Hawa: Wimbo wa 'Nitarejea' wa Diamond nauchukia sana, Umeniharibia maisha yangu

Hawa: Wimbo wa 'Nitarejea' wa Diamond nauchukia sana, Umeniharibia maisha yangu

Money Stunna

JF-Expert Member
Joined
Aug 9, 2011
Posts
13,053
Reaction score
6,304
hawa.jpg


Unakumbuka Video ya Nitarejea ya Diamond? Basi yule msichana aliyeshirikiana naye katika huo wimbo hali yake si nzuri kisanii na kimaslahi pia kisa cha kusema kuwa anauchukia huo wimbo kwani ndo umemuharibia Maisha.

Hawa akihojiwa na Mlimani TV amefunguka na kusema kuwa Pamoja na Wimbo huo kuwa ndio uliomtoa Diamond Kimuziki lakini Diamond hakuwahi kumpa Hata Shiling 10 , Japo ameshawahi kumfuata na kumuomba msaada wakati tofauti tofauti lakini haikuwezekana kupata huo msaada. Hawa amesema alitegemea nae angetoka lakini ameishia kuwa na maisha ya Dhiki huku mwenzake akitengeneza Hela za maana.

Alipoulizwa Kuhusu tuhuma za kutumia Madawa ya Kulevya baada ya kuona mambo hayaendi vizuri, Hawa amesema hakuwahi kutumia Madawa ya Kulevya bali alijiingiza katika unywaji wa pombe sana baada ya Mwanaume aliyempa Mimba Kumkimbia hivyo alianza matumizi ya pombe kupunguza Mawazo.

Hawa anasema Hamchukii Diamond ila Anapenda kumwambia akumbuke alipotoka na Arejee Nyumbani.

Chanzo: Blogs
 
Assme mimba ndio imemuharibia maisha la sio nyimbo ya nitarejea maana sion uhusiano wa kutolipwa ndio ulibikiwe maisha yako yote…!!! Mimba ndio imearibu mara baada ya kukimbiwa ila sio nyimbo na Chibu hakutoka na nymbo hiyo aache longo longo
 
Dimondi mlipe dada hawa mkwanja wake,ungemlipa hela hiyo asingebabaika na wanaume mpaka wamempa mimba,mlipe fedha zake za kolabo,ni kama Nelly na Kelly Dillema ule wimbo wote wanafaidika ila wewe unafaidika peke yako tu.
 
Alokula ndizi hakumbuki alopotupa maganda pole hawa...


Next time mtu akupe chako ndio uingie studio
 
Alie haribi maisha yake ni Hawa mwenyewe kwa kufanya maamuzi mabaya.Kapewa mimba na kijana mwingine wala sio mondi, pili alivoterekezwa akaresort kwenye madawa ya kulevya na matumizi ya pombe yalopitiliza!
Baada ya hapo alichukia jitihada gani kujikwamua? Nadhanj public sympathy haina msaada wowote.
Malipo depends na makubaliano yao halikuwaje.Underground wengi huwa wanalazimisha featuring ila watoke public bila malipo yeyote.Ila kama walikubaliana malipo Diamond alikosea sana.
 
Mm ni napenda kazi anazo fanya diamond na kila kitu kuhusu mzk wake lakini kwa hili hapa diamond amkumbuke huyo Hawa! Hayo malalamiko hayajaanza leo toka kipindi kile diamond ameenda "zizu fashion" kununua nguo na ana mkuta hawa akiwa anauza nguo huku akiimba,siku ya pili tena diamond anarudi anamkuta tena Hawa

ndipo anampenda na kuomba kufanya nae kazi Hawa bila hiyana anakubali na kufanya nae wimbo wa nitarejea wakaenda mbali zaidi wakaingia kwenye mauhusiano( kipindi kile haikuvuma coz diamond alikuwa bado hajawa diamond wa sahizi) ndipo diamond anafanya nae ngono huyu dada

,wakawa na show sikumbuki ni show gani kama sio kil.awards bas BSS kwenye mazoezi diamond alikuwa hata hampi nauli huyo dada ya kufikia mazoezini kila kitu Hawa alifanya kwa gharama zake katika maandalizi yote ya show kwenda na kurudi! Wakafanya bonge moja la show lakini Hawa hakuambulia hata sent ya malipo ya show! Ikawa kama kafanya bure hivi sijui kwann diamond alimfanyia hivyo sijui kwa vile dada alikuwa underground bado sijajua....

ikafika kpindi diamond akamuacha Hawa kimapenzi na kimziki na sahizi venyewe yupo na Zari sijui kama atakua ana mkumbuka Hawa lakini diamond kwa hili akumbuke aliko toka amkumbuke hawa tuache unafiki basi hata bila hvyo amlipe kwa kazi walio fanya hata kama ni elfu hamsini maana hawa hajaambulia chochote zaidi ya kuwa nae kimahusiano!
 
Huyo dada ni teja kitambo na hajaanza leo kuvuta unga stress tu zinamsumbua. Kama ndugu zake wamemshindwa Diamond atamsaidiaje? Dawa yake ni rehab au methadone aache upuuzi yeye kama ndio kamtoa mbona yeye haijawai kutoka ata kwa singo moja!
 
hawa nisha kutana naye kigogo jua lina waka anakata. mzinga wa konyagi. kweli kaharibikiwa. ndo safari za maisha ya wengine yanavyo enda.
 
Back
Top Bottom