndivyo ilivyo kwa hawa, ninaamini wengi sio wakameroon, ila wanavyojipodoa kwa uwongo wa shetani na wachungaji wao kwamba unatakiwa kuwa smart, usmart ule wanaiga ule wa dunia ambao shetani amewavalisha maajenti wake waimba bongo fleva, wao wanavaa vilevile na kubehave vilevile, kumbe hawajui wao ni tofauti kabisa na wapo ulimwengu mwingine. mioyoni mwao hawako wakameroon, ila wamevalishwa mavazi na shetan anayowavalisha watu wa aina hiyo. ndio maana kumekuwa na allegation nyingi sana kwa watu kadhaa ambao sitawataja hapa, kwamba hawaeleweki, sisi tunaowafahamu tunajua wanaeleweka lakini kwa jinsi wanavyojiweka na kubehave kwa kuifuata namna ya dunia hii, kunafanya watu wasiwaelewe na wasione tofauti kati yao na wao. hawa wasitegemee kwamba Mungu anawatambua, katu, Mungu sio vuguvugu kiasi hicho.

Biblia inasema wala tusifuatishe namna ya dunia hii....., unajua dunia inabadilika kila siku, lakini watu wa Mungu hatutakiwi kubadilika kwasababu sisi tunaye Roho wa Mungu ambaye habadiliki. ukiongozwa na Roho hautabadilika hata pale dunia hii itakapobadilika. tatizo ni kwamba kati ya watu 100 katika kanisa, wale wanaoongozwa na Roho, wanaotembea kiroho hawazidi watatu. ndio makanisa ya siku hizi. ndio maana utakuta kanisani wanawake wamevaa vibaya, wachungaji nao wamevaa mavazi ya kumeremeta kama wanamuziki wa congo, wanawaza hela tu badala ya kutengeneza roho. Mungu atusaidie.
Ubarikiwe ndugu kwa mahubiri yako mazuri.
 
Kuna ya kwaya kuu Arusha na Kilimanjaro kwaya.

Ukiwa unaserch usisahau kuweka Kilimanjaro kwaya kutubu dhambi na kuziacha.
Nakuelewa sanaa. Sijui kama vijana / watoto wa leo wanapata malezi kiasi gani ya kuwaivisha kiroho kiasi hiki na kuwaacha na kiu ya kutamani injili ya nyimbo pindi waachanapo na wazazi wao kama tulivyokuwa sisi. Inasikitisha sana. Nathubutu kusema tulilelewa. Mungu awabariki sana wazazi wetu. Dunia ya leo kama hukuivishwa lazima upotee tu. Hakuna namna.
 
Cc: Otorong'ong'o umenifanya nitafute CD kwa ajili ya huo wimbo tu.

Pia nimefurahi sana kupata wadau wa nyimbo za kwaya za zamani.

Katika nyimbo za hao waimbaji, kuna ule wa

"Nakulilia Jehovaa, uko wapii messiah mbona u mbali nami bwanaa"

Katika huo wimbo na kinanda kinavyopigwa daah.
Kuna nuhu, habari ya mwana mpotevu, na ile ya isaka duh harari
 
Kwa hao wawili kweli lazima usikilize maneno ndio ujue wanamwimbia Mungu lkn bila kusikia maneno ni bongo freva
 
Nakuelewa sanaa. Sijui kama vijana / watoto wa leo wanapata malezi kiasi gani ya kuwaivisha kiroho kiasi hiki na kuwaacha na kiu ya kutamani injili ya nyimbo pindi waachanapo na wazazi wao kama tulivyokuwa sisi. Inasikitisha sana. Nathubutu kusema tulilelewa. Mungu awabariki sana wazazi wetu. Dunia ya leo kama hukuivishwa lazima upotee tu. Hakuna namna.
Ndio maana napenda sana kwaya kuliko waimbaji binafs

Waimbaji binafs nawakubali hawa
Ambwene Mwasongwe
Joshua Mlerwa
Shusho


Wengine wapiga hela tu
 
Ndio maana napenda sana kwaya kuliko waimbaji binafs

Waimbaji binafs nawakubali hawa
Ambwene Mwasongwe
Joshua Mlerwa
Shusho


Wengine wapiga hela tu
Tuanzishe Uzi Maalumu wa "Old School Gospels za Tanzania" na Kisha Watu Wachangie Kwa Kuweka Audios,Videos na Picha za Kwaya Hizo!Na Nina Uhakika Kuna Watu Baki Wataongezea Nyama Katika Uzi Huo!
 
Back
Top Bottom