Proved
JF-Expert Member
- Sep 10, 2018
- 32,639
- 42,908
Chadema walipokandamizwa na awamu ya 5 wote tulikuwa kimya tukiwaacha wateseke peke yao.Kwakweli nimechoka na siasa za bongo.
Miezi michache iliyopita Zitto Kabwe alikuwa anashambuliwa Kila Kona kwa sababu ya ruzuku. Wakamwita msaliti na matusi chungu nzima. Leo Chadema chini ya Freeman Mbowe wamechukua ruzuku na wamekausha kimyaaa. Unafiki!
Miezi michache iliyopita walimshambulia Zitto kila kona kwa kukubali kufanya kazi ya pamoja katika Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar wakamwita mnafiki akayaoga matusi mazito kabisa. Leo mgeni rasmi kwenye mkutano mkuu wa BAWACHA ni Rais Samia. Duu, huu ndio upinzani wetu.
Joe Biden wa democratic anakuwa mgeni rasmi wa mkutano mkuu wa Republican. Haijawahi tokea ni Chadema tu ndio utayaona haya maajabu. Wanachukua pesa wanasahau na malengo makuu ya upinzani.
Hongera Zitto Kabwe sasa tumewajua wanafiki halisi wa mageuzi ya Tanzania.
Leo wameridhiana na awamu ya 6 tunawalaumu kwamba ni wasaliti na kupinga hata wao kupokea ruzuku ambayo wameipokea baada ya matokeo mazuri ya maridhiano.
Hii ndio maana ya unafiki.