Hawa wakubwa wanachanganya sana; wamekutana Ujerumani jana kuzungumzia kuijenga upya Ukraine. US$200 bl yapendekezwa!

Hawa wakubwa wanachanganya sana; wamekutana Ujerumani jana kuzungumzia kuijenga upya Ukraine. US$200 bl yapendekezwa!

NIMEONA

JF-Expert Member
Joined
Aug 4, 2019
Posts
3,862
Reaction score
5,693
Mkutano uliitishwa na Chancellor wa Ujerumani na kuhudhuriwa na wajumbe wa NATO wote (source: StarTV habari, BBC na AlJazeera). Swali langu ni kuwa kwani vita imeisha au hii ina maana gani?

Au ndo kweli kama wanavyosema wengine kuwa walikuwa kwenye majaribio yao ya silaha na sasa wameshapata majibu wanarudi kuendelea na mishe zingine?
 
Waziri Mkuu mpya wa Uingereza Rishi Sunak ameshasema wazi kwamba sera ya Uingereza kuhusu kuisadia Ukraine kivita iko palepale.

Na Ujerumani na Marekani bado wana mpango wa kutuma Air Defense Systems zingine, sasa vita vinaishaje bwana.
 
... wakati wewe mchana huu unapanga bajeti ya kupata kitoweo cha jioni hii, wakubwa wanapanga bajeti za miaka 5, 10, 25, 50, hadi 100 ijayo even beyond ambazo hadi vizazi watakuja kuzitekeleza! Hiyo ndio tofauti na huwezi elewa!
 
Ulaya, huu mgogoro wa nishati unaowazuga leo,hawakuwahi uona miaka ya nyuma ?
 
Ulaya, huu mgogoro wa nishati unaowazuga leo,hawakuwahi uona miaka ya nyuma ?
Unapozungumzia nishati mbona Ulaya all options are on the table? Kama kuna vitu viko well planned Ulaya ni suala la nishati; and the energy master plan is so clear. Sio sisi huku hatujui tushike lipi tuache lipi; kila mmoja anakuja na sera yake.
 
Ulaya, huu mgogoro wa nishati unaowazuga leo,hawakuwahi uona miaka ya nyuma ?
Ulaya hii hii wamewahi kupitia dhiki na tabu ambazo sisi bado hatujafikia ikichangiwa pia na hiyo hali yao ya hewa.

Hayo maendeleo waliyonayo leo hayajawanyeshea tu kama mvua wameyapata kwa m'binde na wala hiyo kupungukiwa gesi wakati wa winter sio tishio kubwa sana kwao kama Mujahedeen wanavyojaribu kudanganya hapa.
 
Back
Top Bottom