Haya Kombe la Dunia hilo linakuja tuanze sasa kugawana Timu za Kushabikia mapema

Mkuu, tatizo wewe unadhani labda kila mtu ni lazima ashabikie timu kubwa.

Unabaki mdomo wazi kisa nini?

Mimi naishabikia kwa mapenzi kutoka moyoni na siyo kufuatana mkumbo km nyie kila mtu Germany Germany Germany...

Sawa Baba yameisha!
 
Mkuu, kuishabikia timu hakuhusiani kabisa na kujua mpira. Ushabiki unaendana na mapenzi na hisia kutoka moyoni.

Uchambuzi wa soka ndiyo unaendana na ujuzi/elimu ya soka.

Shikamoo Mkuu.
 

Wewe lazima tu utakuwa unajua Mpira halafu pia umeucheza vile vile. Mpaka sasa bado namuwazia na simpatii Picha huyu Member aliyenitajia Saudi Arabia. Yaani Mwarabu aache Kujivisha Mabomu ya Kujilipua acheze / asakate mpira kweli? Kama kuna Timu ambayo natabiri mapema itarudi Kwao na Zawadi la Kapu la Magoli / Mabao ya Kufungwa huko Urusi katika Fainali za Kombe la dunia basi ni Saudi Arabia. Halafu wako katika Kundi baya sana lenye Timu zenye roho mbaya tupu katika Kandanda.
 
Una uhakika kabisa kwamba Bange / Bangi uliyoivuta leo ilikuwa sahihi kwa matumizi kamili ya Mwanadamu Mkuu?
Yeah... Simba wananyakua UCL... piga ua. Liverpool lazima wakamate kombe la dunia.... Barca wanakamata EURO na Mabwe guys wanakamata VPL...

Mi ntakuwa natibu maumivu ya watakaokuwa wanaumia na matokeo
 
mi nashabikia spain......ila pia nashabikia saudi arabia naomba tu ipite kwe makundi na iran apite kwe kundi lake wakutane itakua bonge la burudani dadeki
 
TIMU ZA KIAFRIKA AMBAZO KUTOKANA NA MAKUNDI WALIYOMO BASI NINA UHAKIKA KWA ASILIMIA 100% KUWA ZITATOLEWA KATIKA HATUA YA MAKUNDI NI:

1) NIGERIA
2) TUNISIA
3) MOROCCO


TIMU ZA KIAFRIKA AMBAZO ZIKIKAZA KIDOGO TU KALINGANA NA MAKUNDI WALIYOMO BASI WATATOBOA NI:

1) EGYPT
2) SENEGAL


Mimi Ni Mshabiki Wa ENGLAND Lakini Sitegemei Hata Kuvuka Robo Fainali.

But ingawa Ninazichukia GERMANY na BRAZIL ukweli utabakia kuwa Ndiyo Timu Pekee Hizi Zenye Nafasi Kubwa Ya Kuchukua Ubingwa.

Na ARGENTINA kama Kawa Wataingia RUSSIA wakiamini Kuwa na MESSI Ndiyo Kushinda Kila Kitu hatimae Watajikutia Wanarudi Kwao Kila Mtu Kwa Ndege Yake.

Ukweli Usiofichika HITLER Kwenye Soka Katuachia Kizazi Chenye Roho Mbaya Kama Yeye.
 
Kweli wewe uliwahi kukipiga, sisi wengine ukituletea kwenye mguu utangonga katika ugoko kisha utapiga katika kidevu habari itaishia hapo, wazazi walituzuia kucheza michezo ya kipuuzi, walisema ''mpira utakufikisha wapi?''.
 
Mtu yoyote anayeshabikia England hajui kabisa Mpira. Samahani kama nitakuwa nimekuudhi / nimekukwaza kwa hili Mkuu.
Mkuu, swali lilikuwa kuchagua timu tunazoshabikia, au timu tunazohisi zitafanya vizuri?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…