ngulyabhule
JF-Expert Member
- Apr 5, 2020
- 344
- 712
Kumeibuka ushindi mkubwa sana kwa huyu mchambuzi anayeitwa Dullah heavy weight wa Wasafi dhidi ya msemaji wa Yanga bwa mdogo Ali Kamwe. Wakati Dullah akiweka uchambuzi wake alibase kwenye facts anazo ziona na uhalisia wake alianzia kwenye asilimia 10 kwa Yanga vs Simba. Ali Kamwe akaibuka kwa kejeri yakatokea ya Dullah kuwa mshindi. Dullah akaja na Kocha hatoboi October Ali Kamwe akaja kwa kejeli zile zile kwamba "walisema October hatoboi si huyo hapa mwalimu na kuipamba klabu kuwa inafanya mambo kwa weledi" analisema hili ilhali October haijakwisha na taarifa ya klabu jana imemfurumusha mwalimu. Swali langu hawa wasemaji ni wachumia tumbo, ama taaluma mbovu au ni watu wasio na aibu au ni vile hawawezi kuusema ukweli hata kama wanaujua?! Mwisho wa siku binafsi naweza ona aibu watu wa nje kuyasema na kuyajua vema mambo ya mpira kuliko wasemaji wa klabu husika. Na hili limetokea kwa wasemaji wengi sana wa vilabu vya hapa Tz. Binafsi sisiti kusema ufike wakati hiki kitengo kitolewe ama kifanyiwe mabadiriko makubwa.