Hawa waliomshangilia kwa bashasha Waziri wa Fedha Jana pale Kwenye Mkutano ni wafanyabiashara wa wapi? Modarators huu uzi usiunganishwe.

busar

JF-Expert Member
Joined
Dec 22, 2011
Posts
1,071
Reaction score
1,067
Nimefuatilia kikao kile, nimesikiliza hoja za wale wafanyabiashara, nikaona masikitiko yao. Lakini wakati wa kuagana na baada ya PM kuwa ameondoka jukwaa likavamiwa na wafanyabiashara waliojaa bashasha na nderemo wakimpongeza Waziri wa fedha. Leo naona ile clip yenye nderemo iko pinned kwenye official accounts za MoF. Sasa ninajiuliza mabadiliko ya haraka ya vilio mbele ya Waziri Mkuu hadi furaha za bashasha ile jioni. Wale vijana ni wa wapi?
 
waTanzania wengi hamuelewi tofauti ya Mwigulu waziri na Mwigulu kama mtu..... Kwenye kikao zile hasira na mapovu yalielekezwa kwa Mwigulu waziri ila maadam kikao kimeisha Ina maana Sasa Wanaongea na Mwigulu kama mtu. Ndio Sasa wanataniana and selfie kama zote.

Ndio maana hata Simba na yanga tambo na matusi huwa mengi ila mechi ikiisha unaona viongozi na wachezaji wanasalimiana na vicheko juu.

Tutofautishe Siasa NA Ukarimu wa waTanzania.
 
Kabisa, nimekusoma
 
Kuna tofauti Kati ya maisha binafsi ya mtu mtaani na huko ofisini
 
Created!

Sent from my Infinix X6511B using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…