Hawa watu wanastahili wamefanya kazi kubwa na ngumu kweli kweli

Hawa watu wanastahili wamefanya kazi kubwa na ngumu kweli kweli

Mi mi

JF-Expert Member
Joined
Jul 14, 2024
Posts
2,748
Reaction score
5,112
Hawa watu wameacha alama isiyofutika katika mataifa yao.

Maana kazi waliyofanya ilikuwa ngumu na kubwa haswa.

Vita ya kupambana dhidi ya umasikini ni vita ngumu inahitaji viongozi wenye akili ya kuwaonea huruma watu wake na kuwatoa walipo pasipo kujali njia gani kutumika bali matokeo ya njia hiyo.

Nakili hawa mabwana kichwani zilikuwamo za kutosha.

Deng Xiaoping mkomunisti halisi aliyekubali kuvua koti la kiitikadi lililo kuwa linambana huku hali za kimaisha za watu wake wachina zikiwa mbaya akaona hakuna namna bali kutumia njia yoyote jambo muhimu ni kuwa itawaokoa watu wake.

Aliziba pamba masikioni mwake hata pale alipoitwa bepari na wakomunisti wenzake na kushughulikiwa haswa wakati wa cultural revolution lakini hakukata tamaa bali aliendelea kuamini kuwa ukomunisti China unahitaji mawazo mapya.

Deng wa China alibadili taswira nzima ya ujamaa na ukomunisti aliiokoa China iliyokuwa inatumbukia.

Pamoja na ushenzi wake mkubwa uliotia doa utawala wake China 1989 pale Tianmen Square ambao umeacha historia chafu maana haukuwa usiku wa kawaida pale Beijing bali ulikuwa usiku mzito kwa wanafunzi waliojongea katika maeneo yale.

Licha ya hayo yote iwe ni mpenda demokrasia,iwe ni mpenda udikteta na hata uwe usiependa chochote hakika utaheshimu kazi ya huyu bwana mchina mfupi kutoka kabila la Hakka kwa hakika alibadili China na kuwapiga chenga ya mwili maadui wote wa China ikiiongozwa na magharibi mpaka leo.
licensed-image.jpeg


Lee Kuan Yew Bwana mdogo aliyeshuhudia ukatili wa Japan na historia mbaya ya ukoloni kwa jamii yake Singapore.

Kukabidhiwa kijieneo masikini yeye na chama chake PAP kilicho jaa chungu ya matatizo, kukosekana umoja baina ya jamii tatu kubwa malay,Chinese,Indians kushindwa kuweza kuendelea katika Federation of Malaya na kuondoka na kuanza na kujitegemea huku umasikini ukitamalaki moja ya changamoto kubwa aliyokumbana nayo bwana Lee.

Lakini changamoto hizo hazikumkwamisha mtoto huyu wa wazazi wa kichina waliyo toroka nchi yao na kwenda kuanzisha makazi mpya nje ya China huko Singapore.

Kijana huyu toka kabila la Hakka kwa kutuliza akili aliweza kuivusha nchi ya Singapore kwa udogo wake wa kila kitu na kuwa giant Asia, si Asia pekee bali duniani kwa ujumla na mataifa makubwa kama China kwenda kujifunza Singapore katika kijieneo kidogo sana.

Hakika waziri mkuu Lee alikuwa na matumizi sahihi ya kichwa chake kwa manufaa ya wasingapore.

Wakomunisti hawataweza kumkumbuka kwa mazuri bwana huyu labda kwa shingo upande maana utawala wake ulijaa ushenzi wa mkono wa chuma kwa wakomunisti waliokuwa Singapore waliokuwa kinyume na mawazo na fikra zake hakika walilambishwa shubiri.

Pamoja na yote kazi kubwa bwana huyu alifanya kuwakomboa wasingapore kutoka katika umasikini na kuishi kwa pamoja kwa upendo na leo hii duniani wanayo nafasi yao kubwa sana pamoja ya udogo wao haujawa kizuizi kwao.
a575ac68a0b347ae98f650b99fd4ac3f_t800.jpg

Moja ya kauli zao maarufu mabwana hawa
1142080-Lee-Kuan-Yew-Quote-I-am-often-accused-of-interfering-in-the.jpg
hq720 (1).jpg
 
Back
Top Bottom