Form One hadi Form Four nilikuwa Mchezaji wa Kutumainiwa kabisa wa Timu ya Shule hapo nchi jirani tu ambako UKIMWI ulizinduliwa rasmi na Hayati Philemon Lutaya na nilicheza hadi katika Mashindano ya Shule makubwa huku mnayaita UMISETA na nilikuwa nikicheza sana nafasi za Beki wa Kulia au Kushoto ila nilipofika Kidato cha Tano kwenda cha Sita kutokana na aina ya Shule niliyokuwepo tulibahatika kuwa na Kocha wa Kizungu ambaye pia alikuwa ni Mwalimu wetu na alinibadilisha kutoka Kucheza nafasi ya Beki wa Kulia na Kushoto na sasa akanitengeneza hadi nikawa nacheza Kiungo cha chini ( yaani namba Sita ) na nakumbuka wakati huo nilikuwa nawaiga sana Marafiki zangu wachezaji mahiri wa Kibongo wakati huo Selemani Matola ' Veron ' na Waziri Mahadhi ' Mendieta ' uchezaji wao na nilitokea Kukubalika mno na Wanafunzi wenzangu hadi na Raia waliokuwa wakiniona nikicheza na nakumbuka hata katika hizo Shule zote nilikuwa napendwa na Mademu kwakuwa nilikuwa ' nakichafua / nakipiga ' sana dimbani Mkuu.
Niliachana na Mpira rasmi baada ya kumaliza Kidato cha Sita na kutingwa zaidi na ratiba zingine za Kitaaluma japo hata wakati nilipokuwa Chuo Kikuu nilijaribu Kucheza lakini sikuweza tena kuwa vizuri kama enzi zangu kwakuwa Mpira wangu mwingi nilipokuwa Chuoni nilikuwa nauchezea sana Gesti / Loji huku Waamuzi / Marefarii wakiwa ni Wahudumu wa hizo Nyumba za Kulala Wageni nilizokuwa nikiingia.
Kwa sasa huwa nikipata muda najaribu kucheza kidogo pale Leaders Club na akina Bakari Malima ' Jembe Ulaya ', Ally Yusuph ' Tigana ', Mtwa Kihwelo ' Dally Kimoko ' na Omary Kapilima ' Caminero ' au pande za Tanganyika Packers Kawe na akina Omary Mkuku, Kudra Omary na Benito John ila siko ' active ' kivile kwakuwa Kasi ya Vyuma Kukaza Kimasha sasa imeongezeka hivyo ' Mbichwa ' wangu muda wote unawaza nitawezaje kuielewa Kasi na hii Falsafa ya Maisha ya Rais JPM.
Ni hayo tu Mkuu.