Elias Msuya
Platinum Member
- Dec 23, 2011
- 267
- 1,014
Julai 10 Kikundi cha Mawaziri wa Jumuiya ya Madola (Commonwealth Ministerial Action Group - CMAG) kilitoa mrejesho wa ziara ya mwakilishi wake, Dk Lazarus Chakwera aliyekuja nchini Machi 2026 kuchunguza vurugu zilizotokea katika uchaguzi wa Oktoba 29, 2026.
Katika taarifa yake, CMAG imetoa muda wa kati ya siku 30 na 90 kwa Tanzania kutekeleza masharti yanayohusu haki za binadamu, maridhiano ya kisiasa na uhuru wa kisiasa umeibua maswali makubwa kuhusu hatima ya uhusiano wa nchi hiyo na jumuiya hiyo ya kimataifa.
Miongoni mwa masharti hayo ni kuhakikisha inatatua kesi ya Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu anayeshikiliwa kwa Zaidi ya mwaka mzika kutokana na kesi ya uhaini, kutatua changamoto za uhuru wa kujieleza na vyombo vya habari na kuitisha majadiliano ya maridhiano kwa vyama vuote vya siasa.
Ingawa tamko la CMAG halijatangaza adhabu za moja kwa moja, limeweka wazi kuwa Tanzania itaendelea kubaki kwenye ajenda ya uangalizi na kwamba hatua zaidi zinaweza kuchukuliwa iwapo hakutakuwa na maendeleo ya kuridhisha kufikia mkutano wa Novemba 2026.
Kwa kuzingatia historia ya Jumuiya ya Madola, hatua hizo zinaweza kuwa na athari za kisiasa, kidiplomasia na hata kiuchumi.
Soma pia: Jumuiya ya Madola yaipa Tanzania siku 30 Kutatua suala la kushikiliwa kwa Tundu Lissu kupitia njia za kisiasa au kisheria
Shinikizo kubwa la kidiplomasia
Athari ya kwanza ni kuongezeka kwa shinikizo la kidiplomasia dhidi ya Tanzania.
Ikumbukwe kwamba Tanzania kwa sasa imeshaingia kwenye mzozo wa kidiplomasia na jumuiya kadhaa ikiwemo Jumuiya ya Ulaya, ambapo hivi karibuni Bunge lake lilipiga kura kuzuia msaada wa Euro milioni 156 uliokuwa umetengwa kwa ajili ya mpango wa mwaka 2026 wa Tanzania, kutokana na kutoridhishwa na mwenendo wa uchaguzi wa Oktoba 2025 na namna serikali ilivyoshughulikia maandamano yaliyofuata.
Pia, Tanzania inasubiri uamuzi wa Bunge la Seneti la Marekani, ambalo nalo linatarajia kujadili muswada unaohusu uhusiano kati kati ya nchi hizo mbili na endapo utapitishwa, huenda Tanzania ikatengwa na Marekani na hata kuwekewa vikwazo.
Kwa hiyo, endapo itapuuza masharti iliyiopewa na CMAG, maana yake ni kuendelea kujiweka kwenye mazingira magumu kimataifa.
Hatua ya kuendelea kuwa chini ya uangalizi wa CMAG kunamaanisha suala la Tanzania litakuwa likijadiliwa mara kwa mara na mawaziri wa mambo ya nje wa nchi wanachama. Hali hiyo inaweza kuathiri taswira ya nchi kama mwanachama anayezingatia misingi ya Jumuiya ya Madola inayojumuisha demokrasia, utawala wa sheria na heshima kwa haki za binadamu.
Kadiri muda unavyopita bila utekelezaji wa masharti, ndivyo uwezekano wa nchi nyingine wanachama kuanza kutoa matamko binafsi au ya pamoja ya kuishinikiza Tanzania unavyoongezeka.
Hatari ya kusimamishwa kushiriki shughuli za Jumuiya ya Madola
Historia ya Jumuiya ya Madola inaonyesha kuwa nchi zinazokiuka misingi yake zinaweza kusimamishwa kushiriki katika shughuli za jumuiya hiyo.
Mataifa kama Nigeria, Pakistan, Fiji na Zimbabwe yaliwahi kukumbana na hatua mbalimbali baada ya CMAG kubaini ukiukwaji wa misingi ya kidemokrasia.
Ingawa hakuna uamuzi wa aina hiyo uliotangazwa kwa Tanzania kwa sasa, iwapo hali haitabadilika, moja ya hatua zinazoweza kujadiliwa ni kusimamishwa kushiriki baadhi ya mikutano, programu na shughuli za Jumuiya ya Madola.
Hatua hiyo inaweza kupunguza ushawishi wa Tanzania katika majukwaa muhimu ya kimataifa.
Taswira ya Tanzania kwa wawekezaji
Kwa miaka kadhaa Serikali imekuwa ikijenga taswira ya Tanzania kama kitovu cha uwekezaji Afrika Mashariki.
Hata hivyo, migogoro ya kisiasa inayovutia uangalizi wa jumuiya za kimataifa mara nyingi huwa sehemu ya tathmini zinazofanywa na wawekezaji kuhusu hatari za kuwekeza katika nchi husika.
Ingawa CMAG haiwezi kuweka vikwazo vya kiuchumi moja kwa moja, taarifa zake zinaweza kuchangia kuathiri tathmini zinazotolewa na taasisi za fedha, makampuni ya bima ya uwekezaji na mashirika yanayopima mazingira ya biashara.
Matokeo yake yanaweza kuwa kucheleweshwa kwa baadhi ya uwekezaji au kuongezeka kwa gharama za uwekezaji kutokana na kuonekana kwa hatari za kisiasa.
Hivi karibuni Tanzania imepoteza fursa ya kuwa na mradi wa kiwanda cha kusafisha mafuta cha Tajiri wa Nigeria Aliko Dangote unaokadiriwa kufikia Dola za Marekani bilioni 17 (Shilingi Trilioni 2.2), ambao sasa umehamishiwa Lamu nchini Kenya.
Kama wawekezaji Zaidi hawatakuja Tanzania, huenda uchumi wake utaendelea kuporomoka.
Mahusiano na wafadhili wa maendeleo
Nchi nyingi wanachama wa Jumuiya ya Madola pia ni wafadhili wakubwa wa Tanzania kupitia misaada ya maendeleo na miradi mbalimbali.
Iwapo wasiwasi kuhusu utawala wa sheria na haki za binadamu utaendelea kuongezeka, baadhi ya washirika wa maendeleo wanaweza kuanza kupitia upya namna wanavyotoa misaada yao, hasa ile inayohusisha utawala bora, haki na taasisi za kidemokrasia.
Si mara zote hatua hizo huchukua mfumo wa kusitisha misaada, lakini zinaweza kujumuisha masharti mapya, kuongeza ufuatiliaji wa matumizi ya fedha au kuelekeza fedha zaidi kwa asasi za kiraia badala ya taasisi za serikali.
Kuathiri ushawishi wa Tanzania kikanda
Kwa muda mrefu Tanzania imekuwa ikijijengea heshima kama taifa lenye mchango mkubwa katika amani na upatanishi barani Afrika.
Imehusika katika juhudi mbalimbali za kutafuta amani katika nchi za ukanda wa Maziwa Makuu na Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC).
Hata hivyo, nchi inayokabiliwa na ukosoaji mkubwa kuhusu masuala ya demokrasia inaweza kujikuta ikipoteza uzito wa kisiasa inapojaribu kushauri mataifa mengine kuhusu utawala bora na maridhiano.
Athari kwa wananchi
Iwapo mvutano kati ya Serikali na Jumuiya ya Madola utaendelea, athari zake zinaweza kuonekana pia kwa wananchi kupitia kupungua kwa fursa zinazotolewa chini ya programu za Jumuiya ya Madola katika maeneo ya elimu, mafunzo, vijana, utawala wa sheria na maendeleo ya taasisi.
Aidha, mazingira ya kisiasa yanayoendelea kuwa na mvutano yanaweza kuathiri shughuli za kiuchumi na kijamii ndani ya nchi.
Serikali ina nafasi ya kuepusha mgogoro
Pamoja na tahadhari zilizotolewa, tamko la CMAG linaonyesha kuwa mlango wa mazungumzo bado uko wazi.
Masharti yaliyowekwa yanatoa fursa kwa Serikali kuonyesha hatua za utekelezaji kabla ya Septemba na Novemba 2026.
Iwapo hatua hizo zitachukuliwa na kuridhisha Jumuiya ya Madola, Tanzania inaweza kuepuka hatua kali zaidi na kurejesha imani ya washirika wake wa kimataifa.
Lakini ikiwa hakutakuwa na maendeleo yanayoonekana, nchi inaweza kukabiliwa na ongezeko la shinikizo la kidiplomasia, kudhoofika kwa taswira yake kimataifa na uwezekano wa hatua zaidi kutoka Jumuiya ya Madola, ambazo zinaweza kuwa na athari za muda mrefu kwa diplomasia, uchumi na nafasi yake katika jumuiya ya kimataifa.