Hawa wasemaji wa vilabu vya soka ni njaa au taaluma mbovu?!

Sasa ndugu ulitaka Ali Kamwe akubali kwamba Kocha hatoboi October, uliona wapi hiyo.

Lakini pia kejeli, majigambo, dharau ni sehemu ya mpira wa bongo.
 
Ally kamwe ni staff wa yanga, kuna ethics ya namna ya ku-handle taarifa za ndani na nje!! Staff anaweza kuvujisha taarifa za ndani kwa mtu ambaye sio staff ili kuwaanda audience na taarifa rasmi ya nje, vile unaona kamwe sometimes anatetea vitu vilivyo wazi wkt ukweli anaujua bayana, ni namna ya kuishi na ethics sio busara kamwe ashabikie eti manqoba hatoboi october na wakati haijawa rasmi.
 
Kumeibuka ushindi mkubwa sana kwa huyu mchambuzi anayeitwa Dullah heavy weight wa Wasafi dhidi ya msemaji wa Yanga bwa mdogo Ali Kamwe. Wakati Dullah akiweka uchambuzi wake alibase kwenye facts anazo ziona na uhalisia wake alianzia kwenye asilimia 10 kwa Yanga vs Simba. Ali Kamwe akaibuka kwa kejeri yakatokea ya Dullah kuwa mshindi. Dullah akaja na Kocha hatoboi October Ali Kamwe akaja kwa kejeli zile zile kwamba "walisema October hatoboi si huyo hapa mwalimu na kuipamba klabu kuwa inafanya mambo kwa weledi" analisema hili ilhali October haijakwisha na taarifa ya klabu jana imemfurumusha mwalimu. Swali langu hawa wasemaji ni wachumia tumbo, ama taaluma mbovu au ni watu wasio na aibu au ni vile hawawezi kuusema ukweli hata kama wanaujua?! Mwisho wa siku binafsi naweza ona aibu watu wa nje kuyasema na kuyajua vema mambo ya mpira kuliko wasemaji wa klabu husika. Na hili limetokea kwa wasemaji wengi sana wa vilabu vya hapa Tz. Binafsi sisiti kusema ufike wakati hiki kitengo kitolewe ama kifanyiwe mabadiriko makubwa.
Kwahiyo unadhani alipaswa kusema.." ni kwelii, huyu kocha mwezi wa kumi hatoboiii, me nawaambiaa, mtayakumbuka maneno yanguu"

Na mahali pengine unafikiri alipaswa aseme "Aisee sisi yanga kwenye derby hatutoboii, yaani tuna asikimia 10 tuu, hatutoki nawaambiaa"

Au tuandikie wewe alivyopaswa kujibu, akiwa ni msemaji wa club
 
Alafu Hawa wachambuzi muda mwingi wanatumia hisia zaidi Kama huyu dullah heavy weight Kuna siku alisema dumbia nikama cristian Ronaldo.ukitaka uchambuzi MZURI fuatilia hizi media kongwe Kama clouds, East Africa,TBC lakini hizi nyingine zinatafuta views YouTube
 
Kwahiyo unadhani alipaswa kusema.." ni kwelii, huyu kocha mwezi wa kumi hatoboiii, me nawaambiaa, mtayakumbuka maneno yanguu"

Na mahali pengine unafikiri alipaswa aseme "Aisee sisi yanga kwenye derby hatutoboii, yaani tuna asikimia 10 tuu, hatutoki nawaambiaa"

Au tuandikie wewe alivyopaswa kujibu, akiwa ni msemaji wa club
Mtoa uzi ni mjinga sana
Anaweka hisia kwenye eneo ambalo huitaji hisia

Kuna msimu ahmed ali alisema bado wananafasi ya kuchukua ubingwa ilihali nafasi ilikuwa haipo

Sasa yeye anataka msemaji aiponde timu yake na aungane wanaoiponda timu yake ili wamfurahishe yeye

Alitaka ali kamwe aungane na dullah mwezi wa tisa kwamba manqoba hatoboi ni mambo ya hovyo sana
 
Pana jambo hunielewi tangu hapo juu hoja yangu hata kama yeye anajua timu mbovu sasa why awajibu wachambuzi ? Maana yangu akikaa kimya kuna shida?
 
Mtoa uzi ni mjinga sana
Anaweka hisia kwenye eneo ambalo huitaji hisia

Kuna msimu ahmed ali alisema bado wananafasi ya kuchukua ubingwa ilihali nafasi ilikuwa haipo

Sasa yeye anataka msemaji aiponde timu yake na aungane wanaoiponda timu yake ili wamfurahishe yeye

Alitaka ali kamwe aungane na dullah mwezi wa tisa kwamba manqoba hatoboi ni mambo ya hovyo sana

Hisia umezileta wewe sijui kichwani mwako umejaa makamasi badala ya ubongo! Kwani Dulla aliposema Yanga mbovu yeye Ali angekaa kimya kungeleta video ya sasa ambayo Dullah anatamba nayo?! Hivi unatumia kiungo gani kifikiria?!
 
Kwahiyo unadhani alipaswa kusema.." ni kwelii, huyu kocha mwezi wa kumi hatoboiii, me nawaambiaa, mtayakumbuka maneno yanguu"

Na mahali pengine unafikiri alipaswa aseme "Aisee sisi yanga kwenye derby hatutoboii, yaani tuna asikimia 10 tuu, hatutoki nawaambiaa"

Au tuandikie wewe alivyopaswa kujibu, akiwa ni msemaji wa club

Si kila maneno ya haters yanahitaji kujibiwa ni sawa na wewe mtu akuambie mkeo mbaya sawa si wako yeye unamjibu ili iweje?! Ndiyo naana yangu sasa sijui kama umenielewa?
 
Ali kamwene yupo kazini,na huyo mchambuzi yupo kazini.
Ali kamwene hawezi kusema kuwa kocha atafukuzwa.japo anajua.
 
Hisia umezileta wewe sijui kichwani mwako umejaa makamasi badala ya ubongo! Kwani Dulla aliposema Yanga mbovu yeye Ali angekaa kimya kungeleta video ya sasa ambayo Dullah anatamba nayo?! Hivi unatumia kiungo gani kifikiria?!
Anakaaje kimya ilihali ni msemaji wa timu
 
Ni msemaji wa timu siyo mchambuzi wa timu mambo ya kuwajibu wachambuzi siyo usemaji ! Kula ya wachambuzi hapa Tz inategemea sana hizi timu mbili sasa hivi yule Dullah anavimba kisa tu alijibiwa na Ali na yeye kuonekana mshindi
 
Kumeibuka ushindi mkubwa sana kwa huyu mchambuzi anayeitwa Dullah heavy weight wa Wasafi dhidi ya msemaji wa Yanga bwa mdogo Ali Kamwe. Wakati Dullah akiweka uchambuzi wake alibase kwenye facts anazo ziona na uhalisia wake alianzia kwenye asilimia 10 kwa Yanga vs Simba. Ali Kamwe akaibuka kwa kejeri yakatokea ya Dullah kuwa mshindi. Dullah akaja na Kocha hatoboi October Ali Kamwe akaja kwa kejeli zile zile kwamba "walisema October hatoboi si huyo hapa mwalimu na kuipamba klabu kuwa inafanya mambo kwa weledi" analisema hili ilhali October haijakwisha na taarifa ya klabu jana imemfurumusha mwalimu. Swali langu hawa wasemaji ni wachumia tumbo, ama taaluma mbovu au ni watu wasio na aibu au ni vile hawawezi kuusema ukweli hata kama wanaujua?! Mwisho wa siku binafsi naweza ona aibu watu wa nje kuyasema na kuyajua vema mambo ya mpira kuliko wasemaji wa klabu husika. Na hili limetokea kwa wasemaji wengi sana wa vilabu vya hapa Tz. Binafsi sisiti kusema ufike wakati hiki kitengo kitolewe ama kifanyiwe mabadiriko makubwa.
Hiyo ni idara ya propaganda ya timu. Usitegemee sana kusikia mambo technical, otherwise wewe ndio ujui haya mambo vizuri inakubidi ujifunze.
 
Nimekupa hoja nawe weka hapa hoja yako na si kuandika as if umekalia kitu chenye ncha kali!
Yule ni msemaji sasa kama hujui kazi ya msemaji
Sasa ulitaka ali kamwe aiponde Yanga ndo maana nikakuambia hamnazo

Kazi ya msemaji ni kuitetea timu inaposhambuliwa mtandaoni ina maana na hili hulijui ndo maana nikakuita hamnazo

Yaani timu ipondwe mtandaoni hata kama wananchoongea ni kweli msemaji unakaaje kimya

Mimi sijui kutukana na sijafundishwa kutukana kama unategemea na mimi ntaporomosha matusi pole sana
 
Kumeibuka ushindi mkubwa sana kwa huyu mchambuzi anayeitwa Dullah heavy weight wa Wasafi dhidi ya msemaji wa Yanga bwa mdogo Ali Kamwe. Wakati Dullah akiweka uchambuzi wake alibase kwenye facts anazo ziona na uhalisia wake alianzia kwenye asilimia 10 kwa Yanga vs Simba. Ali Kamwe akaibuka kwa kejeri yakatokea ya Dullah kuwa mshindi. Dullah akaja na Kocha hatoboi October Ali Kamwe akaja kwa kejeli zile zile kwamba "walisema October hatoboi si huyo hapa mwalimu na kuipamba klabu kuwa inafanya mambo kwa weledi" analisema hili ilhali October haijakwisha na taarifa ya klabu jana imemfurumusha mwalimu. Swali langu hawa wasemaji ni wachumia tumbo, ama taaluma mbovu au ni watu wasio na aibu au ni vile hawawezi kuusema ukweli hata kama wanaujua?! Mwisho wa siku binafsi naweza ona aibu watu wa nje kuyasema na kuyajua vema mambo ya mpira kuliko wasemaji wa klabu husika. Na hili limetokea kwa wasemaji wengi sana wa vilabu vya hapa Tz. Binafsi sisiti kusema ufike wakati hiki kitengo kitolewe ama kifanyiwe mabadiriko makubwa.
Aibu naona mie huku jamani mpaka sasa sijaamini kwamba kocha kanyolewa October hii 😢😢😢😢
 
Mimi huwa nawashangaa sana watu. Eti mtu umeangalia mpira, ukaona kila kitu, halafu unakuja kushangaa eti mtu amekaa anasubiri uchambuzi kutoka kwa wengine. Yaani uchambuliwe wakati unaona kabisa mpira unavyoendelea wazi wazi kabisa.
 
Yule ni msemaji sasa kama hujui kazi ya msemaji
Sasa ulitaka ali kamwe aiponde Yanga ndo maana nikakuambia hamnazo

Kazi ya msemaji ni kuitetea timu inaposhambuliwa mtandaoni ina maana na hili hulijui ndo maana nikakuita hamnazo

Yaani timu ipondwe mtandaoni hata kama wananchoongea ni kweli msemaji unakaaje kimya

Mimi sijui kutukana na sijafundishwa kutukana kama unategemea na mimi ntaporomosha matusi pole sana

Ndiyo maana anapoteana na kuonekana hovyo mbele ya wachambuzi kwa sababu ya kutetea mambo ambayo hata mwenda wazimu anaweza ng'amua. Haya aitetee sasa kauli yake aliyo ikanusha kuwa kocha hafukuzwi.
 
Back
Top Bottom